Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Wapendwa wanaJF ambao mmefunga pingu za maisha, vipo 'vijimambo' vidogo vidogo ambavyo wanandoa wanaviacha au kuvipuuzia na hatimaye kukuta upendo mliokuwa nao tangu mwanzo wa ndoa yenu graph yake inashuka siku hadi siku. Hapa nimetumia neno 'vijimambo' kwa sababu havionekani kwamba ni vya maana sana! Kumbuka hapa nazungumzia ndoa takatifu, sio ukimada!
Nianze na mfano ufuatao: "Priscilla na Michael walioana kwa muda mrefu, lakini upendo wao wa mwanzo ulizidi kuporomoka na waligombana mno kila siku mpaka walifikia mahali pa kunyimana hadi unyumba. Priscilla alidai baadaye kwamba 'hajisikii' tena kumpenda Michael. Mwanzo wa ndoa yao walielewana sana, maneno kama 'sorry honey', 'I love you,' 'I miss you', nk yalikuwa hayaishi midomoni.
Siku moja Priscilla alienda kwa Buchanan kuomba ushauri ili atafute namna ya kuachana na Michael! Buchanan alimshauri kwamba njia nzuri ya kumwacha ni hii ifuatayo: amfanyie mambo mazuri sana ndani ya wiki mbili, mambo hayo yawe ni yale ambayo hajawahi kumfanyia. Haijalishi kwamba Michael tabia yake imebadilika au la. Baada ya wiki mbili, ndipo amwambie kwamba anamwacha Michael.
Kweli Priscilla alipokea ushauri na kuamua kuufanyia kazi. Na kwa wakati huo Michael alishaanza tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani na mara nyingine alilala kusikojulikana! Baada ya Wiki moja ya Priscilla kumkaribisha vizuri, kumwogesha, kutokula chakula eti mpaka mume wake arudi, kumsimulia matukio ya siku ile, kumwomba msamaha kwamba eti hakusikia wakati anaingia, nk tabia ya Michael ilianza kubadilika ghafla.
Baada ya wiki mbili Priscilla alienda kumwona Buchanan kama walivyokubaliana kwamba waonane ili kumjulisha kama wameshaachana. Walipoonana Buchanan alimuuliza kama walishaachana na Michael, lakini Priscilla alimwambia maneno machache: 'I have fallen in Love with Him Again, kwa hiyo siwezi kumwacha, ngumu sana kumwacha.' Ndivyo Buchanan alivyookoa ndoa ya Priscilla na Michael!"
Ushauri: Wanandoa msisahau 'vijimambo' katika ndoa, vitaifanya ndoa yenu ionekanae mpya kila siku! Usisubiri u-fall in love out of nothing! Hiyo itakuwa ni tamaa ya mwili ambayo inakuwepo kwa kitambo tu na baadaye inatoweka. Acha hisia za mwili ziletwe na 'matendo mazuri' yaani 'vijimambo!' Honeymoon forever! Have a great day!