Kwa upigaji huu hatutokubali. Mhe. Rais tunakuaminia na tunatamani useme neno tu, tunaamini pesa watatulipa na watairudisha Wathamini wa Jiji

Jacobo John

Member
Apr 5, 2020
19
2
Hizi ni barua kutoka Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, tuliwahi kuambiwa kuwa eneo letu lililipwa fidia mwaka 1985 likitambulika kama kiwanja namba 2 Madenge.

Watanzania wenzetu tunaomba mtusaidie, mwaka 1985 Ardhi ilikuwa inalipwa fidia? Pili kiwanja kinachotajwa kipo kilomita zaidi ya tano kutoka eneo letu. Eneo la Madenge kwa wenyeji wa Dodoma lipo usawa wa Shule ya Elshadai upande wa Jeshi kwenye kilima huko mji wa Serikali umefika lini wakati mji wa Serikali upo Mtumba.

Kama eneo lililipwa fidia mwaka 1985 uthamini wa mwaka 2016 ulikuwa wa nini? Cha ajabu wanaosadikika kuwa wenye eneo JWTZ ndio waliofanya uthamini wa eneo letu lililopo Mtumba. Pia, wakati wa makabidhiano kwa Nini hawakusema eneo Hilo lililipwa fidia mwaka 1985 hadharani nasi tukasikia tungemalizana pale pale.

Lakini walichukua eneo na madai yetu na Waziri wa TAMISEMI alikubali na kusema Serikali italipa, pia Mhe. Rais akitamka wakati wa uzinduzi wa mji wa Serikali kuwa ameambiwa Kuna watu wanadai fidia katika eneo hilo wawe wavumilivu watalopwa sasa hizi barua za kukataa kulipa zinatoka wapi? Pia, tunajiuliza TZ kuna wenye kauli dhidi ya Mhe. Rais Magufuri ama Rais huwa anapewa taarifa za uongo?.

Wataalamu hawa niwasumbufu sana na wamekuwa kikwazo. Pia, Ofisi ya RAS nao inawataalamu imeshindwa kubaini eneo la Madenge lipo wapi? Wizara ya ardhi nayo inashindwa kutambua kiwanja namba 2 Madenge kipo wapi? Ndio maana sisi tunaamini kuwa Serikali imehujumiwa pesa zake na watu wachache na tunaiomba kama ambavyo imekuwa ikichukua hatua katika Halamashauri zingine ije na Dodoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom