Kwa wale wana JF wenzangu wenye kutegemea maji ya visima watapata tabu saana kuvilipia

stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,227
5,132
Kwa wale wana JF wenzangu wenye kutegemea maji ya visima watapata tabu saana kuvilipia
IMG_5003.JPG

Yaani kuwa na visima vingi nchini ndio inawapa mamlaka ya kuwakwamua wananchi?
Ingekuwa busara wenye visima wakapewa hela juu kwa kusaidia jamii.

Wao kama wizara wameshindwa kuweka mabomba nchi nzima halafu wanataka tozo kwa kisima khaa
Yaani wahenga tunakumbuka miaka ya 60 na 70 maji yalikuwa kila nyumba
 
Serikali inakosea sana kwenye hili, mita 15, sehemu zingine lazima uende chini zaidi hadi mita 60 kupata maji.

Wajikite zaidi kuangalia usalama wa maji, sio kuwasumbua wadau.

Maji ni uhai, ni muhimu sana ili kuishi, kuoga, kupika, kunywa, usafi wa nyumba, tuwe na utu, ubinadamu.

Serikali iangalie upya hili wazo/ sera yao.

Baadhi ya waliopewa madaraka ni kama kichwani wana tope
Raia wakifanikiwa, wao wanatumia mafanikio ya raia kutafutia umaarufu kwa wakubwa wao, tusipokuwa makini itafika wakati watatoza ada kwa maji ya mvua ya kuvunwa, itafika wakati watatoza ada kwa wamiliki wa matank ya kuhifadhia maji, solar panels nk.... alimradi tu wamfurahishe mkubwa

Nilitegemea wafanye kinyume chake, kila anayekuja na solution ya tatizo fulqni katika jamii, apewe ruzuku, ingesaidia sana katika kuisaidia serikali kwenye kufikisha huduma zilizoshindikana kwa raia wengine tena kwa haraka zaidi, hao wenye visima wangewezeshwa wangesambaza maji kwa haraka maeneo ambayo serikali imeshindwa, kwa mwendo huu wa kukamua wananchi hatutakwenda mbali,
 
They are thinking to tax life itself, poor them!

Profesa hajajibu swali, kaulizwa iwapo je mtu ana kisima kina urefu wa zaidi ya mita 15 lakini maji anayotumia ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani tu ( kunywa, kufulia na kupikia) je atahitaji kulipia?. Kakwepa hili swali.

Hili swali ni zuri na la msingi kwa sababu siyo kila sehemu maji yanapatikana ndani ya mita 15
 
Kisima ambacho hakizidi mita 15 ni cha mkono, kiuhalisia dar tumechimba vya kuanzia mita 80, atoe majibu either tufukie tuendelee kupata tabu au wanatutoza fine kiasi gani, then na sisi tuende mahakamani kudai huduma za maji kama hizo zilizopo ikulu tupate na huku mbagala
 
Wakati mwingine kwa haya majibu wanayotoa hawa viongozi wetu, sometimes unaweza kudhani kuwa lile wazo la waziri mmoja wa Kijerumani anayeomba kuitawala tena Afrika lifanikiwe tu. These guys wanaotuongoza are a total failure!
 
Haya ndio madhara ya kuikumbatia ccm
Wengi hawakua wakiamini kua yatatupata wote

Sasa hakuna kulalamika nikutii matakwa bila shuruti hakuna nama

Baadae itakuja pia tozo ya kuangaziwa na jua tozo ya kupua

Mtaewa tu
 
Niliposikia pombe kamteua gavana ambaye si mchumi bali afisa mbobezi wa kodi..
nilibashiri haya..
*Ubunifu wa kodi za kila rangi..
*Kifo cha uchumi
 
Hawa watu sijui wanatuonaje, huduma hizo hawatoi bado tukihangaika wenyewe wanatujia na mitozo lukuki, wakati mwingine inafikia wakati unajiuliza hawa jamaa wanataka nini? Huduma ambayo ni sehemu ya majukumu yao wameshindwa kuitoa badala ya kuwatia moyo wale wanaopambana kupunguza lile gap waliloshindwa wao kuliziba ndio kwanza wanawakatisha tamaa, Mungu tusaidie waja wako.
 
Kuna visima vimechimbwa kwa ajili ya kilimo. Sijaona ufafanuzi wake kwenye kiambata cha bei ( sikuangalia video kwa kuchelea bundle langu kukata). Je, hivi navyo vinaagukia wapi?
 
Haya ndio madhara ya kuikumbatia ccm
Wengi hawakua wakiamini kua yatatupata wote

Sasa hakuna kulalamika nikutii matakwa bila shuruti hakuna nama

Baadae itakuja pia tozo ya kuangaziwa na jua tozo ya kupua

Mtaewa tu

Hakuna anayeitii SISIEMU kiufupi ni kwamba Jeshi lao, polisi wao, Usalama wa faiTa wao, NE-C yao, bunge lao, Utawafanya nini?.
Wana risasi za kutosha kwa ajili ya kila muandamanaji, lakini hawana uwezo wa kutoa maji safi na salama hata kwa nusu ya raia wao!.

Hao watu wanamuogopa Mzungu zaidi kuliko wanavyotuogopa Sisi wananchi!. ndiyo maana akiongea mzungu wanatetemeka, ila tukiongea sisi wananchi they dont give a damn!
 
Back
Top Bottom