Kwa wana ndoa na wanaotarajia kuingia ndoani

Kwa wana ndoa na wanaotarajia kuingia ndoani

Siku zote mila na desturi zetu pamoja zinatufundisha na kusisitiza maadili kama sehemu ya kujenga jamii iliyostaarabika.

Baada ya kutumia mitandao hasa jf kupitia jukwaa hili la MMU nimegundua kuna tabia inapandikizwa kutoka kwa watu ambao hatujui ni wa namna gani nje ya hapa.

Michango mingi ya members humu inaonesha kukinzana na maadili tuliyokulia na kufundishwa kama vile uasherati na zinaa.

Michango inayotolewa humu ni jinsi ya kupata mwanamke wa kulala naye au kuharibu ndoa za watu kwa kutembea na waume na wake zao.

Hakuna mijadala inayoweza kuwapa uelewa vijana pengine jinsi ya kujiandaa na majukumu ya kifamilia baada ya uchumba, au namna ya kuboresha mahusiano ya ndoa, badala yake watu wanafundishana jinsi ya kuharibu kwa ajili ya tamaa za mwili.

Akili za watu waliokuwa wanaamini kuwa ZINAA UASHERATI ni dhambi sasa zimechafuliwa na mashauri ya watu na sasa hawaoni ni shida kulala hata mke au mume wa mtu!!!!

Mmomonyoko huu wa maadili ndio unazitesa familia nyingi, wazazi wakitengana huku watoto wakibaki bila uangalizi jambo ambalo linaendeleza uharibifu.

Nawashauri watu mmbadilike, mkumbuke kuwa mnayoyaandika haya hayatafutika na yatakuja kusomwa na kizazi cha baadae.

Mtu mzima unaandika upumbavu huku ukijua mitandao inasomwa hadi na watoto wa miaka 15!!!!

Tumieni muda wenu kujenga ndoa na mipango ya ndoa na sio kubomoa na kupindisha rafsiri/maana za maneno.

Kama wewe ni mcha MUNGU na unaamini kuwa Uasherati na Zinaa ni dhambi(machukizo) kwa MUNGU kwanini usiwe wa kwanza kukemea hizo dhambi?

Leo hata ngono kupitia haya kubwa sio dhambi tena bali sifa na ujanja! unaelekea wapi rafiki?

Badilika, ulikuja peke yako hapa jf na ipo siku utaondoka peke yako, unayoyaandika hapa yatakuwa ushahidi siku zako za usoni.

Mkuu asante kwa kutukumbusha wajibu wetu kama watu wazima humu jamii forum

Mkuu wewe ni member wa humu hjamii forum umekuwa ukiona kero mbali mbali au ideolody mbovu zinazopandikzwa humu

Je wewe huwa unatoa michango positive? Kiasi gani?
Kabla ya kulalamika ni vema usiwe unakaa kimya mkuu, anza wewe kuwa mfano wa kutoa michango chanya na kutoa

Kumbuka kwamba jf kuna watu wa aina nyingi mno, kuna watu wapo kwa ajili ya jokes, kuna watu wanatumia jf kama sehem ya kurelax, kuna watu wanatumia kama sehemu ya kueneza mawazo yao potofu...


Hayo yote hayaepukiki kabisa ca msingi ni kutumia akil sio kuiga kila kitu
 
Pesa ni ya kawaida sana haiwezi kunipa furaha ya namna ile aise...hebu sote wawili tupeane muda kutafakari hiyo furaha inasababishwa na nini,tusaidiane ati.

Khaaa........ mkubwa haya!!!! Furaha yako wewe niitafakari mim dah!!!!

Hili litakuwa ajabu la 8 la dunia.

Lakini heri kama unafuraha maana uongeza baraka.
 
Hayo mambo ya 50000 za samaki samaki hakiamungu ukipata demu anaechuna hv wiki 2 tunakuzika kwa stress

Jamani sasa hapo umechunwa au umesadia kumfurahisha demu?? Ukiwa na dem hakikisha ana furaha muda wote
 
Back
Top Bottom