kwa wale wanapenda dagaa je wajua jinsi ya kuzipika? jifunze kupiti hapa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
NAMNA YA KUPIKA DAGAA+NYANYA CHUNGU+NAZI: RURAL OR URBAN STYLE
2.jpg


Hawa ni wale dagaa wa kigoma lakini wadogo wadogo sana, wachambue vizuri kwa kiasi utakacho kupika, halafu uwaoshe vizurii wasiwe na michanga.

1.jpg

Andaa kitunguu, nyanya, carrot, hoho, ndimu na nyanya chungu, bila kusahau tui la nazi.


3.jpg


Weka mafuta kidogo sana kwenye sufuria kwakuwa mboga yetu tunaweka nazi, yakipata moto weka dagaa zako ulizozisafisha vizuri, zigeuze geuze halafu weka maji ya ndimu uliyokamua, geuza geuza moto usiwe mkali sana, katia kitunguu, endelea kugeuza hadi uone vitunguu vinageuka rangi na kuwa brown, halafu weka nyanya ulizokatakata ukachanganya na hoho na carrot, funika kwa muda kidogo inategemea na wingi wa mboga yako, ukifunua nyanya zitaanza kulainika ukigeuza utaona zinachanganyika na dagaa kuashilia zinalainika.

4.jpg

Kabla hazijalainika sana, weka nyanyachungu kwa juu ulizokatakata ukubwa uutakao, kwakuwa nyanya huwa zina maji mpaka hapo unakuwa hujaweka maji, ila ukiona mboga inashika chini, weka maji kidogo, funika, baada ya muda funua geuza geuza, weka chumvi kiasi, yale maji yakianza kukauka na kwakuwa nyanyachungu hazitakiwi ziive sana na kulainika sana weka tui lako.

5.jpg

Ukiweka tui la nazi acha ichemke vizuri, chumvi iwe ya kutosha isizidi sana maana chumvi ikizidi ni matatizo, utakuwa umeridhika imeiva ipua.



6.jpg

Na hii ni mboga yetu ikiwa tayari kuliwa na wali, ugali, ndizi za kuchemsha, mihogo ya kuchemsha, viazi hali kadhalika, ni tamu sana.

7.jpg



Ukishakula, baada ya nusu saa, shushia matunda yako bila kusahau maji ya kunywa, unamshukuru Mungu kwakukujalia msosi kama huu, unawaza next meal itakuwa ni chakula gani.

Msosi huu umeangalia mtu wa kawaida kabisa na aishiye mazingira yeyote either mjini au kijijini na mahali ipatikanapo nazi, na ni mboga ya kupika kwa muda mfupi sana,mpishi ni mimi mwenyewe
 
Mkuu dah umenikumbusha msosi wa home loh!! Hakyanani, jmos nimenunua tudagaa flan twa vietnam hata wife hakuweza pika despite ya kuweka curry na coconut! Hakyanani hapa nimepata hamu sana ya hii maneno.

Hapo kwenye matunda sasa dah, ni nusu saa baada ama kabla?
 
Mkuu dah umenikumbusha msosi wa home loh!! Hakyanani, jmos nimenunua tudagaa flan twa vietnam hata wife hakuweza pika despite ya kuweka curry na coconut! Hakyanani hapa nimepata hamu sana ya

Hapo kwenye matunda sasa dah, ni nusu saa baada ama kabla?

Hee dagaa hilo lanyweshwa maji hatar hasa lile la baharini nahisi hilo la vietnam lina chumvi....
 
Huyu Jerrymsigwa weeh muache tu. Kwa nini hakupika mwenyewe!

shosti, dagaa lake ugali na tembele. Hapo hadi sarawili nafungua kishikizo. Mie sipendi dagaa wa kigoma, nawaona wagumu afu naogopa miiba. Labda nipate hao wadogo
Kaka JERRYmswiga umenkera kumsema wifi yangu....

Alafu hiyo kigoma kuna bahari? Au wa maji baridi hao dagaa?
 
Last edited by a moderator:
Aaahaaaaahaaaa...
Dah small fish upate na BADA kwa kikombe cha chai pembeni mtu mzima lazima ubebwe...

***Thanks***
 
mchele wa kyela huo mamii. haachwi mtu hapa, tunajiwezesha.
Kinyume chake ni pishori na kitumbo, lol. Hivi pishori ina mapishi mbali mbali? Manake nahisi hata nazi haikoi

Pishori kwa biriani au pilau kwa sisi huku mazoea yetu....ila nimemskia shosti Angel Nylon mbea ndio tamu zaidi kwa pilau..
Hapa nasubiri aipike anigongee mlango na kibakuli nijilie pilau la mbea..lol
 
Last edited by a moderator:
Mwanangu huwa anapenda kuwaita samaki wachanga, yaaani ukimuwekea na ugali ujue ni lazima samaki mchanga waishe kwanza ndio ale ugali...Heh i love it
 
safi sana, dagaa hili mpango mzima na ugali na kapilipili pembeni halafu uwe hujala dagaa siku nyingi mbona utabebwa!! asante MziziMkavu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom