Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,827
- 730,273
Mijadala imepamba moto mitandaoni kuhusiana na vyeti feki na agizo la kuwafuta kazi maramoja , pressure ni kubwa watu na watu wamechanganyikiwa wakifikiri wataanzaje kurudi kijiweni huku changamoto za maisha zikiwakabili
Rafiki huna haja ya kupaniki, kila jambo na majira yake.. Hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya
Ni wakati wa kusimama imara na kuanza upya, kuangalia fursa zilizopo ...kila jambo hutokea kwa sababu maalum.... Kwa wale waaminio Mungu hawezi kukufungia milango yote. Ni kiasi cha kutulia na kuona mlango wako ulipo
Ni kati ya watakaofukuzwa ndio watakuja kuwa matajiri wa baadae viongozi na hata watu wenye vipawa mbalimbali, maigizo na sanaa muziki na utunzi, wakulima wenye mafanikio na wafugaji wa kupigiwa mfano
Ni wazi ulikuwa na kitu cha ziada akilini mwako very unique cha kipekee mno.... Lakini kibarua cha utumwa wa kutumikishwa kazi nyingi zenye ujira usiokidhi mahitaji, viliminya kipawa chako cha biashara
Cha kilimo
Cha muziki
Cha sanaa mbalimbali
Cha ufugaji
Cha ubunifu mbalimbali
Cha uandishi na utunzi
Fursa imekuja sasa itumie vema, ni wakati wako sasa.. Hutakuwa tena na majuma yenye kuchosha.... Kudamka alfajiri na kukimbizana na muda uwahi kibaruani
Hutakuwa tena na woga wa makaripio na manyanyaso ya bosi mkorofi
Hutakuwa tena na Jioni zenye kuchosha kutokana na kazi tele za mchana kutwa
Wewe sasa ni mpya
Wewe sasa ni mshindi na si mshindwa... Simama imara uondoke kesho yenye matumaini furaha na mafanikio inakusubiri
Ondoka sasa kwa kujiamini
At last your bright future is here.... Dreams can come true
Stay strong and focused
Jr