Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Mambo ya kukunja ngumi ni ya miaka ile ya 80,napiga kwa kutumia push bars
Kuna aina ya push-up man, je push-up unazopiga...ni za nakoz (nuckles) mbili au zote ...na kama ni push-up za nuckles zote ni zile unakuwa kwenye flat surface au za kuweka miguu juu ya kitu kama jiwe, stuli au ukutani...150 push-ups mana ake uko fit,
na kama we unaona uko vizuri jaribu zile za vidole vitatu then uje unipe mrejesho......alafu utofautishe nuckle push-ups na palm-push-ups

Sent by Diaspora
 
Ndio maana nikasema nimeacha gym nimeamia kwenye push up
Hapa umekuja ku-brag ama kukutana na wapenda push up mkuu!????



Anyway, ukipiga push up according to standard huhitaji kwenda gym kabisa..na mwili hautepeti hata ukiumwa.

Sent by Diaspora
 
Teheteheeeee!mwanaume hutakiwi kuwa na kifua flat kama sakafu
Me nimeanza na 10mornie,20 jion,nakajitahidi kuongeza walau 5 kila baada ya siku tatu,now napiga 30 asbh,30 jion.its enough 4 me,mabadiliko nayaona kifua kinapanda wastani,sio Kama mwanzo kilikuwa Kama meza.

Sent by Diaspora
 
Wakuu mimi naomba tips, ninaanzaje hili zoezi. Mana nikajaribu kuenda hata moja inanishinda.
 
RATIBA YANGU.

j3 na ijumaa nakimbia uwanja wa mpira x10 bila kupumzika baada ya hapo napiga mazoezi ya tumbo na bar push ups 20x5.

J4,J5 ALH JMOS na JPILI ni push ups 20x 5 + squats
 
pole sana.
Mkuu nenda Hospital inatibika hiyo kitu.
Ukichelewa matibabu yake yatakuwa opresheni.
Kuna dawa za Pilex tablet au pilex cream
husaidia kuondoa hilo tatizo.
Lakini nakushauri uende Hospital kwanza.
Kuna dhana kwamba bawasiri inatibika kienyeji, ni kweli
lakini na Hospitalini wanaponyesha.

Natamani sana hizo,ndio zilikuwa zangu. Home kwangu nimetenga room kabisa. Ilikuwa kila asubuhi,saa moja na nusu namalizia hapo. Naanza na kuruka kamba na kichura hiyo dk 30 nakata. Nakuja push up zile za two nakoz tu,mkupuo wa 30,30 mara 5. Nakuja unashika mikono kwa nyuma kwenye kama mwamba wa kitanda,yaani unaukigeukia huo mwamba unashuka chini na kupanda. Mikono tu na visigino ndio vinakuwa vimeubeba mwili. Hayo mazoezi nimeanza nayo miaka 20 iliyopita. Sasa kilichokuwa kinanitokea kila nikikomaa mayo sana ilikuwa napata bawasiri, yaani kama vidude vinatokea sehemu ya haja kubwa,kama tuvidole tudogo hivi. Wakati wa haja,nikimaliza ile mishipa ya ndani inauma. Ikawa hiyo inakuja na kupotea nikawa naendelea na mazoezi huku nikitafuta tiba. Nimehangaika sana na tiba. Hivi ninavyoongea nimeacha mazoezi kabisa,kwa sababu sasa nikifanya tu kidogo napata maumivu makali balaa. Bado nahangaikia tiba,tiba ni adimu sana. Inaniuma sana nikikumbuka mazoezi,natamani mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapiga push za ain ngap?? Kuna aina nying sana.

Kwa hiyo level yako. Piga oblique, Soda ya kopo, jiwekee chalenge ya 30 - 1
Kwa kifupi gym nilishaacha kwenda long time nikaamua kuanza kupiga push up home tu!

Kwa kifupi huwa naenjoy sana hasa marafiki wakija kunitembelea huwa nawapa challenge ya kushindana na Mimi huwa nacheka sana baada ya push up 15 tu wanaanza kuhema kama mbwa koko!wakati Mzee mzima hapo naenda zaidi ya push up 150

Tukutane hapa wapenda mazoezi

Sent by Diaspora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom