Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 218
- 297
Lengo kubwa la Azimio la Arusha lilikuwa ni kuweka misingi na itikadi ya Taifa iliyojikita kwenye "Ujamaa na Kujitegemea". Kufanya Kazi Kwa Bidii ndio kilikuwa kitovu cha itikadi hii ya Ujamaa na Kujitegemea.
Waasisi wa itikadi ya 'Ujamaa na Kujitegemea' wakiongozwa na Mwanafalsafa hii Hayati Mwal. Julius K. Nyerere walikusudia kulinda Uhuru wa Taifa na watu wake katika nyanja zote; kisiasa, Kiuchumi na Kijamii japo Uhuru wa kujiamria mambo yetu wenyewe ulikuwa tayari umeshapatikana mwaka 1961 na Azimio la Arusha lilifanyika 1967 lakini tulihitaji Uhuru wa Kujitegemea na ndio maana itikadi hii ya Ujamaa na Kujitegemea ilisimikwa kama mwongozo wa Taifa.
Msingi wa Azimio la Arusha ulikuwa kupambana na aina zote za Dhulma, unyonyaji, dharau, unyonge na kutwezwa utu yaani kutothaminiwa na zaidi kupambana kuondoa matabaka Kati ya walio nacho na wasionacho (haves & have not). Yote haya yalilengwa kutekelezwa kwa kuipa serikali nguvu ya kumiliki vyanzo vikuu vya Kiuchumi ili kusiwepo na mfanyabiashara au mtu yeyote wa kuiweka serikali mfukoni yaani mtu kuwa na jeuri zaidi ya serikali ndio suala la utaifishaji lilipoanzia.
Mwalimu Nyerere alifahamu kwamba tusipokuwa huru Kiuchumi tukategemea misaada na mikopo kutoka ughaibuni hatutakuwa huru ni sambamba na kauli ya aliyewahi kuwa Rais wa Burkina Faso Thomas Sankara, aliyewahi kuwa Rais wa Burkina Faso aliposema, "He who feeds You Controls You" yaani anayekulisha ndiye anayekutawala . Kwahiyo kwa kutambua hilo Azimio la Arusha, lilisisitiza wananchi kufanya Kazi Kwa Bidii katika uzalishaji.
Azimio la Arusha lilikuwa mwiba wenye ncha Kali sana kwa kiongozi yeyote mwenye nia ya kutaka kujipatia utajiri kwa kutumia cheo au kuhodhi Mali za umma. Azimio halikuwa rafiki kabisa kwa watu wa namna hii kutokana na miiko ya uongozi iliyowekwa katika Azimio la Arusha ambayo kwa baadhi ni pamoja na;
Cheo ni Dhamana sitakitumia Cheo changu kwa manufaa binafsi
Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa. Na miiko mingine mingi tu.
Azimio lililenga kujenga misingi imara ya uongozi bora ambao ni Moja ya nguzo kuu 4 za Maendeleo yaani Ardhi, Watu, Siasa safi na uongozi bora. Mwalimu alitaka Uongozi uwe ni Kazi ya kujitolea kama ya sadaka sio ya kufaidika kama unataka kufaidika fanya biashara sio kugombea na kutaka Uongozi kwa nguvu zote.
Mambo yalianza kunoga pale Azimio la Arusha lilipoanza kutekelezwa lakini kwenye msafara wa Mamba na Kenge nao huwa hawakosi wanaliunga humohumo kwenye msafara na hapo viongozi wa kimichongo michongo walipoanza kujitokeza kimya kimya na kuhujumu Azimio la Arusha. (itaendelea)