Part (II) Azimio la Arusha halikupendwa na halitapendwa na viongozi wa kimichongo michongo

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
May 4, 2016
218
297
____________________________
Ni kwamba baada ya Azimio la Arusha kuanza kutekelezwa, mabadiliko yalianza kutokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka Kwa uzalishaji wa chakula na bidhaa za viwandani, ongezeko la viwanda.

Viwanda kama Mwatex, Sunguratex, Mutex, General tyre, chapa kazi n.k. Ambavyo baadaye vilikufa sambamba na mashirika mengine mengi ya umma yalikufa na kubaki historia tu.

Lengo hasa la Mwalimu Nyerere na waasisi wenzake wa Azimio la Arusha lilikuwa ni kuwa huru kabisa kwa kujitegemea wenyewe kiuchumi huku mkazo mkubwa kwa wananchi ukiwa ni KUFANYA KAZI KWA BIDII na kwa PAMOJA, KIDUGU, KIRAFIKI, KIJAMAA (UJAMAA).

Waliamini kama wananchi watafanya kazi kwa bidii, Kwa umoja basi matokeo yangekuwa ni kuwa wamoja na kujitegemea kiuchumi kama nchi. Bahati nzuri kwenye kuwa wamoja na kujiona kama wote ni ndugu ndani ya Taifa , tulifanikiwa Kwa kiasi kikubwa. Mziki ni kujitegemea.

Azimio lilianza kuhujumiwa punde baada ya Azimio lingine yaani Azimio la Zanzibar ambalo wengi wanaamini Azimio la Zanzibar lilikuwa ni mshale uliotumika kutungua Azimio la Arusha ambalo lilikuwa limeshapaa japo wengine wanadai lilikuwa ni uboreshaji zaidi wa Azimio la Arusha, hilo ni jambo lingine tuliweke kando tutalijadili siku nyingine.

Kitu kilichofanya na kinachofanya viongozi wa kimichongo michongo wasilipende Azimio la Arusha ni mkazo Kwa viongozi kuhusu kumiliki Mali. Uongozi ulikuwa ni kujitoa sadaka na sio sehemu ya kujitajirisha. Mathalani;

i) Kiongozi wa chama hakupaswa kushiriki jambo lolote la Kibepari/Kibeberu.
ii) Asiwe na hisa katika kampuni yoyote
iii) Asiwe mkurugenzi (C.E.O)katika kampuni yoyote
iv) Asiwe na nyumba za kupangisha
v) Asilipwe mishahara miwili.
Hapa viongozi walengwa walikuwa ni madiwani, wakuu wa chama, wabunge, mawaziri, viongozi wa serikali wa ngazi ya kati na ya juu.

Hapa mtu kuwa Kiongozi ulikuwa ni wito na sio tamaa. Mwongozo ulikuwa kwamba Kama unataka kumiliki mapesa mengi basi usiwe Kiongozi, Fanya biashara TU. Happy hakukuwa na rushwa kugombea uongozi, mtu akitaka kuwa tajiri anagombea nafasi ya Uongozi. Hii nchi Dira (vision) ilishawekwa, tatizo ni tamaa za wachache.

Ukiacha serikali ya awamu ya kwanza, hayati Dr. Magufuli wa awamu ya tano ndiye Rais ambaye alikuwa anajaribu kutekeleza maono /vision ya Azimio la Arusha japo ni kwa sehemu ndogo sana lakini akaishangaza Dunia Kwa maendeleo makubwa Kwa muda mfupi. Magufuli alikuwa akisisitiza kufanya kazi kwa kaulimbiu ya "Hapa Kazi Tu", ambao ni sawa na msisitizo uliokuwa umewekwa kwenye Azimio la Arusha.
Endapo akipatikana Kiongozi wa kutekeleza maono ya Azimio la Arusha hata Kwa asilimia hamsini tu ndani ya miaka kumi, Tanzania itakuwa inazisaidia nchi maskini na kutoa mikopo na kuuza mitumba kwenye mataifa mengine.

Lakini hali iliyopo Sasa ni Shaghalabaghala, Viongozi ndio wamiliki wa Makampuni makubwa makubwa! Kiongozi anamiliki vituo vya mafuta (sheli), anamiliki kampuni za mabasi na usafirishaji, Kiongozi anamiliki kampuni za ujenzi, Kiongozi anamiliki kampuni za majenereta na umeme wa upepo, anamiliki kampuni za usambazaji maji na ndio huyohuyo anatunga Sheria, ndio huyohuyo anashiriki mijadala bei ya umeme ipande au isipande, maji yaletwe kwa wananchi au yasiletwe. Je unategemea angependa Azimio la Arusha?

Kwa ufupi, Azimio la Arusha lilitaka kuondoa matabaka (social classes), kupambana na urasimu, kuweka uwiano wa maendeleo kati ya mijini na vijijini, na kila raia afurahie matunda ya rasilimali za nchi yake. Pia kutenganisha kati ya UONGOZI na MALI/BIASHARA.
 
Pia pitia kitabu Cha SIR ANDY CHANDE kiitwacho SAFARI TOKA BUKENE ameelezea vzuri Sana jinsi azimio hili lilivyoleta mabadiliko na wengi kupoteza Mali japo nchi ilinufaika ila mwendelezo wake ndyo tulifeli

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
e10c549cda2151bed1145c51370fd183.jpg
2025#wassira
 
Nimekutana na makala zaidi nazotumika kufundishia wanafunzi elimu ya dini ya kiislamu, ni lishangaa kuona Azimio la Arusha lilipingwa na wameandika kwamba " lilitumika kuua uislamu nchini hasa kwa kuwapora shule na mahospitali yao" ukweli nimeshangaa kuona kumbe ubinafsishaji ulikua kwaajili ya kufifisha uislamu.
 
Hao jamaa uwezo wao wa akili huwa na wakutili mashaka sana.

Ukisoma kitabu cha miaka 10 baada ya azimio la arusha mwalimu Nyerere alielezea mengi sana na kwa upana.

Sema hao jamaa wana mambo yao tu...ni wivu tu unawasumbua ukiongeza ujinga na umasikini ndio shida zaidi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu huenda unayoyasema ni kweli....ila Uislam unasisitiza sana Watu kusoma na kupambania haki na maendeleo
 
Hao jamaa uwezo wao wa akili huwa na wakutili mashaka sana.

Ukisoma kitabu cha miaka 10 baada ya azimio la arusha mwalimu Nyerere alielezea mengi sana na kwa upana.

Sema hao jamaa wana mambo yao tu...ni wivu tu unawasumbua ukiongeza ujinga na umasikini ndio shida zaidi.

#MaendeleoHayanaChama
Waislam wana akili timamu sana Chief...na Uislam ndio Dini sahihi katika mgongo huu wa Dunia,usiuchafue Uislam na Waislam kwa makosa ya Watu wachache walio beba ujinga
 
Back
Top Bottom