kwa walio na ndoa tu......!!!!!!!

Mdogo wangu kama
ulivyoambiwa mwanzo ndoa hhuwa haina formular. mimi ndoa yangu ina miaka
minne nilianza kwa kufuata formular kutokana na kwamba nilikuwa nasoma
sana makala za shaluwa kwenye web ya shigongo. nikawa nafuatilizia kila
kitu. tulikuwa tunagombana sana na ke wangu coz kila nilichokisoma
nuilienda kukifanyiia kazi kwa mke wangu.
jambo la maana kwako jaribu kujiweka katika nafasi nyuma ya mkeo. yaani
kila jambo mpe mkeo kipaumbele, msifie kila mara hata pale ambapo
unajua hakufanya vizuri tafuta tu pointi moja umsifie ili ajiione
anapendwa na anakubalika. jambo lingine ambalo ndilo la muhimu kuliko
yoote jenga uhusiano na MUNGU wako kama wewe ni mkristo kama mimi
jitahidi usali pamoja na mkeo, na kuwa mstari wa mbele kwenda kanisani,
kama wewe ni mwislamu vilevile. mleteee zawadi mkeo kila mara mara 2 ama
3 kwa wiki hivi. sio lazima zawadi kubwa hata kama ni pipi, chokolate
ama chochote ili mraddi tu ajue kuwa unapokuwa mbali na yeye huwa
unamkumbuka. kama wewe ni mfanyakazi ukisafiri usirudi bila zawadi ya
kueleweka kama nguo, kitambaa, viatu ,mkoba na chochote kile
utakachoone. katika siku yako tenga muda wa kukaa na mkeo mkiwa wawili
kabla ya kulala. na wanawake maranyingi wanapenda kufanya mapenzi mchana
na asubuhi kuliko usiku maana usiku wanakuwa wamechoka kwa kazi nyingi
za mchana kutwa na wanahitaji pumnziko so epuka kudai unyumba muda mfupi
tu baada ya kwenda kulala. pia muone mkeo ndo mwanamke pekeee mzuri
duniani tena msifie mara kwa mara kwa uzuri alionao na ukiwa unasema
hayo mwangalie usoni usiseme ukiwa umeficha uso ataona unamdanganya. pia
wakati wa mamboz wanaume wengi akimaliza tu anageukia upande wa pili,
hiyo ni sumu ya penzi mwanamke anapenda kukumbatiwa mara mmalizapo mambo
yenu kwani hujiihisi kuwa hana thamani tena baada ya kukupa uroda so
kulifuta hilo just endelea kumkumbatia kwa dakika 15 hivi baada ya kuwa
mmemaliza kupeana shughuli. nawatakia ndoa njema
umeandika ushauri uliojaa maneno ya busara,hongera sana,i liked that
 
Kila mmoja awe tayari kuyavumilia mapungufu ya mwenzi wake... By the way mbona hujatuambia huyo bi dada ni nani nae tumpe hongera zake? Kila la heri mkuu..
asante kwa ushari wako. huyu bii dada yeye hakuwa amejisajiri bali yeye alikuwa akipitia tu post za wanao tafuta wachumba. ila tarehe 19 nitaweka pc zetu kwenye fb yangu.
 
mawasiliano, jambo la msingi sana, kama mekwaruzana au mwenzio amekukera au umemkera kwa namna yotote, hakikisha kabla hujatoka asubuh kwenda kwenye mihangaiko yako mmeongea na kufix tatizo hlo.

Sala muhim sana, siku majarib ni mengi kwenye ndoa zetu lazima kumtanguliza Mungu...........................

hongera na Mungu akutangulie, ndoa yako iwe na mafanikio
asante mungu awe nawe! ili mawazo yako yatusaidie wengi tunao hitaji, asante.
 
asante kwa ushauri wako ila nitakuwa tofauti juu ya sim, mii sim yangu iwe huru kwa mke wangu hata yake iwehuru kwangu. na chamuhim tujuwe kama kunawatu wanaweza tumia sim kama siraha yao ya kutugombanisha. na uwazi na kutowekeana mipaka juu ya ndoa yangu naamini changu ni chake na chake ni changu.
 
1. Mpende mwenza wako( uone kuwa kuwa naye ni perfect choice). 2. Ukikosea omba msamaha, akikosea akiomba msamaha,msamehe kwa dhati, achilia kabisa usilimbikize moyoni. 3. ikitokea ubishi wa aina yeyote, agree to disagree. 4. Sikuzote mshukuru kwa kukubali kuoana na wewe. (these 4 principles works in both ways out)

asante nitazigatia!
 
Back
Top Bottom