Kwa wakina dada mnaojiona wa mjini

Kwa wakina dada mnaojiona wa mjini

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,096
Reaction score
22,826
KURINGARINGA KUNAVYOWAPONZA MABINTI

Kuringa kwa wasichana wa kibongo ni athari za malezi. Ulaya mtoto wa kike na kiume wanakua pamoja.. wanahug, wanajuana zaidi but responsibly.. coz wanafundishwa elimu ya afya ya uzazi mapema.

Hapa kwetu binti akiwa na miaka 13 anaambiwa Usicheze na wavulana ni mashetani wakubwa, na ole wako tukukute na wavulana, utahama hapa nyumbani' Hapa binti anaanza kuwaona wavulana km viumbe hatari sana.

Akiwa na miaka 20 wazazi wanamuambia ‘Kwa kweli Sisi wazazi wako hatumpendi yule mvulana unaefuatana nae' binti anazidi kujiweka mbali na wanaume.. hapa ndo anaringa balaa.

Akiwa na miaka 25 wazazi wanaanza ‘Vipi mama? Kimya, hujatuletea mwenzio yoyote kututambulisha' hapa ndo binti akifuatwa anadengua kidogo kumbe anataka.

Akiwa na miaka 28 wazazi wanakuja juu 'Wewe vipi wenzio wote wameolewa wewe unasubiri nini' hapa ndo kile kibinti kilichokua kinakuringia kinaanza kukutumia vitext vya kipuuzi.. mara mambo, mara nimekumiss.. umenimisd my foot?

Akiwa na miaka 30 wazazi wanasema 'Tumeshakuonya
acha kuchagua wanaume.. we vipi?' binti anapanick anatamani kuolewa lakini alisharingaringa sana.

Akiwa na miaka 33 wazazi wanamuita kwa mazungumzo ‘Kuna mzee mmoja
kule Sumbawanga tumesikia anaweza kuondoa nuksi, twende tukupeleke' binti anaanza kuwaza kuvuta mume kwa tunguri wakati wakati aliringa mwenyewe.

Akiwa na miaka 38 wazazi wanamuita tena "Kuna Mchungaji Mabibo wanasema ukifunga wiki tu
unafunguliwa' Binti anafunga na kuomba mara kubadilisha makanisa lakini hafanikiwi.

Akiwa na miaka 40 wazazi wanamuambia "kuna mzee mmoja kafiwa na mkewe anatafuta mke wa kumpunguzia mawazo.. unaonaje tukupe namba zake? Hata huyo ni sawa tu.. usichague sana.. tufariji wazee wako tuone japo kajukuu'

NB: GIRLS PLZ BE CARE.. KURINGA RINGA NI HATARI KWA FUTURE YAKO
 
Kwenye maelezo yako nimengudua kuwa wewe ni fataki,,,! na umeshajaribu kufanya ufataki wako mabinti wanaotoka kwenye famalia zenye uelewa walikuongopa kama ukoma, that why umekuja kufungua thread ya kupotosha mabinti ili ufanye vzr ufataki wako,

mabinti you must be care!!
 
BAK wakati namalizia kusoma hapa naomba unipigie lile songi la "msichana wa sura nzuri kitu gani kinakufanya usiolewe"
 
Last edited by a moderator:
MankaM; Mimi ndiye nimekopiwa thread yangu.......tazama tarehe utaelewa.
 
Last edited by a moderator:
MankaM: i hope umecheki na kuona.
 
Last edited by a moderator:
Shy land; sipo hapa kupotosha kama unavyodhania.Mwisho wa siku nikuwapa fursa vijana wenzangu especially ma bi dada wajitazame nyendo zao,kwani maisha hayana formula......na kama unabisha fanya utafiti wako utashuhudia nini kinaendelea......pengine na wewe ni muhanga hapo bila kujijua kwenye hili tatizo.......kwanini uone ukaribu wa mtoto wa kike na wa kiume ni batili kwa kutumia kigezo cha sex tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom