Nimesoma nje na unavyofikiria sivyo. Sijui vyuo vingine ila niliposoma kuna paper utasema zimetoka Mars. Mwalimu analeta concept hujawahi hata sikia kupima kama kuna mwanafunzi anafikiria nje ya box na kuna watu wanapiga 100 na wengine 10.
We nakushauri usome sana tu achana na mambo kama yamefundishwa au la. Kufika chuo maana yake una uwezo wa kujiongeza mwenyewe huitaji kusukumwa. Ukiona umefeli usitafute kisigizio, tatizo sio lao, tatizo ni lako mwenyewe. Alafu sijui professor hata moja ambaye sio postgraduate.
Unasomea fani flani, sioni sababu yoyote ya kutokujiongeza na kusoma mambo kibao yanayohusika, beba kitabu all the time. Wengine tulishagraduate ila hadi leo tunajisomea kila siku kuongeza maarifa, inatakiwa iwe kama routine tu kitu unaenjoy sio adhabu. Ukifanya hivyo hatotoa swali alafu useme ni nje ya alichofundisha, jibu lazima utakua nalo.