Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,466
- 2,860
Mkuu,Nakubaliana na wewe kuhusu kutoa ushauri japo uzoefu unaonyesha kuwa kwa serikali hii kutoa ushauri usiopendwa at best utapuuzwa and more likely mtoa ushauri utaingia matatani.
LAKINI sikubaliani nawe juu ya kukomaa kwenye kuendelea na mradi unaoonekana wazi hautaleta tija kwa taifa. That is throwing away good money after the bad.
Usafiri wa reli na meli duniani kote, gharama zake ziko chini sana ukilinganisha na usafiri wa barabara. Hata sasa, jaribu kufanya order ya bidhaa hata kama hutanunua, then omba quote ya usafiri wa either 20ft/40ft container toka China mpaka bandari ya dar.
Then tafuta wasafirishaji wa hapa hapa bongo, uliza gharama za container hilohilo toka Dar-Mwanza; gharama ni mara 3 au 4 ya gharama ya kusafirisha toka China mpaka Dar. Ila kwa kutumia reli, gharama huwa ziko chini mno.
Tukipunguza gharama za usafirishaji wa malighafi au bidhaa mara baada ya SGR kukamilika, gharama ya vitu madukani pia itapungua. It is simple logic mafuta ya diezel/petrol kwa Dar na Tanga bei iko chini kuliko Mwanza au Bukoba. Simple reasoning gharama ya usafirishaji kwa maroli tunafidia wanunuzi wa mwisho.
Lengo la SGR ni zuri sana tu. Ila tunawajibu wa kushauri mambo gani mbadala yafanyike wakati huu kama source ya kuongeza uzalishaji kwenye mambo ambayo tuna deficit kubwa na tunategemea imports kama uzalishaji wa samaki, uzalishaji wa maziwa na kusindika, uzalishaji wa mayai... Haya ni mambo ambayo tukiweka mifumo ya kuwa na industrial farmers vijana wetu watapata ajira kwenye organized production pattern. Then tokea hapo tunawekeza kwenye mazao ya viwanda vya ndani na ku-export finished products. SGR itahusika kwenye mchakato wote huu. Hatuwezi kuikwepa. Mjerumani alikuwa na akili na alijenga RELI ya kati na ilimnufanufaisha mpaka sisi tumeikuta