Kwa wake tu: Wakezetu badilikeni!

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,231
Reaction score
1,496
Ilikuwa ni research ndogo. Nipo kazini mida ya saa tano. Nachukua simu yangu ya kiganjani naandika ujumbe...'Hi baby, niko busy sana, naomba saa saba unishtue niende lunch. Mis u already'. Baada ya kuandika hivyo, natuma ujumbe huu kwenda kwenye number mbili. Moja ya wife, ya pili ni mchepuko. Guess what!!!!! Saa saba on dot, simu inaita. Kuangalia ni mchepuko. Nikapokea nikaambiwa nikale. Naenda kula huku attention yote ikiwa kwenye simu, nijue my wife wangu kachelewa kwa dakika ngapi. Nimekula, nimemaliza, nimerudi ofisini naanza kazi, still attention ipo kwenye simu. Saa nane na nusu inainggia msg.....'umeshakula?'. Wakezetu badilikeni jamani.
 
Aah unakera eti unajisifia kiaina una mke na mchepuko aiseee
[emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36]
 
Mkuu pole sana aisee....ndio wake zetu hawa inabidi tuishi nao kwa akili sana halafu muda mwingine wanapelekea tuwe na 'mpango wa kando' bila kupenda yaani
 
Sasa chukua mchepuko weka ndani uone atakuaje? Kama nyinyi kamsemo kenu kwamba hakuna kampeni baada ya kushinda uchaguzi, basi nasisi hakuna haja ya kubembelezana akat ushaniweka ndani upo?
 
Sabbu wanajua wameshawekwa ndani hamna kujisumbua tenaa
 
Mkuu kwanza alijua tu unamuenjoy maana sio kawaida. Hivyo ingekuwa ni ile kitu daily hapo sawa ila siku moja ndo umletee hayo masongombingo eti nishtue sa saba nikale.. Aaahh hiyo kitu hamna..

Huo mchepuko si lazima ujipendekeze maana unajua kuwa wenyewe ni tempo hivyo unataka ujitahidi uwe pamanenti
 
Ukimchunguza sana bata
Hutamla utamuonea
Kichef chefu
 
Nilijua wewe ni binti, kumbe uko vizuri kichwani. Ubarikiwe
'Nilijua wewe ni binti,kumbe uko vizuri kichwani'

Mkuu msaada wa kauli yako hapo juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…