Kwa wale wanaotumia magari binafsi kwenda Tanga, Kilimanjaro na Arusha tumieni barabara ya Bagamoyo

kifaru 1

Member
Oct 21, 2013
28
0
Ndugu zangu mnaokwenda mikoa ya kaskazini hasa wachaga tumieni barabara ya bagamoyo ni fupi haina foleni.Barabara haina mawimbi na wale wazee wa tochi hawapo achaneni na Chalinze jamani.
 
SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Ushauri mzuri lakini hujatoa maelekezo muhimu. Mimi nimekuja dar kutembelea jamaa zangu nataka niondoke kesho kurudi Moshi 23/12/na kivitz changu. Hiyo ya kupitia Bagamoyo kutoka dar ni moja kwa moja au kuna mahali unachepukia.Hebu toa maelekezo ya njia ndugu!
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
36,159
2,000
Labda kuanzia Tegeta na kuendelea ndio hakuna foleni,lakini kuanzia mwenge kuitafuta mbezi afrikana masaa matatu!! Na hii ya mbezi louis nayo foleni kuanzia magomeni mpaka mbezi kwa mwisho! Hakuna cha nafuu moja ni sumni na nyingine senti hamsini.
 
Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,708

Yaani ni kama National na Panasonic vile.....
 
Majura Jack

Member
Oct 11, 2013
30
0
Mmh ni kama Sumni kikwele na 50Cent kinyamwezi
Haina tofauti hiyo ni kuruka geti na kukanyaga Mlinzi!....
 
Majura Jack

Member
Oct 11, 2013
30
0
Aaswa kama Tui na Maziwa!
Au kushika Sumu unaambiwa kanawe,unafungua koki ya bomba na sumu kiganjani then ukimaliza kunawa unafunga koki bila kuiosha hapo sumu itakuuwa tu!
Hiyo ndo miundo mbinu bila mbinu bunifu!
 
wanakopi

Senior Member
Sep 30, 2012
109
195
nimetoka jana na nimepita iyo njia ni nafuuu sana kuliko ile yakule tena sijakutana hata na ajali hata moja kwa njia iyo pia safi unanunua zako matunda yakutosha hasa mananasi ila kikubwa ni kuwa makini sana maana wengi wao wanaandesha uku wamelewa na magari ni mengi sana me ni mmakuwa nimealikwa tu na wana ila nimependa sana hawa watu kwa kuacha mambo yao na kuja kwao sio kama wengine awaendi hapana ila hawa kiboko
 
Bethania

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
327
250
Ushauri mzuri lakini hujatoa maelekezo muhimu. Mimi nimekuja dar kutembelea jamaa zangu nataka niondoke kesho kurudi Moshi 23/12/na kivitz changu. Hiyo ya kupitia Bagamoyo kutoka dar ni moja kwa moja au kuna mahali unachepukia.Hebu toa maelekezo ya njia ndugu!

Wewe amuka mapema halafu nenda mpaka bagamoyo utapata
njia ya msata
 
Cyan6

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,534
0
Wa Mbezi beach Mikocheni, Tegeta ndiyo njia yetu tulishaistukia toka mwaka jana! Ila wa kimara nadhani ya Chalinze itawafaa zaidi. Hii Bagamoyo rd ikiisha itakuwa mteremko tuu!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,548
2,000
Ndugu zangu mnaokwenda mikoa ya kaskazini hasa wachaga tumieni barabara ya bagamoyo ni fupi haina foleni .barabara haina mawimbi na wale wazee wa tochi hawapo achaneni nachalinze jamani

Matatizo ya Tanzania hayatamalizwa kwa njia za ki-mkato ki-mkato. Watu wengi wakihamia huko tatizo bado litawafuta! Njii ya kutatua matatizo ni kukabili na si kuyakimbia!
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,540
2,000
Labda kuanzia Tegeta na kuendelea ndio hakuna foleni,lakini kuanzia mwenge kuitafuta mbezi afrikana masaa matatu!! Na hii ya mbezi louis nayo foleni kuanzia magomeni mpaka mbezi kwa mwisho! Hakuna cha nafuu moja ni sumni na nyingine senti hamsini.

Mkuu,

Baganoyo Road foleni inaishia Tegeta kama ulivyosema,
But Morogoro Road Foleni inaishia Kibaha maana kote huko ni Tochi na Ujenzi.

Pili Morogoro Road inatumika na magari mengi maana hata wa Mbeya, Songea, iringa, Morogoro, Malori Makubwa wote humohumo.
Wakati Bagamoyo ni vigari vidogo tu, kwani Zaidi ya Tani 10 haziruhusiwi.

MLETA MADA YUPO SAHIHI KABISA.
Moja ni Senti Hamsini, wakati ingine ni Shillingi Hamsini!!
 
Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,582
2,000
Ni kweli mkuu njia ni nzuri..tumewahi kupita njia hiyo na tulikuwa hatuijui kabisaa..tulikwenda kwa kusoma ramani,ni raha saana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom