Kwa wale wanandoa mnaoaana leo tu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wale wanandoa mnaoaana leo tu!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 3, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  [h=3]Matiti ni Mali ya nani?[/h]

  Matiti ni chakula cha mtoto![​IMG]Linapokuja suala la matiti wanaume wengi (si wote) hunyang'anyana hati miliki ya matiti na watoto wanaonyonya hata hivyo wanawake nao kila mmoja ana mtazamo wake tofauti, hebu angalia maoni ya wanawake hawa wa Nigeria wanavyojibu swali la nani ni mmiliki halali wa matiti ya mwanamke.

  Mrs. Arogundade
  Mume wangu ndiye anamiliki matiti yangu kwa sababu mume alikuja kabla ya mtoto.
  Baada ya mtoto kunyonya kwa muda inakuwa zamu ya mume wangu kwani tunalala kitanda kimoja.
  Mtoto wangu ana access ya matiti yangu kwa muda tu wakati mume wangu ni mali yake maisha yetu yote.
  Matiti yangu ni kitu ambacho mume wangu huchezea na pia ni mto wake wa kulalia.
  Ukweli ni kwamba mume wangu hujisikia wivu kama mtoto wangu ataendelea kunyonya zaid ya muda aliopewa.
  Linapokuja suala la matiti yangu mume wangu huwa anachanganyikiwa, hawezi kufanya ile kitu (sex) bila matiti yangu.

  Mrs. Omisade
  Mume wangu ni mmiliki ya matiti yangu.
  Mume wangu akiyakamata tu matiti yangu basi huwa tunakuwa na mahaba ya nguvu katika uso wa dunia
  Mume wangu hawezi kuanza chochote bila kugusa matiti na pia hunisisimua sana kwa ajili ya kufanya mapenzi pia mume wangu hunambia huwa anamuazima mtoto wetu matiti na akimaliza anatakiwa kurudishiwa mali zake kutoka kwa mtoto.

  Mrs. Alhaja Sadiku
  Kitu kimoja ninachopenda kuhusu mume wangu ni pale anapochezea matiti yangu kama vile machungwa, pia huwa namruhusu mtoto wangu kuchezea matiti kwa kadri anavyoweza.
  Najua mume wangu alilipa mahari kitu inachompa access ya mwili wangu wote.
  Matiti ni kwa ajili ya chakula cha mtoto wangu.

  Mrs. Olagbaju
  Ukweli mume wangu ndiye anamiliki matiti yangu.
  Ila lazima akubaliane nami kwamba wakati tunayonyesha mtoto lazima aache kwa ajili ya mtoto wetu.
  Wakati ninaponyonyesha naweza kumruhusu mume wangu kuyachezea kwa mikono na si kunyonya.
  Mume wangu anamiliki matiti yangu permanently na pia anamiliki kila kitu nilichonacho pamoja na matiti.

  Mrs. Agunbiade
  Mtoto wangu ndiye anamiliki matiti yangu.
  Mume wangu ana mtazamo tofauti kwani huwa hapendi kabisa kuyanyonya, wakati nanyonyesha hapende kabisa hata kula chakula changu yeye hapendi kabisa harufu ya maziwa kutoka kwenye matiti yangu.

  Mrs. Amadi
  Mume wangu hawezi kufanya bila matiti, kabla kitu chochote kutokea yaani kufanya mapenzi lazima achezee matiti yangu na bila matiti siwezi kusisimka.
  Mume wangu husahau huzuni zote akianza kunyonya matit yangu.

  Mrs. Ganiu
  Mume wangu ndiye anayemiliki matiti yangu, mtoto wangu hunyonya kwa muda tu, then automatically matiti hurudi kwa mume wangu.

  Mrs. Daniel
  Mume wangu anamiliki matiti yangu kwa sababu alinioa kihalali.
  Tunapotaka kuwa kwenye huduma ya pamoja ya usiku kila mara ni utukufu, huanza kwa mume wangu kunichezea matiti yangu na kuyakandakanda halafu tendo huanza.

  Mrs. Omole
  Mume wangu aliniambia kwamba nilipokutana naye kwa mara ya kwanza matiti ndiyo kitu kilimvutia sana yeye, hivyo ni mali yake, najua matiti yangu ni sehemu ambayo mume wangu ni dhaifu, siwezi kumnyima mali zake, hata kama mtoto wangu anayanyonya, mume wangu bado huyanyonya na kuyachezea.

  Mrs. Ojo
  Kabla ya mtoto kuzaliwa matiti yangu yalikuwa ni toy la mume wangu kuchezea.
  Baada ya mtoto matiti ni kwa ajili ya mtoto, mume wangu anaishia kuchezea tu si kuyanyonya.

  Mrs. Alao
  Mume wangu anamiliki matiti yangu kwa sababu tulikuwa pamoja kabla ya mtoto kuzaliwa.
  Moto anaweza kuazima matiti kwa muda tu, mume wangu anamiliki matiti yangu permanently na mtoto huwa yake kwa muda.

  Mrs Salome
  Mume wangu ni owner wa matiti yangu.
  Hawezi kufanya mapenzi bila matiti yangu.
  Mume wangu huniambia matiti yangu ni chakaazi (succulent ).
  Matiti yangu humpeleka mbali sana mume wangu na husisimka hadi kufika juu sana hata kabla hatujaanza kitu chenyewe.
  Mtoto wangu ipo siku atayacha na kwenda kuanza nyumba yake hivyo lazima nimridhishe mume wangu kwa matiti yangu.
  Mungu alinipa matiti ili kumridhisha mume wangu katia suala la tendo la ndoa.
  Siwezi kunyonyesha mtoto miezi 7 bila kuyarudisha kwa mmiliki wake ambaye ni mume wangu mpenzi.

  Je, wewe kama ni mwanamke matiti yako ni mali ya nani? Mtoto au mume wako
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ukiwa katika Kristo ndoa ni tamu[​IMG] Je, unapita katika ndoa ngumu hata unawaza sijui kesho itakuwaje?
  Kila siku ikipita unaona afadhari ya jana kwa kwani ndoa ni ngumu, ipo ovyo, kupigana kila wakati, kitu kidogo basi mzozo mkubwa huzaliwa, nyumba ni moto, ni kudharauliana tu na visa kila iitwapo leo?

  Kwa tabia mbaya alizonazo partner wako unajilaumu hata kwa nini ulichukua uamuzi wa kuoana naye.
  Kila ukimtazama sasa hana mvuto kabisa, amechuja, ni mbaya na havutii, hapendezi tena na anakutia kichefuhcefu unatamani mlale vyumba tofauti au asafiri miaka isiyojulikana.

  Unaanza kufikiria kuachana ndiyo njia rahisi na kwamba ni permanent solution.
  Wakati huohuo mawazo yako na akili yako na moyo wako na nguvu zako zote umeelekeza nje, kwa partner mwingine ambaye unaamini kwa moyo wako kwamba ni mzuri, mtamu, yupo single, independent, loving, romantic, caring na ukiwa na yeye basi maisha yatakuwa matamu zaidi.

  Hata umeamua kubadilisha marafiki ili kukubaliana na nafsi yako kwamba ukiwa na hao marafiki wapya ambao ni single na wenye tabia mpya kama yako basi dunia itakupa kile unahitaji.

  You can not satisfy sin!

  Ukweli ni kwamba mambo si rahisi kama unavyofikiria.
  Pia ni kweli mawazo kama haya (mawazo ya kujenga nyumba kwa mabua) huwapata wengi sana kwenye ndoa zetu.
  Hebu vuta pumzi, pumua upya na jikusanye na kuanza kufikiria upya hata kama ndoa unaona haina ladha, imekuwa upside down, umeshindikana na haina mwelekeo ukweli bado unaweza kuirudisha kwenye siku zake za honeymoon.

  Wakati unaendelea kufikiria jinsi utakavyokuwa unajirusha na partner wako mpya katika viwanja mbalimbali, please fikiria kwanza watoto wenu (mtoto), pata picha jinsi utakavyowaambia watoto kwamba wewe na mwenzako mmeachana na wao sasa wanaishi na mzazi mmoja.
  Fikiria jinsi ya kugawana picha zilizomo kwenye Album yenu ya harusi, Fikiria mtakavyoanza kugawana mali.
  Fikiria utasema nini kwa Mungu maana uliahidi mbele zake na mbele za wandamu kwamba utaishi na hii ndoa hadi kifo kitakapowatenganisha.
  Fikiria familia, ndugu, marafiki nk
  Na cheti cha ndoa je, rings je?

  Je, bado unamawazo ya kuachana naye?
  Una uhakika hakuna mambo mazuri kwake kuliko mambo mabaya?
  Usije kuwa unataka kubadilisha seat kwenye meli ya MV Bukoba ukaishia kuzama ziwa Victoria, au usije kuwa unabadili seat kwenye meli ya TITANIC najua waweza jua nini kilitokea.

  Naamini unadhani kwa sura aliyonayo huyo partner 2 basi hutapata matatizo au migogoro yoyote.
  Ukweli ni kwamba hata ukipata partner mpya kinachobadilika ni sura tu matatizo ni yaleyale kwani wote ni binadamu na ndoa imara si kukimbia matatizo bali kukabiliana nayo na kujifunza na kuendelea mbele.
  Je, umeshaomba ushauri kwa kiongozi wako wa dini naye akashindwa? washauri wa mambo ya ndoa nao wakashindwa?

  Tafiti zinaonesha wengi walioamua kuachana na kuanza ndoa mpya baada ya muda hukutana na matatizo makubwa zaidi na magumu zaidi kuliko yale ya kwanza na hutamani kama wangerudi kwenye ndoa zao za kwanza.

  Kitakachokusaidia ni kubadilisha mtazamo (altitude) siyo kubadilisha ndoa na ukweli ni kwamba ni rahisi kubaki kwenye ndoa kuliko kuanza ndoa mpya.

  Usije ukaruka majivu ukakanyaga moto
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Wanaume wana ngozi nene kuliko wanawake, ndiyo maana wanawake huwahi kupata ndita (wrinkles) haraka na mapema kuliko wanaume wanapozeeka.

  Wanaume wana damu nzito kuliko wanawake, hii ina maana kwamba wanaume huwa na damu yenye oxygen nyingi zaidi na kupelekea kuwa na energy kubwa zaidi pia wanaume hupumua na kuvuta hewa nyingi kuliko wanawake hii ina maana wanawake huvuta hewa mara nyingi na hupumua mara nyingi zaidi kuliko wanaume.

  Wanaume wana mifupa mikubwa kuliko wanawake pia mifupa ya wanaume na wanawake imejipanga tofauti ndiyo maana kuna tofauti kubwa sana katika kutembea kwa mwanaume na mwanamke.

  Wanaume wana misuli mingi kuliko fat katika miili yao hivyo kuwa rahisi kupunguza uzito, wanawake wana layer ya ziada ya fat ndani ya ngozi ambayo huwawezesha kuwa na joto la ziada hata wakati wa baridi hivyo wanawake huwa na energy reserve nzuri na joto la asili kuliko wanaume, ndiyo maana wakati wa baridi sehemu zingine kiwango cha wanawake kupata mimba huongezeka maradufu.
  Guess why?
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Harusi zingine kazi kwelikweli!

   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  Wapo ambao siku ya kwanza ukitokea na maua basi umefungua mlango katika moyo wake.[​IMG] Fikiria wewe ni kijana wa kiume umepanga kukutana na binti ambaye unategemea awe mchumba wako, unawaza je, itakuwaje? Je, atanikubali kweli? Ataridhika jinsi nilivyo kweli? kiroho kinakutunda kweli maana hujazoea haya mambo!
  Huhitaji kuwaza au kufanya mambo makubwa just relax fuata hizi tips bila shaka lazima utamvutia kiasi cha yeye kutaka kukutana na wewe tena na tena.

  HAKIKISHA IDARA YA USAFI UMEKAMILIKA
  Umeoga vizuri, umevaa nguo safi, unaweza kuvaa nguo za gharama na bado zikawa chafu so vaa nguo safi, piga mswaki na kuwa na meno safi.
  Wapo akina dada akishajisikia unanuka basi bye bye, au akiona meno ni machafu na mboga za tangu juzi zimo kwenye meno anakata tamaa kabisa, au mdomo unaonuka.
  Pia angalia kucha zako zipoje, kama ni chafu una balaa wewe!

  JALI MUDA
  Jitahidi kuwepo mahali mlikubaliana katika muda muafaka, kama ni mara ya kwanza na umemuweka dada wa watu akusubiri zaidi ya saa nzima huwa haipendezi pia ni dalili kwamba hupo makini. Hata kama umechelewa kuna dhalula karibu kumpigia simu na kumueleza sababu na utafika muda gani. Siyo kwenda kujieleza baada ya kufika huku umechelewa.

  USIWE MTU WA KUJISIFIA NA KUONGEA TU
  Usitumie muda wako wote kuongea habari zako mwenyewe na wewe kuongea tu bila yeye kumpa nafasi kuongea. Ni vizuri sana ukawa na hekima kuuliza maswali huku ukimpa nafasi kubwa yeye kuongea huku wewe unamsikiliza. Pia be fun, hakikisha anfurahi ila usizidishe maana inabidi usome saikolojia zake kujua ni dada wa aina gani.
  Pia hata kama lugha yako ina maneno ya ajabu ajabu uwe makini kwani kuna akina dada wengi hujiuliza hivi kama anatukana, au analalamika, au analaani hivi leo siku ya kwanza je, tukioana?
  Pia achana na habari za kuanza kuongelea mahusiano yako ya nyuma au habari za wanawake wengine unless either ni mama yako mzazi.

  TABASAMU.
  Kutabasamu ni ufunguo wa moyo wako ulivyo ndani, isijetokea dada aka smile na wewe ukawa umeweka tu ndita usoni na kuzima mdomo kama uso wa mtu anayekunywa gongo. Mwanamke anayehitaji mwanaume friendly, aliyetulia na uwe wewe kama ulivyo bila kujifanya ni mtu Fulani hivi.

  TEMBEA NA PESA
  Inatokana na sehemu ambayo umepanga kukutania na kama mwanaume ni vizuri kutembea na pesa ingawa kweli unaweza kuwa na dada ambaye ana pesa na anataka kulipa ni vizuri hiyo bill lipa wewe kwa mara ya kwanza kwani itaonesha huna uchungu na ngawira zako. Pia ukishapewa bill usiulize sana maswali yanayoonesha upo very concerned na hizo pesa just pay it tight away.
  Siyo unaenda bila pesa na bill ikija unaanza kung’aa macho na kujihurumia.

  ANGALIA TABIA ZAKO
  Jitahidi kuwa gentle, fungua mlango kwa ajili yake, unapoongea mwangalie usoni siyo kifuani. Jiamini hata unapoongea ongea kama mwanaume ambaye ni source of woman’s happiness. Unaweza kumgusa wakati unaongea ila uwe makini kumsoma kama kweli anafurahia kwani this is your first time, kuna wanawake wanapenda kuwa touched.
  Pia uwe makini usiwe mtu wa ku-force mambo kwa maana kwamba unataka kila kitu siku hiyo hiyo kieleweke.
  Hapa unafungua mlango tu wa kukutania mara kwa mara na kufahamiana kwani akipendezwa na wewe leo basi kesho atataka mkutane tena na ndipo unaweza kuanza kuingiza topic zako maana sasa mmeanza kuzoeana.

  UKICHEMKA JUU YAKO MAR A POCHI NIMESAHAU LOH
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Wao hawatumii simu kuwasiliana.
  [h=3]Wana cheat na hawakamatwi, why?[/h]

  [​IMG]Wao hawatumii simu kuwasiliana.

  [FONT= ]Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine[/FONT]​
  [FONT= ]HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
  Mara nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
  Kwa kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji anapata.[/FONT]​
  [FONT= ]HAWATUMII SIMU
  Wanaume wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi, nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.[/FONT]​
  [FONT= ]WANALIPA CASH BILA RISITI
  Kawaida hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea). Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda na jinsi alivyotumia pesa.
  Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]WANABANA MATUMIZI
  Kawaida cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa so mambo ya pesa wapo makini sana.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]HAWADANGANYI OVYO
  Hawana tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
  Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.[/FONT]​
  [FONT= ]HAWATUMII MARAFIKI
  Kawaida hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu. Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari kuzunguka ni mkubwa.[/FONT]​
  [FONT= ]WANAENDA MBALI
  Kawaida cheaters wa aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia, hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi wanamfahamu.
  <!--[if !supportLineBreakNewLine]-->
  <!--[endif]-->[/FONT]​
  [FONT= ]KUMBUKA
  Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
  Kumbuka kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]SWALI[/FONT]
  [FONT= ]Mume wangu nahisi si mwaminifu na ana cheat je ni njia ipi rahisi niweke kufanikiwa kumkamata?[/FONT]
  [FONT= ]JIBU[/FONT]
  Tumia siku nzima unamfuatilia wapi anaenda na kuwa na nani, ila Hakikisha ni siku ambayo tangu mapema umemwambia utakuwa busy sana ili ajue hutamfuatilia, hivyo kwa kuwa upo busy ataamua kwenda kujirusha kama kawaida yake.


  [FONT= ]Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine[/FONT]​
  [FONT= ]HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
  Mara nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
  Kwa kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji anapata.[/FONT]​
  [FONT= ]HAWATUMII SIMU
  Wanaume wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi, nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.[/FONT]​
  [FONT= ]WANALIPA CASH BILA RISITI
  Kawaida hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea). Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda na jinsi alivyotumia pesa.
  Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]WANABANA MATUMIZI
  Kawaida cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa so mambo ya pesa wapo makini sana.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]HAWADANGANYI OVYO
  Hawana tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
  Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.[/FONT]​
  [FONT= ]HAWATUMII MARAFIKI
  Kawaida hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu. Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari kuzunguka ni mkubwa.[/FONT]​
  [FONT= ]WANAENDA MBALI
  Kawaida cheaters wa aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia, hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi wanamfahamu.
  <!--[if !supportLineBreakNewLine]-->
  <!--[endif]-->[/FONT]​
  [FONT= ]KUMBUKA
  Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
  Kumbuka kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt.[/FONT]​
  [FONT= ]<!--[if !supportEmptyParas]--> [/FONT]​
  [FONT= ]SWALI[/FONT]
  [FONT= ]Mume wangu nahisi si mwaminifu na ana cheat je ni njia ipi rahisi niweke kufanikiwa kumkamata?[/FONT]
  [FONT= ]JIBU[/FONT]
  Tumia siku nzima unamfuatilia wapi anaenda na kuwa na nani, ila Hakikisha ni siku ambayo tangu mapema umemwambia utakuwa busy sana ili ajue hutamfuatilia, hivyo kwa kuwa upo busy ataamua kwenda kujirusha kama kawaida yake.
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  [h=3]Hasira Huimarisha Ndoa[/h]

  Linapokuja suala la hasira hakuna cha mweupe wala mweusi, hakuna cha mfupi wala mrefu, hakuna cha mnene wala mwembamba;
  wote tunapata hasira na tunatofautiana katika kuithibiti hasira.[​IMG] Hasira ni hisia asili ambazo humtokea mtu yeyote.
  Na hasira ni mwitikio wa mtu kutokana na hisia za usalama wake, furaha yake au amani yake na kila mmoja wetu amewahi kuwa na hasira na inawezekana hata sasa hivi unaposoma hapa bado una hasira ambazo zimekujaa kutokana na kuudhiwa bosi wako, mume wako, mke wako, mchumba wako, kiongozi wako, rais wako, watoto wako, wanafunzi wako au kitu chochote.

  Watu tunatofautiana sana linapokuja suala la kiwango cha hasira na jinsi ya kuiyeyusha hiyo hasira.
  Wapo watu akipata hasira hata kuongea hawezi kabisa na wengine wanakuwa wepesi hata kuzipiga, wengine akiwa na hasira anazira kabisa kufanya kitu chochote.
  Migomo mingi mashuleni na makazini wengi huongozwa na hasira ndiyo maana wakati mwingine hufanya vitu vya ajabu.
  Na wale waliopo kwenye ndoa naamini wanajua mengi sana kuhusiano na neno HASIRA kwani kupata hasira katika ndoa ni jambo ambalo halikwepeki kwani mnakutana watu wa malezi tofauti na aina tofauti ili kuwekana sawa lazima kuna vitu mmoja hatapenda na wakati mwingine kupata hasira.
  Wengine akishakuwa na hasira kama ni kwenye ndoa basi ujue umeumia na ni kasheshe kwelikweli, maana kulala ni mzungu wa nne, chakula utajijua mwenyewe, inakuwa vita ambayo huna jinsi.
  Wapo ambao pia akiwa na hasira ni kilio utadhani kuna msiba.
  Kuna wengine ni mashujaa wa kukaa na hasira zaidi ya wiki, wengine zaidi ya mwezi na wengine zaidi ya mwaka pia wapo wengine hasira zao huishi kwa muda kidogo sana na hasira zikiisha anaweza kukuomba msamaha mara moja.
  Na wengine akipata hasira atakununia tu hata kukusalimia hana mpango.

  Hasira zinajenga au kubomoa na hili linatokana na mwitikio wako ukipata hasira.
  Tatizo si kuwa na hasira bali ni jinsi gani una react ukiwa na hasira.
  Watu wanaojifunza mambo ya hasira wamepata data zinazoonesha kwamba watu waliopo kwenye ndoa ndiyo wenye hasira mara kwa mara kuliko taasisi yoyote duniani.

  Uthabiti wa ndoa unategemea sana ni jinsi gani wanandoa wana deal vipi wakiwa na hasira kwani ndoa nyingi zimekuwa hell kwa sababu ya wao kushindwa kuthibiti hasira zao.

  IMANI POTOFU KUHUSU HASIRA
  Kama kwa nje unaonekana huna hasira basi huna tatizo na hasira.
  Ukijifanya huna hasira basi hasira huondoka yenyewe.
  Kuwa mwema muda wote ni njia ya kuonesha kwamba hasira haiwezi kukuumiza
  Ndoa yako itapata shida kama utaonesha kwamba umekasirika.

  Wataalamu wa mambo ya hasira wanakiri kwamba hasira ni kitu kizuri kwenye mahusiano ya ndoa na ni kitu ambacho kipo katika ndoa zote na kwamba hasira huimarisha ndoa na huimarisha pale tu mnapotatua tatizo la hasira kwa njia ya kuelewana.
  Kila mwanandoa ana haki ya kumruhusu mwenzake kuonesha hasira yake, kujieleza kwamba umekasirika na kueleza nini kimesababisha kupata hasira.
  Kitu cha msingi ni wewe mwenye hasira kueleza kwa upendo, hekima na busara kwa mwenzako kwa nini umekasirika na nini kimesababisha upate hasira.
  Unapopata hasira ni vizuri kuelezea hasira zako kwa maneno ya upole na kwa sauti ileile kama vile unapoongelea mambo mengine ukiwa na mpenzi wako.
  Pia ni vizuri kwa mwanandoa kumsoma mwenzako mwitikio wake akiwa na hasira unatakiwa kufanya nini. Wapo ambao akiwa na hasira kaa mbali kwani baada ya muda hasira zake kuishi ndipo mnaweza kukaa na kujadili.

  Kujua mwenzako amekasirika na kumruhusu kuelezea hasira zake tena kwa upole na moyo wa upendo ni vizuri kwani utakuwa mwanzo wa kujua tatizo lilikuwa ni nini hadi kupelekea yeye kukasirika na kujua tatizo ni kitu kizuri kwani utafanya juhudi kutorudia tena.

  JINSI YA KUONDOA HASIRA
  Kwanza ni kukubali kwamba una hasira yaani mwenzako ajue una hasira, ingawa ni rahisi sana kujua mke au mume wako sasa ana hasira.
  Kwa kuwa una hasira usikubali kumaliza hasira zako kwa kuanza kumlaumu mwenzako.
  Elezea kwa utulivu na upole kabisa kwa nini una hasira na kitu gani kimesababisaha upate hasira.
  Jitahidi kuchukua hatua, fanya kitu ili kuondoa tatizo lililosababisha uwe na hasira.

  KUMBUKA!
  Pia maandiko yanasema:
  Mwe na Hasira, ila msitende dhambi;
  jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.
  (Efeso 4:26)


   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  FREE OF CHARGE-MIAKA 50 YA NDOA NA JF  Mwanamke akiwa controlled hawezi kujiamini; kutojiamini kunamfanya kila anachofanya asiwe na uhakika,
  Na kutokufanya vitu kwa uhakika matokeo yake ni kuishi maisha ya upweke[​IMG] Wengi wanaamini kwamba kuolewa au kuoa ni kuondoa upweke, ukweli ni kwamba unaweza kuolewa au kuoa na ukaishi ndani ya upweke uliokithiri.
  Wapo wanandoa wengi wanaishi katika upweke mbaya zaidi kuliko wale ambao hawajaoa wala kuolewa.

  Tabia ya kupelekeshwa (controlled) imekuwa ni tabia ambayo wanaume wengi (si wote) katika jamii za kiafrika umedumu kwa muda mrefu na bado ipo.
  Tabia ya kupelekesha hujionesha kupitia hisia za manano, matendo na ishara na watu wenye tabia ya kupelekesha.
  Wapo ambao huanza tabia ya kupelekesha tangu kuanza kwa mahusiano na kwa kuwa wengi hudhani tabia kama hizo zitakuja kubadilika huchukulia ni suala dogo sana.
  Huanza kwa kukupelekesha na vitu anavyokupa kama zawadi, muda wako, wakati mwingine hata kama hujafanya kosa anakwambia wewe kwamba ndiye muhusika na umesababisha.

  Mwanandoa anayepelekesha mwenzake kawaida haridhiki na kazi na mambo anayofanya mwenzake na huonekana kama vile mwenzake hajafikia viwango vinavyotakiwa kuishi pamoja. Mwenzake haruhusiwi kununua kitu, haruhusiwi kuleta rafiki, haruhusiwi kutumia pesa hata kidogo bila yeye kujua, haruhusiwi kuwa na marafiki, haruhusiwi kufanya chochote bila ruhusa.
  Na wengi ya watu wanaopelekesha wenzao huwa na masauti makubwa, ukimbishia anatoa sauti kubwa hadi unanyamaza mwenyewe.

  Bahati mbaya ni kwamba wengi ya wanao wapelekesha wenzao huwa hawajui kama wanachofanya ni kuwapelekesha bali ni kuwapenda na kuwalinda.
  Wapo wanawake au wanaume ambao wapo katika mahusiano na wanajitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri, hata hivyo kwa kuwa waume zao au wake zao ni watu ambao ni controlling, juhudi zao za kuimarisha ndoa na maisha kwa ujumla huishia katika kujuta na kujiona wapweke.
  Ni muhimu kujadili na mume wako au mke wako kama mmoja anahisi anapelekeshwa.
  Na kama ni ndiyo basi fanya mabadiliko badilika.
  Wapo wanandoa akisikia mwenzake anasafiri au hatakuwepo basi anajiona raha sana, sababu kubwa ni kwa kuwa anayeondoka ni controling, anampelekesha, anamnyima uhuru, demanding, msumbufu, dikiteta.
  Je, ukisikia mke wako au mume wako anasafiri utajisikiaje, huru au mpweke?
  Jibu unalo na jibu linaonesha unapelekeshwa au la.   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Really??
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Huna haja ya kuingilia, ndo maisha waloyachagua.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  PAMOJA NA HASIRA HUIMARISHA NDOA LAKINI NOMA PALE MNAPOKASIRIKA WOTE HATARI

  [h=3]Ktk Ndoa msikasirike wote[/h]

  [​IMG]
  Hawa ni Bwana John na mke wake Betty Deep River Canada waliponikaribisha nyumbani kwao walinifundisha mambo mengi kuhusu ndoa.


  Ni jambo lisilopingika kwamba ndoa zina raha yake na utamu wake hasa kila mmoja akimtanguliza mwenzake na kufuata misingi sahihi ya kuimarisha upendo, furaha na amani katika ndoa.
  Ni mafanikio ya ajabu sana kwa jamii za leo kuona watu wanasherehekea kufikisha miaka 5, 10, 15, 20, 45 na hata zaidi 50.

  Unapoongea na watu ambao ndoa zao zimeweza kuvuka milima na mabonde hadi miaka 35 ni lazima usikiliza kwa makini kwani kuna maneno ya hekima na busara.

  Wao wanasema siri kubwa ya ndoa yao kudumu kwa muda mrefu ni kama ifuatavyo:
  Msikasirike wote kwa wakati mmoja.
  Kama unataka kulaumu basi fanya kwa upendo wa hali ya juu sana.
  Usikumbushie makosa ya nyuma.
  Ni vizuri wakati mwingine kuachana na ulimwengu wote lakini si kuachana ninyi wawili.
  Usiende kulala huku mmoja akiwa na donge moyoni.
  Hakikisha umempa mwenzako sifa kwa kazi moja aliyofanya angalau kwa siku mara moja.
  Kama umefanya makosa, kubali na omba msamaha.
  Ili kugombana wanahitajika watu wawili tu, hivyo chunga sana.
  Wakati umekosea kubali na wakati upo sahihi kaa kimya.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  Try!! Utafurahia mwenyewe mpwa
   
 13. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Much appreciated mkuu,

  ".....muheshimu mke/mume wa ujana wako...."

  Zile kauli za Kipya Kinyemi japo Kidonda zisipewe tena nafasi katika jamii yetu. Well said Pdidy!!
   
 14. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waoooh sasa najua why
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  haaahaaaa your real great
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  mke wangu achoki kunikumbusha tangu tuanze kupanda ndege usshawai ona tunashuka na viti
  nkamwambia hapana akaniambia ukiona hivyo ujue leo nikalia hiko anakuja mwingine siku nyingine nikipanda nakalia hiko hiko
  so unakuwa umebadilisha nini??la
   
 17. V

  Vonix JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wengi tunadhani hivyo,ingawa kiukweli muhusika mwenyewe ndiye anayetakiwa kubadilisha hiyo altitude hata ukapata ushauri toka kwa mchungaji au aliyewasimamia ndoa yenu bado haitasaidia kama moyo wako haujakubali kurudi maana tukumbuke hata wao hao wasuluhishi huenda wanamatatizo kwenye ndoa zao kwani wao pia ni wanadamu.
   
 18. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  jamani mbona majaribu sasa?
   
 19. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yoa the best
   
 20. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mwanamme ana mbavu pungufu ya mwanamke, source,,, Mwanzo.
   
Loading...