Kwa wana CCM walio huru kimawazo, Hali hii kweli inawafurahisha ?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Wakati tunapowasilisha mada hasa zile zenye mwelekeo wa kukosoa utawala uliopo mara nyingi hujitokeza maoni kwamba kwa nini na yale mazuri hayasemwi. Inategemea . Binadamu kwa kawaida hukusudia kupeleka ujumbe fulani pale anapoandika lolote. Hata mada hii imejielekeza kwenye UPANDE WA KUANGALIA YALE AMBAYO MWANDISHI ANADHANI YANAHITAJI KUPATIWA MAJIBU NA YUMKINI WAKO WATAKAOHOJI.

Leo napenda kuwauliza wana CCM walio huru kimawazo (Free thinkers) kuhusu mambo kadhaa .

Kwanza ni mwenendo wa utawala wa rais Magufuli kwenye maeneo yafuatayo.

Hali ya siasa na uhasama uliopo
Baina ya viongozi wa serikali na wapinzani. Kwamba tumeshuhudia mbinyo uliozaa sokomoko kubwa kutokana na kubanwa demokrasia na uhuru wa kisiasa. Bila shaka jambo hili linaashiria kupoteza umoja wetu na kujenga chuki. Mnadhani ilikuwa ni lazima itumike njia hii ya sasa ili Raius aliyepo na serikali yake ndio aweze kufikia malengo ? Unafikiri Rais na utawala wake wako sawa kweli ?

Hali ya uchumi wetu na ajira.

Hatutaki hapa utetezi wa kisiasa. Unadhani hali ya maisha ya watu wengi kuwa wanalalamikia maisha ni kutokana na kutojituma au ni kwamba fursa za kibiashara , mazingira ya biashara, ukata, na mengineyo yamechangia ? Kwa nini watu wengi wanalalamika sana ?

Suala la ajira . Nafasi za uajiri ni chache kwa mashirika binafsi na serikalini hazitoshi. Kwa nini ajira binafsi zimekuwa haba, na kwa nini mashirika na makampuni yanaendelea kupunguza wafanyakazi na mengine kufunga ofisi. Mnafikiri hakuna tatizo lolote?

Kwa nini hata serikalini kuna malalamiko ya wafanyakazi kutopandishwa madaraja na mishahara kwa kipindi kirefu?

Diplomasia yetu
Hili ni eneo ambalo nalo limeporomoka kwa kasi ndani ya utawala wa Rais Magufuli. Mnadhani diplomasia yetu inapaswa kwenda hivi hali ya sasa ilivyo kwa maslahi ya Tanzania au kuna njia nyengine ingefaa?

Kweli kiini cha kuporomoka kwa diplomasia ni uzalendo au kukosa mbinu tu za kushughulikia mambo yanayojitokeza?

Mtikisiko wa amani yetu , vifo na watu kupotea.

Hili kweli linawafurahisha au kuhuzunisha?
Ikiwa hayo tuliyosema yanatokea, jee watu wako sahihi kuilaumu serikali au alaumiwe nani ? Kwa mfano mauaji ya kibiti, watu kupotezwa bila majibu na watu kushambuliwa bila wahusika kukamatwa au jitihada za kuwakamata kufifia mnadhani serikali haipaswi kulaumiwa ?

Watu kukosa furaha na malalamiko.

Katika utawala huu ni wazi kuna ongezeko kubwa la watu kukosa furaha na kulalamika. Wengine wanalalamika mitandaoni, wachache bungeni, wachache kwenye hadhara za wazi ambazo ni chache mno kuziona na wengi wanalalamika mioyoni. Huu ni ukweli. Mnadhani hali hii ni njema kwa Taifa?
Wafanyakazi serikalini wanalalamika, wafanyabiashara na wawekezaji wanalalamika, wanasiasa wanalalamika, wanadini wanalalamika na kukosoa. Hali hii inawafurahisha kama watanzania ?

Mwisho.

Mambo ni mengi na sio kusudio la mtoa mada kuandika maelezo mengi.

Kwa ufupi nyinyi wana CCM mlio huru mnafurahishwa na mwenendo wa mambo yalivyo leo ndani ya miaka 3 ya utawala wa Rais Magufuli na kwa nini ? Tafadhalini jielekezeni katika maeneo yaliyotolewa ufafanuzi hapo juu na kwa kuzingatia sheria zetu, utamaduni wetu na ustaarabu wetu.

Na Mwisho kabisa mnadhani nini kifanyike ili kurejesha utengamano uliokuwepo kabla kwa maslahi ya Taifa ?

Kishada.
 
watu hawako CCM eti kwakua wanaipeeenda CCM lahasha, wengi wao ni ma opportunist, wachimia tumbo kwa lugha nyepesi. Wako huko kuvizia nafasi za uongozi maana ndio njia rahisi zaidi ya kutajirika hapa nchini.
 
Mimi nilikuwa nakipenda sana Chama Cha Mapinduzi,mpaka awamu hii ilipoingia nikaanza kuona uvunjifu mkubwa wa Haki za Watanzania.
Nilikuwa na Group langu kubwa la kampeni ila kwa sababu Wapinzani nao ni Ndugu zangu Watanzania nikasema NO!..mipango mingi ya kununua na kuwatisha wapinzani nikaona we're Sleepwalking in to a Civilwar and One man rule.

Nimehama CCM tokea November 2018 nimehamia Upinzani niligundua mbinu nyingi za Kuwalisha Sumu viongozi wa Upinzani Lowassa ni Mmojawapo Ninamshauri Fred Lowassa akampime mzee wake,tokea nihamie upiinzani nimewashauri viongozi kadhaa,na najisikia niko free.
 
Wakati huu wa mpito haya yote hayana budi kutokea kwani nchi ilioza na sasa inasafishwa!
 
Haa haa haa:oops::oops::oops:, bro...kusafisha nchi ndo kuhusishe mpaka watawala kuua watu????

Hoja yako ingekuwa na maana na kukubalika kwa kiasi fulani iwapo usafishaji huu ungehusisha yote hayo mengine...

Lakini kwa mauaji ya kisiasa yanayoendelea hai - justify hata chembe hoja yako ya utetezi na malengo ya serikali ya awamu ya tano chini ya Pombe Magufuli zaidi ya kuthibitisha kuwa ipo nia ovu zaidi nyuma ya mbinu hii ya kiutawala!!

Na nia hii ovu kamwe haiwezi kuwa ni kuisukuma mbele Tanzania kimaendeleo, bali kuirudisha nyuma.
 
Hakuna mwanaccm mwenye mawazo huru , wote wastaafu na wa sasa wako kama mwanamke aliyeingia kwenye ndoa baada ya kufumaniwa ( ndoa ya mkeka ) , ukifanya uchunguzi utagundua mwanamke wa namna hawezi kuwa na kauli wala mawazo huru , anachopanga mumewe ndio hicho hicho

Sijui nikupe mfano gani ili unielewe , kwa ujumla ni afadhali hata mtumwa kuliko mwanaccm
 
Mfano wako ni dhahiri!..Mimi nikiwatazama viongozi wengi naona kama wanasubiri nguvu ya Mungu tu ili warudi utawala uliopita.Hawaonekani kuwa huru wanapoongea!
 
Mkuu hapa wata kwambia kuwa wewe sio Mzalendo ,usifie kila kitu kinacho fanywa na Awamu hii.Hata tukitaka kwenda kuwa kong'oli Shangazi zako wewe Sifia tu...
 
Barikiwa Sana Kamanda wangu! Nakukumbuka vyema ulivyokua unatulisha tango pori, Hakika wokovu umekaribia Sana
Mimi nilikuwa nakipenda sana Chama Cha Mapinduzi,mpaka awamu hii ilipoingia nikaanza kuona uvunjifu mkubwa wa Haki za Watanzania.
Nilikuwa na Group langu kubwa la kampeni ila kwa sababu Wapinzani nao ni Ndugu zangu Watanzania nikasema NO!..mipango mingi ya kununua na kuwatisha wapinzani nikaona we're Sleepwalking in to a Civilwar and One man rule.

Nimehama CCM tokea November 2018 nimehamia Upinzani niligundua mbinu nyingi za Kuwalisha Sumu viongozi wa Upinzani Lowassa ni Mmojawapo Ninamshauri Fred Lowassa akampime mzee wake,tokea nihamie upiinzani nimewashauri viongozi kadhaa,na najisikia niko free.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika kipindi hiki , urafiki wa baadhi ya makada wa CCM kwa wapinzani umekuwa mashakani. Wengine wanajificha kwa kuogopa kuonekana msaliti. Mambo kama ushirikiano wa kibiashara na kifamilia kwa baadhi ya watu umekuwa mashakani. Katika hatua hiyo bado kuna watu hawajaona ubaya huu.
 
Wakati huu wa mpito haya yote hayana budi kutokea kwani nchi ilioza na sasa inasafishwa!

Hii ni dhahiri kwamba tuna tatizo kama taifa. Ziko njia mbali mbali za kusonga mbele bila kuathiri utamaduni wetu kama watanzania. Pengine uwezo wa viongozi tulionao ndio tatizo. Kupitia short cut ya kuharibu maisha ya watu, kupoteza watu, kuuwa n.k kwa kisingizio za mpito ni kukosa maarifa na weledi. Kuna njia nyingi tu zingeweza kutumika na kufika huko tunakokusudiia kwenda.
 
Hebu tazama athari zinavyojitokeza sasa. Inapofika mahali muhimili wa dola hausimamii jukumu lake la msingi kwa muhimili mwengine ni tatizo. Nchi za wenzetu linapokuja suala lenye maslahi ya Taifa na ikionekana serikali inataka kulazimisha mambo basi Bunge au MAHAKAMA hutumika kwa haraka kuzuiya. Leo mwenendo wa Mahakama uko wazi . Ishu kama ya CAG na huu muswada wa Vyama vya siasa zinasikitisha sana. Hatukushangaa Mahakama kufanya figisu kwa ile kesi ya kutaka Tafsiri ya Kikatiba ,kilichotokea wote tumekiona. Halafu siku mbili tu unasikia Jaji anapandishwa cheo na Serikali.

Nafikiri Msingi wa Kesi au Content ndio mahakama ingejielekeza nayo kwa kuangalia maslahi ya Taifa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom