Kwa ujasiri wa kukamata Panyaroad 100 kwa muda mfupi huyu DC Jokate apandishwe Cheo kuwa Mkuu wa mkoa wa DSM!

Huyu Mwananchi mkuu wa Wilaya ya Temeke mh Jokate baada ya kuonyesha utumishi uliotukuka kuwashughulikia Panyaroad anastahili kupandishwa kuwa RC DSM

Sabato njema!
Ebu John tuache, alafu unywe chai, tulia kwanza, ww una jump into conclusion kubwa kubwa tu hata kufikiri kidogo? Ogopa sana mtu anayefanya maamuzi makubwa kwa pupa bila kufikiri.. Ebu kaa chini, tulia John, una nini? John ebu jina hili lifanyie ukuu
 
Hahaha........wewe utakuwa Makolo wa Msimbazi
 
Hahaha........wewe utakuwa Makolo wa Msimbazi

Mie Yanga, 100%, ila John, yaani umekaa chini, ukawaza, hadi ukaanza kuandika, tujue kwamba umefikiria Jokate awe RC, John kweli? Basi, mm naanza kuwa na wasiwasi na uwezo wako, au umri mwenzetu? Au tatizo limekuanza, afya ya akili au mazingira au pombe au umehongwa au una mapenzi au nn John? Kweli? Ebu tulia John
 
Sidhani kama anastahili, hili janga limeanza polepole wote wakiwa wanajua si mkuu wa wilaya, RC, makananda wa polisi wa wilaya wala kanda maalum.
Wakaliacha likakua watu wakajeruhiwa na wengine roho zikaacha mwili ndio wanaamka.
Ni mambo ya hovyo sana haya kwa sisi waafrika hatuwezi kuwa pro active.
 
Mkuu yaani Mama tu mwenyewe mpaka sasa kutuacha hoi kwa gharama za maisha kupanda,sasa unapendekeza utopolo tena kwa Dar,dah!
 
Huyu Mwananchi mkuu wa Wilaya ya Temeke mh Jokate baada ya kuonyesha utumishi uliotukuka kuwashughulikia Panyaroad anastahili kupandishwa kuwa RC DSM

Sabato njema!
Mkuu Yohana Mbatizaji, johnthebaptist , naunga mkono hoja, yako hii, Kwa ujasiri wa kukamata Panyaroad 100 kwa muda mfupi huyu DC Jokate apandishwe Cheo kuwa Mkuu wa mkoa wa DSM!, hivyo nashauri, akitoka ile likizo, apandishwe cheo, kutoka kuwa DC hadi kuwa RC, na apewe mkoa but not necessarily DSM!.

Hii sio mara ya kwanza kwa sisi wana jf, kumuombea mtu cheo, hata DC Makonda, ni watu wa humu humu jf ndio waliomuombea cheo
akawa RC. Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
P
 
Rudisheni machinga barabarani hali tete mtaani angalau iliwasaidia kupunguza makali
 
Back
Top Bottom