Wakati tunapowasilisha mada hasa zile zenye mwelekeo wa kukosoa utawala uliopo mara nyingi hujitokeza maoni kwamba kwa nini na yale mazuri hayasemwi. Inategemea . Binadamu kwa kawaida hukusudia kupeleka ujumbe fulani pale anapoandika lolote. Hata mada hii imejielekeza kwenye UPANDE WA KUANGALIA YALE AMBAYO MWANDISHI ANADHANI YANAHITAJI KUPATIWA MAJIBU NA YUMKINI WAKO WATAKAOHOJI.
Leo napenda kuwauliza wana CCM walio huru kimawazo (Free thinkers) kuhusu mambo kadhaa .
Kwanza ni mwenendo wa utawala wa rais Magufuli kwenye maeneo yafuatayo.
Hali ya siasa na uhasama uliopo
Baina ya viongozi wa serikali na wapinzani. Kwamba tumeshuhudia mbinyo uliozaa sokomoko kubwa kutokana na kubanwa demokrasia na uhuru wa kisiasa. Bila shaka jambo hili linaashiria kupoteza umoja wetu na kujenga chuki. Mnadhani ilikuwa ni lazima itumike njia hii ya sasa ili Raius aliyepo na serikali yake ndio aweze kufikia malengo ? Unafikiri Rais na utawala wake wako sawa kweli ?
Hali ya uchumi wetu na ajira.
Hatutaki hapa utetezi wa kisiasa. Unadhani hali ya maisha ya watu wengi kuwa wanalalamikia maisha ni kutokana na kutojituma au ni kwamba fursa za kibiashara , mazingira ya biashara, ukata, na mengineyo yamechangia ? Kwa nini watu wengi wanalalamika sana ?
Suala la ajira . Nafasi za uajiri ni chache kwa mashirika binafsi na serikalini hazitoshi. Kwa nini ajira binafsi zimekuwa haba, na kwa nini mashirika na makampuni yanaendelea kupunguza wafanyakazi na mengine kufunga ofisi. Mnafikiri hakuna tatizo lolote?
Kwa nini hata serikalini kuna malalamiko ya wafanyakazi kutopandishwa madaraja na mishahara kwa kipindi kirefu?
Diplomasia yetu
Hili ni eneo ambalo nalo limeporomoka kwa kasi ndani ya utawala wa Rais Magufuli. Mnadhani diplomasia yetu inapaswa kwenda hivi hali ya sasa ilivyo kwa maslahi ya Tanzania au kuna njia nyengine ingefaa?
Kweli kiini cha kuporomoka kwa diplomasia ni uzalendo au kukosa mbinu tu za kushughulikia mambo yanayojitokeza?
Mtikisiko wa amani yetu , vifo na watu kupotea.
Hili kweli linawafurahisha au kuhuzunisha?
Ikiwa hayo tuliyosema yanatokea, jee watu wako sahihi kuilaumu serikali au alaumiwe nani ? Kwa mfano mauaji ya kibiti, watu kupotezwa bila majibu na watu kushambuliwa bila wahusika kukamatwa au jitihada za kuwakamata kufifia mnadhani serikali haipaswi kulaumiwa ?
Watu kukosa furaha na malalamiko.
Katika utawala huu ni wazi kuna ongezeko kubwa la watu kukosa furaha na kulalamika. Wengine wanalalamika mitandaoni, wachache bungeni, wachache kwenye hadhara za wazi ambazo ni chache mno kuziona na wengi wanalalamika mioyoni. Huu ni ukweli. Mnadhani hali hii ni njema kwa Taifa?
Wafanyakazi serikalini wanalalamika, wafanyabiashara na wawekezaji wanalalamika, wanasiasa wanalalamika, wanadini wanalalamika na kukosoa. Hali hii inawafurahisha kama watanzania ?
Mwisho.
Mambo ni mengi na sio kusudio la mtoa mada kuandika maelezo mengi.
Kwa ufupi nyinyi wana CCM mlio huru mnafurahishwa na mwenendo wa mambo yalivyo leo ndani ya miaka 3 ya utawala wa Rais Magufuli na kwa nini ? Tafadhalini jielekezeni katika maeneo yaliyotolewa ufafanuzi hapo juu na kwa kuzingatia sheria zetu, utamaduni wetu na ustaarabu wetu.
Na Mwisho kabisa mnadhani nini kifanyike ili kurejesha utengamano uliokuwepo kabla kwa maslahi ya Taifa ?
Kishada.