Kwa wale wapenzi wa mbio na michezo ya pikipiki

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,957
12,543
Kwa wadau na wapenzi wa michezo ya mbio za pikipiki mnakaribishwa kuja kushiriki na kutazama maeneo ya Tanganyika Packers Kawe nyuma ya kanisa la Mwamposa.

Michezo ya pikipiki za matairi mawili, matatu na manne (Quadbike). Mshiriki wa kucheza ni mtu yeyote aliye na bike na safety gears na hakuna kiingilio.

Muda ni kuanzia saa 9 mchana kila jumapili. Karibuni mshuhudie burudani kila weekend.
 
Watu wote mnakaribishwa mje mtazame burudani na kubadilishana mawazo kuhusu usafiri wa pikipiki.

Pia unaweza kuja na pikipiki ya aina yoyote utakutana na mafundi utauliza na kusaidiwa kitaalamu.
 
Jumapili hakuna ibada hapo kwa mwamposa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ibada zipo, michezo inafanyika uwanjani nyuma ya kanisa.

Kama unataka ufike kirahisi pita njia hiyo ya Mbezi kwa Zena ukifika kwa hao mafundi fenicha utaona njia ya kukatiza uwanjani. Pia unaweza ukaenda mpaka usawa wa Feza Secondary au ukapita hapo hapo kanisani unaruhusiwa.
 
Back
Top Bottom