Kwa waliowahi kuishi Iringa, comment hapa tafadhali

Mk wawa High school 2002-2005,Mkwawa university 2011-2014,kula misosi makanyagio na pombe Sana Tembo bar kule mjini
 
nakumbuka mwaka 2003-2004 sekondari mkwawa,ukiwa na 500 siku nzima uingii mesini,unaenda sehemu inaitwa makanyagio.100 asubuhi unapata chai kwa maandazi matatu,mchana 200 wali kwa maharage,jioni 200 tena unapata wali kwa maharage.
Tulikua pamoja,Makongoro west,unamkumbuka Nelcon?
 
Mkwawa High School 2003/2004 kabla haijabadilishwa kuwa chuo!To be honest hakuna shule nzuri kimiundombinu km ilivyokuwa mkwawa kwa shule zet za serekali!Maisha yalikuwa pouwa sana unakutana na watu kutoka kila pembe ya Tz!
Mkuu akiwa Mbao
 
kitu cha Ifunda Tech, 1988 hadi 1991, baridi usipime, niliishi ifunda chumba D2 toka form one hadi form four. Namkumbuka sana mzee Matebela, mzee wa kusupply Maziwa na makorokocho mengine shuleni. Kulikuwa na mpishi anaitwa mwakalinga....

Mambo ya banda bichi kupata mkangafu, mdindifu na mteke... We acha tu... Lyande kuoga kwa kupaka maji mwilini lakini mgongo hauhusiki
Ifunda nimetoka 2008 banda Beach bado ipo na ubora wake
 
We form wani wangu... We group gani? mi group Four 88-91 D2 seuta.... Nammis sana mchili, Bladi kinyakanyaka, Mbungi nilikutana naye Iringa Nov 2012 stend ya Iringa, Kitomali mzee wa kuzaa watoto karibu karibu (Mapacha wa nje), Kuna Shabani wa lelctrical Science...
Mbungi, shabani wa electrical science na ktomali mkewe nae mwalimu lakn jioni anauza maandazi na chakula mgahawani... Wahuni maandazi wakaanza kuyaita vitomali ishu ni mwl. Kitomali akusikie ukiita maandazi vitomali maji utaita mma.. Head teacher Vaginga manywele
 
Nilisoma Ilala Shule ya Msingi darasa la kwanza mpaka la Saba (1987-1993),nikachaguliwa Form One Lugalo (1994-1997). Iringa nitarudi,maana nakijua kihehe zaidi ya lugha yangu
 
Mkuu dah sekeni sinzasinza tulikua tunatishiwa sana tukiwa wadogo mimi nimekaa igula mkuu
Hilo vitu laini limechomelewa sana kwenye garage ya Mzee ipogolo pale enzi hizo mzigo mkubwa linalokuwa limepakia ni mapindigesi na kuku wengi wa kienyeji likifika ipogolo linagombaniwa mno na akina Guliano dalali maarufu wa Kuku pale ipogolo
 
nilisoma pale living stone int school (lisco) njombe .karibu na kibena..nakumbuka sana yale malori yanayofanana na matrekta yanayobeba magogo yakipita pale, kwa aliesoma pale ani pm, nimemiss sana old school stories including ile ishu ya vibwengo
Wewe ulikuwa boya ulimtia hasara baba yako, nakuhakikishia Iringa hakuna shule yenye jina la living stone "living stone" labda kama ile "Livingstone" ilibadilishwa jina.
 
Mkwawa High School 2003/2004 kabla haijabadilishwa kuwa chuo!To be honest hakuna shule nzuri kimiundombinu km ilivyokuwa mkwawa kwa shule zet za serekali!Maisha yalikuwa pouwa sana unakutana na watu kutoka kila pembe ya Tz!
Mkwawa ilikuwa shule ya wazungu Saint Michael na Saint George kabla ya kufungwa na kuhamishiwa Mbeya School hivi sasa Iyunga ambayo pia ilikuwa ya wazungu, shule hizi hazitafikiwa na shule yoyote ile ya serikali kwa miundombinu yake, labda ukoloni urudi tena! Ni vigumu kuamini kuwa watoto walikuwa wanatoka Afrika Kusini kuja kusoma huku.
 
Iringa si mchezo,

Kuna bus moja la zamani sana, limeandikwa vitu laini linatoka kilolo ndani huko !!!!! Nimekaa mitaa ya Ndiwili kwa mtalaam SEKENI, huyu mkinga alikuwa maarufu sana. RIP Sekeni.
tuliishi tukiambiwa huyu mzee alikuwa nyonya damu. watu wakiamua kukuzushia. wenyeji wa ndiwili tulidanganywa.
 
Back
Top Bottom