Kwa wale mlopitia Chuo Kikuu; Ni kweli lecturers waliosoma Postgraduate wanatunga mitihani kutokana na walichofundisha?

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,881
3,636
Hivi ni kwa nini wale lecturers waliobahatika kusoma postgraduate studies zao nje ya Tanzania wanakuaga watu waelewa sana. Yaani utakuta kwenye test au UE analeta vile vitu amefundisha.Na hata kama ufaulu kwenye test utakua mbaya basi hatosita kutoka "make up".Sasa tatizo linakuja kwa wale postgraduate zao wamefanyia Tanzania....duuhhh...hawa jamaa wanakuaga na roho kama za walimu wa sekondari...Hiv ni kwanini?
 
Kwenye heading unauliza swali upate kujibiwa ila maelezo yako ni wewe sasa unasimulia!

Anyway, Chuo kikuu maswali yalishatungwaga zamani usiogope, malecturers huwa wanapoint tu kwenye database zao komaa na madesa
 
Nenda pale COET mama wa electrical mkenya flan... sijui hapendi wengine mfikie level zake utamsikia "pumbavu mnadanganyana kwenye makorido mko Ud mnachukua Engineering nani kawaambia hapa mnachukua shenzi nyie mnatafuta" yule mama ni kwiki... kule electrons kuna kijinga kimoja kifupi kinanyoa panki nacho ni shida.... haya uje mnyama bujuru
 
Kuna shida kwenye mfumo wetu wa elimu...

Malecturers wanataka mkalili mambo magumu bila hata kuelewa... wanataka kufundisha mambo mengi hata kama kwa sasa hayana umuhimu watafundisha tu...

Wanataka waonekane wao wanafahamu zaidi hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo. Na kufelisha ni kawaida.

Nakumbuka Advance tulifundishwa Biology na Mjapani ...yaan alikuwa anafundisha vitu kwa ufupi na concentration yake ilikuwa wanafunzi tuelewe...

Akitoa test inakuwa nyepesi mno na si rahisi mtu kufeli.

Nikawa najiuliza inamaana wao wanafundishwa hivyo na wameendelea na wanauelewa wa mambo mengi na kiteknologia wapo juu pamoja na maisha yao yapo advanced ila wanasoma vitu kwa wepesi na kizingatia practical . Ukifananisha na sisi complications nyingi lakini hamna lolote vyuoni na shuleni kwa ujumla ukienda kazini mambo mengi unakuta ni mapya na utahitaji kufunzwa upya.
 
Madogo wengi siku hizi hawajielewi, unaweza kila siku ukawa unatoa make up, imagine unafundisha hesabu watu wa business kwa mfano. Hapo usipo wakomalia kila siku test tu
 
Kwenye Department ya Molecular biology and biotechnology kuna Dr. Makene na Dr. Maeda ni wasumbufu kuliko hata ule usumbufu wa mbu.Mitihani yao ni migumu mno na huwa wanajisifu sana kukamata wanafunzi .Hata vitabu wanavyotumia ni vigumu, hebu fikiri medical bacteriology mtu anatumia bacterial pathogenesis: Molecular approach
 
Hivi ni kwa nini wale lecturers waliobahatika kusoma postgraduate studies zao nje ya Tanzania wanakuaga watu waelewa sana. Yaani utakuta kwenye test au UE analeta vile vitu amefundisha.Na hata kama ufaulu kwenye test utakua mbaya basi hatosita kutoka "make up".Sasa tatizo linakuja kwa wale postgraduate zao wamefanyia Tanzania....duuhhh...hawa jamaa wanakuaga na roho kama za walimu wa sekondari...Hiv ni kwanini?
Nawe ni msomi?. Daaah tulia usome.
 
Wao nao walifanyiwa hivoo
Sishangai hata ss tunaofanyiwa hiv nasi tutalipiza kwa tutakao wafundisha
Hatar saana
 
mbele ni mbele tu, hao wanafanya waliokua wanafanyiwa huko mbele ukifeli basi we mzembe, nenda CoET pale kuna mtu anaitwa Msemwa P.B tokea bachelor hadi Phd kasoma udsm alikua anashika watu utadhani mitihani yake ina gundi
Hv bado yupo
 
Nimesoma nje na unavyofikiria sivyo. Sijui vyuo vingine ila niliposoma kuna paper utasema zimetoka Mars. Mwalimu analeta concept hujawahi hata sikia kupima kama kuna mwanafunzi anafikiria nje ya box na kuna watu wanapiga 100 na wengine 10.

We nakushauri usome sana tu achana na mambo kama yamefundishwa au la. Kufika chuo maana yake una uwezo wa kujiongeza mwenyewe huitaji kusukumwa. Ukiona umefeli usitafute kisigizio, tatizo sio lao, tatizo ni lako mwenyewe. Alafu sijui professor hata moja ambaye sio postgraduate.

Unasomea fani flani, sioni sababu yoyote ya kutokujiongeza na kusoma mambo kibao yanayohusika, beba kitabu all the time. Wengine tulishagraduate ila hadi leo tunajisomea kila siku kuongeza maarifa, inatakiwa iwe kama routine tu kitu unaenjoy sio adhabu. Ukifanya hivyo hatotoa swali alafu useme ni nje ya alichofundisha, jibu lazima utakua nalo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom