kwa Walio Na Familia!!...Inawahusu!!

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,519
1,825
sisi kama wazazi hivi tunakuwaga na muda kweli wa kuaangalia watoto wetu hata mara moja kwa wiki ipasavyo? ukiangalia na hivi tunavyobanwa na majukumu kazini na sehemu za kutafutia tonge.. Nyumba nyingi sana siku hizi zinawasichana wa kazi, lakini sio wasichana wote wapo makini kwa watoto ni asilimia chache tu, je wewe kama mama umeshawahi ukiwa nyumbani hata kama ni siku moja tu ya wiki kumchunguza mtoto wako awe wa kike ama wakiume, umeshawahi kumuangalia maumbile yake kama ni mzima au vipi?

kwa nini ninasema haya; Jana uswahilini kwetu kumetokea jambo ambalo limenisikitisha na kuniuma sana, kijana mmoja ambaye yupo form one amekamatwa kwamba anatabia za kulawiti watoto, sasa hivi alimfanyizia mtoto wa miaka minne!!!!!!!!! baada ya mama yake jana jumapili kuwa nyumbani na kukaa karibu na mtoto
wake wa kike nakugundua anatoa harufu mbaya huko kwa bibi.
Baada ya kuona hivyo akaamua kumuita mwanaye chumbani na kumvua nguo na kumwambia alale kwenye kitanda baada ya kumchunguza
akagundua anatokwa na uchafu mwingi huko chini na pamechezewa ndio mama kushtuka na kumuuliza mtoto kwa upole ili mtoto asiogope na kushindwa kumjibu, basi yule mtoto akamtaja kwamba yule ananifanyiaga hivi!!!!
Basi ndio yule mama kupagawa kwenda kwa yule mtoto kwakuwa ni jirani kumbana kweli na kwa vitisho ndio yule mtoto kukubali na kuanza kulia akiomba msamaha, yule mama wa mtoto wa kike hakutaka kuelewa hayo akambeba pamoja na mama yake mpaka polisi ambako alikaa huko mpaka jioni ndio ndugu zake yule mtoto wa kiume kwenda kuomba radhi na kumbembeleza sana yule mama amsamehe na kumtoa kijana wao.

Baada ya muda mrefu sana wa kuvutana huku na huko baadaye yule mama akakubali kumsamehe mbele ya mjumbe wa nyumba kumi
na kumwambia kwamba ahame mtaa na kila mzazi mtaani hapo akakubaliana na hilo swala kwamba yule mama na mwanaye wahame.

Inauma sana sasa hapa afadhali mtoto alikuwa anajuwa kuzungumza je kwa watoto ambao hawawezi kuzungumza vizuri, sio wa kike tu siku hizi hata wanaume hufanyiwa hivyo..jamani tuwe makini tusikimbize sana tonge tukasahau majukumu yetu kwa watoto wetu.
 
asante kwa kukumbusha, maana siku hizi majukumu yapo kwa wadada au kaka wa kazi ndo wnaangalia je watoto wamekula wamelala hadi wengine wamebeba majukumu zaidi ya kulea watoto na kulea famila hadi huduma kwa mama au baba wanatoa. Hivyo muhimu tenga mda angalia watoto wakoje sio tu maumbile hata suala la maendeleo yao kimasomo.
 
so sad....

Na inasikitisha zaidi kwa huyo mama kukubali kijana atolewe ....kitendo hicho kitasababisha watoto wengine wawe hatarini
 
Mwanamke wa hii generation ana kazi hasa.azae,alee,afanye kazi za ofisini,za nyumbani-manake akimwachia sana dada wa kazi mwishowe anapata promotion.

kujibweteka haiwezekani manake maisha magumu hayaruhusu akae tu.mwishowe naona mwanamke ana mzigo mkubwa sana.
 
Aksante kwa taarifa tunashukuru ila pia tusisahau kumkabidhi MUNGU familia zetu. Sio waume tu hata watoto, ndugu, majirani na hata maadui zetu.
 
Tunashukuru sana kwa kutukumbusha!kwa upande wangu sina imani kabisa na hao housegirls na houseboys!nipo tayari kumuachisha kazi mke wangu ili alee watoto kw uzuri then housegirl aje baadae wakati watoto wamekua wakubwa na ndipo wife arudi kazini!
 
Mwanamke wa hii generation ana kazi hasa.azae,alee,afanye kazi za ofisini,za nyumbani-manake akimwachia sana dada wa kazi mwishowe anapata promotion.

kujibweteka haiwezekani manake maisha magumu hayaruhusu akae tu.mwishowe naona mwanamke ana mzigo mkubwa sana.

nao Wasichana Wa Kazi ,Ukiwaachia Watoe Huduma Muhimu Za Kifamilia!!
Ni Changamoto Kwa Mwanamke zidi Ya Mumewe!!
Uko Sahii!!
 
Tunashukuru sana kwa kutukumbusha!kwa upande wangu sina imani kabisa na hao housegirls na houseboys!nipo tayari kumuachisha kazi mke wangu ili alee watoto kw uzuri then housegirl aje baadae wakati watoto wamekua wakubwa na ndipo wife arudi kazini!

Pande Zote Ni Hatari Tupu,Ari Inatisha Si Kidogo!!
 
Haya mambo ya kuombana msamaha baada ya mtu kuabuse watoto huwa siyaelewi kabisaaa! Na ajabu zaidi wote tunaona sawa. You rape my son or daughter and we negotiate about it? If the system wont deal with you i will personally! Gggggghhhrrr! Spoiled day!
 
Na anapohamishwa mtaa ni ili akatafute new victims? Seriously! Hata serikali ya vilaza tu inajua, rapists hawapati hata parole manake ni dhambi wanayopaswa kuilipia in full!
 
asante.

Na mie siwezi hata kukodi watu wa kumshugulikia, nitamshiighulikia kwa mikono yangu miwili.

Back
Top Bottom