Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
Hahaha mbu wachawi wa zamani wangeona haya kumtoa kikoa 'mtoto ulokabidhisha Ila wachawi wa sasa wanaona ndo wamerahisishiwa njia. Sikushauri kufanya hivyo hata kidogo
...Gaijin, heri ya nusu shari kuliko shari kamili. Mume utasaidiwa tu. Mfano; kama bajeti haitoshi Mpe pesa mkeo uone kama kapu halitarudi limejaa.
Heri lifti ya lifti niijuayo, hata akiiba ataibia kiuoga uoga.
Kwanza, mimi ningemwambia mke wangu sitaki kusikia tena habari za huyo jamaa - mkarimu n.k. je, kabla ya lifti alimkirimia nini? Lunch? Pili, kama mke wangu atataka hiyo lifti basi ahamie kwa huyo jamaa mpaka mwisho wa maisha yake duniani ili aweze kufaidi hiyo lifti vizuri.
...dah, una wivu sana wewe. Unaweza pata magonjwa ya BP na kisukari siku si zako.
tatu, nikigundua wanapeana lifti bila mimi kujua nitamchukua mke wangu na kujifanya kumtembelea huyo jamaa nyumbani kwake na kumwacha huko mke wangu - yaani kumkabidhi kwa huyo bwana. Nne, wanawake wengi upenda magari aidha kumiliki au lifti.
...dah! unakwenda kuhalalisha kabisaaaa? hehehehe... busara na UAMINIFU vimepotelea wapi jamani, humuamini mkeo hata kidogo?
Na mwisho, ni wote wawili ni kuka chini na kutafuta la kwenu kama si ya kwenu; maanake kama anatamani gari, lazima atatamani na vingine!!! Mwisho kabisa wake wanatakiwa kuangaliwa na kuelekezwa na waume zao kama mzazi anavyomwelekeza mwanaye!!!!!!!
...hii ndio busara bana, sio kumtelekeza kwakua kapewa lifti. Usafiri wa daladala mjini shida mzee! :coffee: