Mkuu hizo interview za Utumishi nazifahamu kuliko unavyofikiria..,
Mkuu kumbuka wote mnaoitwa kwenye Usaili huo wa Mahojiano wote mnasifa zinazowiana hivyo anaetafutwa ni yule tu ambae ataonesha utofauti kati ya nyie wote wenye sifa zinazofanana.
Utofauti huo utakuwa kwenye nyanja tofauti kutokana na Vigezo vyao wanavyovitumia katika kupata hao walio bora..,
Mathalani, Majibu ya Maswali ya darasani unapaswa kujibu kidarasani kwenye Mtihani wa kuandika, lakini unapoona umeulizwa Swali la darasani kwenye Usaili wa Mahojiano basi lijibu kama MTU mwenye tajiriba ya hicho kitu, na si kulijibu kwa kunakili hadi nukta kama ilivyo kwenye Makaratasi yako kwakuwa wote Mtatoa maana sawa kama Mlivyosoma hivyo hakutakuwa na utofauti wa anae juwa na asie juwa. Aidha yapo mengi unayopaswa kujitofautisha kwenye Usaili ili kuwa tofauti na Wasailiwa wenzako ingawaje kubwa ni kujiamini tu!!!