Kwa wana ndoa na wanaotarajia kuingia ndoani

Wisest man

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
993
Reaction score
333
Siku zote mila na desturi zetu pamoja zinatufundisha na kusisitiza maadili kama sehemu ya kujenga jamii iliyostaarabika.

Baada ya kutumia mitandao hasa jf kupitia jukwaa hili la MMU nimegundua kuna tabia inapandikizwa kutoka kwa watu ambao hatujui ni wa namna gani nje ya hapa.

Michango mingi ya members humu inaonesha kukinzana na maadili tuliyokulia na kufundishwa kama vile uasherati na zinaa.

Michango inayotolewa humu ni jinsi ya kupata mwanamke wa kulala naye au kuharibu ndoa za watu kwa kutembea na waume na wake zao.

Hakuna mijadala inayoweza kuwapa uelewa vijana pengine jinsi ya kujiandaa na majukumu ya kifamilia baada ya uchumba, au namna ya kuboresha mahusiano ya ndoa, badala yake watu wanafundishana jinsi ya kuharibu kwa ajili ya tamaa za mwili.

Akili za watu waliokuwa wanaamini kuwa ZINAA UASHERATI ni dhambi sasa zimechafuliwa na mashauri ya watu na sasa hawaoni ni shida kulala hata mke au mume wa mtu!!!!

Mmomonyoko huu wa maadili ndio unazitesa familia nyingi, wazazi wakitengana huku watoto wakibaki bila uangalizi jambo ambalo linaendeleza uharibifu.

Nawashauri watu mmbadilike, mkumbuke kuwa mnayoyaandika haya hayatafutika na yatakuja kusomwa na kizazi cha baadae.

Mtu mzima unaandika upumbavu huku ukijua mitandao inasomwa hadi na watoto wa miaka 15!!!!

Tumieni muda wenu kujenga ndoa na mipango ya ndoa na sio kubomoa na kupindisha rafsiri/maana za maneno.

Kama wewe ni mcha MUNGU na unaamini kuwa Uasherati na Zinaa ni dhambi(machukizo) kwa MUNGU kwanini usiwe wa kwanza kukemea hizo dhambi?

Leo hata ngono kupitia haya kubwa sio dhambi tena bali sifa na ujanja! unaelekea wapi rafiki?

Badilika, ulikuja peke yako hapa jf na ipo siku utaondoka peke yako, unayoyaandika hapa yatakuwa ushahidi siku zako za usoni.
 
Ungeweka na mifano
sijawahi kuona threads hapa watu wakishawishi watu hayo unayoyasema
labda weka link....au labda kuna kutoelewa hizo threads
 
Zipo nyingi tu, wewe angalia zilizoko MMU na maudhui yake halafu u-balance na hii story.
 
Fata huu msemo "za kuambiwa changanya na zako"
then mind business zako, hicho unachokitaka wewe hakiwezekani unadhani humu watu wote akili zipo sawa?
ukiharibu ndoa yako kwa comments za humu hiyo ni ujinga yako usitusingizie
 
ni kweli unayosema ila jf hutakiwi kuchukua kila ushauri unaopewa
 
Fata huu msemo "za kuambiwa changanya na zako"
then mind business zako, hicho unachokitaka wewe hakiwezekani unadhani humu watu wote akili zipo sawa?
ukiharibu ndoa yako kwa comments za humu hiyo ni ujinga yako usitusingizie

Kama unajua haiwezekani kwanini uone inawezekana mimi kufuata misemo ya watu kama ulivyoshauri?

Wewe ulitakiwa kuwa mfano wa "mind your own business" kwa kutokuchangia kama unadhani kwangu inawezekana.
 
Kwanini nisichangie wakati dhumuni la kuwa kwenye social network ni kusocialize?
nna kitu cha kushare I shere haijalishi ni cha aje, watu wame post nnacheka naondoa stress, ushauri unaofaa nachukua usiofaa nawaachia wenyewe mwisho wa siku "za kuambiwa changanya na zako"
hatufanani tabia hatuwezi kua sawa
 
tumblr_inline_nqqfpnE8DF1txzj31_500.gif
 
Kwanini nisichangie wakati dhumuni la kuwa kwenye social network ni kusocialize?
nna kitu cha kushare I shere haijalishi ni cha aje, watu wame post nnacheka naondoa stress, ushauri unaofaa nachukua usiofaa nawaachia wenyewe mwisho wa siku "za kuambiwa changanya na zako"
hatufanani tabia hatuwezi kua sawa

Yaani povu limekutoka kwa kuwa na wewe ni mmoja wa waliozungumziwa hapa, teh teh teh teh teh.
 
Siku zote mila na desturi zetu pamoja zinatufundisha na kusisitiza maadili kama sehemu ya kujenga jamii iliyostaarabika.

Baada ya kutumia mitandao hasa jf kupitia jukwaa hili la MMU nimegundua kuna tabia inapandikizwa kutoka kwa watu ambao hatujui ni wa namna gani nje ya hapa.

Michango mingi ya members humu inaonesha kukinzana na maadili tuliyokulia na kufundishwa kama vile uasherati na zinaa.

Michango inayotolewa humu ni jinsi ya kupata mwanamke wa kulala naye au kuharibu ndoa za watu kwa kutembea na waume na wake zao.

Hakuna mijadala inayoweza kuwapa uelewa vijana pengine jinsi ya kujiandaa na majukumu ya kifamilia baada ya uchumba, au namna ya kuboresha mahusiano ya ndoa, badala yake watu wanafundishana jinsi ya kuharibu kwa ajili ya tamaa za mwili.

Akili za watu waliokuwa wanaamini kuwa ZINAA UASHERATI ni dhambi sasa zimechafuliwa na mashauri ya watu na sasa hawaoni ni shida kulala hata mke au mume wa mtu!!!!

Mmomonyoko huu wa maadili ndio unazitesa familia nyingi, wazazi wakitengana huku watoto wakibaki bila uangalizi jambo ambalo linaendeleza uharibifu.

Nawashauri watu mmbadilike, mkumbuke kuwa mnayoyaandika haya hayatafutika na yatakuja kusomwa na kizazi cha baadae.

Mtu mzima unaandika upumbavu huku ukijua mitandao inasomwa hadi na watoto wa miaka 15!!!!

Tumieni muda wenu kujenga ndoa na mipango ya ndoa na sio kubomoa na kupindisha rafsiri/maana za maneno.

Kama wewe ni mcha MUNGU na unaamini kuwa Uasherati na Zinaa ni dhambi(machukizo) kwa MUNGU kwanini usiwe wa kwanza kukemea hizo dhambi?

Leo hata ngono kupitia haya kubwa sio dhambi tena bali sifa na ujanja! unaelekea wapi rafiki?

Badilika, ulikuja peke yako hapa jf na ipo siku utaondoka peke yako, unayoyaandika hapa yatakuwa ushahidi siku zako za usoni.

Tangu uzaliwe leo umeongea KITU cha Maana sana.
 
Hivi unafaham hili ni jukwaa gani na hapa sio madrasa wala sundy skuli?
 
Back
Top Bottom