Kwa waliowahi kufumaniwa mlijiteteaje?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Kufumania sio kazi rahisi kama neno lenyewe linavyozungumzwa. Ni kazi inayohitaji maandalizi na kujitoa kisaikolojia na nguvu ya mwili. Unaweza kumkosa mke au ukajikosa mwenyewe.

Jamaa fulani mtaani kwetu hapa kalazwa hospitali kutokana kipigo alichopata alipokwenda kumfumania mkewe!

Jamaa aliyefumaniwa aliona njia pekee ya kujiokoa na kipigo na fedheha ni kupambana. Mwisho wa siku kamjeruhi vibaya mwenye mali yake.

Inauma sana, umemfumania mke wako akishughulikiwa na kisago cha mbwa koko umepata!!
 
Duh kama unajua huna ubavu wa kupambana usiende kufumani kwasababu anaefumaniwa kuna mawili apambana kujiokoa au anywee sasa akiamua kupambana kujiokoa na wewe unaefumania hukujiandaa utaishia kuwa kama huyo jamaa yako
 
Back
Top Bottom