Kwa wanaofahamu naomba mnisaidie

musajohn58

Member
Oct 28, 2014
34
8
Mke wangu alikuwa na ujauzito wa miezi 8 lakini cha kushangaza ilitokea tarehe 26 December akaanza kutokwa damu tu na tumbo kumuuma sana ndipo tulipoenda hospital kupata msaada ila sikuamini masikio yangu nilipoambiwa na doctor kuwa mtoto kafia tumbon ndipo doctor alifanya utaratibu wa kumtoa na akatoka kwa njia ya kawaida.

Doctor nilimuuliza sababu ya yule mtoto kufia tumbon hakunijibu chochote zaidi aliniambia ni Bahati mbaya tu,

Mke wangu aliendelea vyema na tukarejea nyumban, baada ya siku 6 mke wangu alianza kuhisi ganzi kwenye lips ya mdomo wa juu na kichwa kuuma ila anasema kuna mshipa unavuta kuanzia mgongoni kupitia uti wa mgongo hadi kichwani ndio anahisi kichwa kumuuma,

pia ganzi imefika hadi mdomo wa chini anavyosema, tumeenda kwa doctor akatuambia ni areji tu ambayo ameipata kipindi cha kusukuma mtoto akatupa dawa lakini bado analalamika tatizo liko palepale, jaman mwenye uzoefu naomba anisaidie.
 
Pole sana mkuu... ngoja wataalamu waje hii tatizo imemtokea ndugu yangu juzi kati tu
 
Back
Top Bottom