Nguli, umenishika pabaya. Umenikumbusha wazee waliokaa (kari) nyuma ya full suit(nyumba ya iliyoezekwa na majani ya mgomba), kina mama wako kwa mbele huku mbege ikigawanya na mzee wa heshima. Anachota kata kubwa anapelekewa mzee mkubwa zaidi kiumri, jamaa anapiga (pafu) la nguvu, mzee baada ya kuipokea anamtafuta aliye na umri mdogo kuliko yeye anamwambia (bencho/ riya) kunywa kidogo, jamaa anapiga pafu kidogo anamrudishia mzee. Daah, mzee anaipokea na kwa ustadi mkubwa anaipuliza kidogo kusogeza(miincho) ulezi pembeni halafu anaipiga kama mara tatu hivi, kwa! kwa! kwa! Zoezi linaendelea hadi watu wakikolea (mbasa) ngoma inaanza...! Kumbuka wakati huo nyimbo za dini kama TUPALIZE SAUTI ZEETU, WOTE TUMTUKUZE LEOO....zinaimbwa kwa sauti kuubwa. ni raha sana. Mimi naaza mapema kabisa kula (ngesi) dawa ya kusafisha tumbo!
hahaha kumbe ma -lavd wanajua kasoro anaweza kukutwanga ukimletea mchezo
, CHIEF MGALULA, Chrispin+, FirstLady1, Jibaba Bonge, Kyachakiche, mlachake, NEMA, Nguli, Willy
HABARI ZENU MASHEMEJI?
Mapenzi yanaenda na fedhwa hawana muda wa kuintertain midebwedo, kule stout inaendeshwa kama kawa na mandolini 110 unazijua wewe? aa wapi unajua vitz na starlet tu. ha ha ha h
, CHIEF MGALULA, Chrispin+, FirstLady1, Jibaba Bonge, Kyachakiche, mlachake, NEMA, Nguli, Willy
HABARI ZENU MASHEMEJI?
Hii thread imefanyiwa hujuma sione kabati ka thanks, uchambuzi ya kinifu bado hapo sijaweka picha ya rembonyi/sehemu ya kuchinjia ka mbuzi ya mrumu.
Hahaha! Bwashee dada alishakutengenezea machalari ya mlali (Ndizi mshale)? Raha yake ukutane na mfupa wenye mshesha (rojorojo ya kutafunika) Na utumbo. Wacha kabisa. Kule kwetu nyama haitengwi na utumbo. Raha ya aina yake.
Halafu masale kwa wingi, mengine yakichongwa kupata (UWAMBO ) mti wa kuchomea nyama. Mkia wa kondoo unachomwa mwanzo kukoleza moto huku harufu ya nyama choma ikienea eneo zima la jirani!
Sisi magonjwa GAUTI hatuzijui na nyama tuankula kilo kama 5 kwa siku huku mjini nusu kilo mtu yuko chalii hoi na vidole vimepinda hawaijui moombo/majani machungu YENYE HARUFU nzuri.Supu inawekwa (ikingi) aina ya jani chungu la kuondoa uwezekano wa kupatwa na matatizo ya tumbo pale utakapo tafuna nyama kwa wingi na mbege! Inakuwa na aroma nzuri kweli kweli.
Uko fiiti hii xsmas lazima ni onje mkiwa wa kondoo ya nyama ya kidari iliochomwa ikachanganywa kwenye damu mmbichi, kisusio na ninaweza kuvuka mipaka nikaonja MLASO kidogo, kitalolo kitakuwa chai yangu.
Juice itakuwa kivuo na nyalo.
jamani mie mbona mnaniacha solemba na hiyo mitori ,kiburu ,kitawa + kisusio
Hahaha! Ukishakolea mbege unapotea kwenda kulala. Kesho ukidamka unaenda kuzengea ngera!
Wapwa karibuni Moshi December tufanye get tugedha pale. Bia itakuwa Mbege, mdudu itakuwa mbuzi. Sore wanywaji wa banta, nyie mtakunywa nyalu (mbege togwa). Wapenzi wa maji tutawachotea kwenye mto, yale mnayouziwa lita kwa buku kule mtakunywa bure ndoo kadhaa!
Tehe tehe tehe, aika Ruwa - na mie natia timu mlimani. Najiandaa na ndafu iliyokomaa kwa kisusio mwanangu usipime. Big up wameeku na wakyeku.