nguluvisonzo
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 515
- 72
wakati chaguzi ngazi ya msingi ndani ya chadema zikiendelea ghafla tunapata taarifa kwamba chaguzi hizo zimesitishwa na badala yake inaandaliwa program ya taifa kwenda kusimamia matawi,jambo ambalo ni kinyume cha katiba ya chama inayosema kila ngazi husimamiwa na ngazi ya juu yake,imekuwa ni desturi ya chadema makao makuu kuhodhi na kujilimbikizia majukumu yote ya chama hata yale ya ngazi ya chini kabisa kwa lengo la kujinufaisha na ruzuku ya chama huku wakiacha mikoa,wilaya na majimbo ikiwa haina cha kufanya.kutokana na mwendo huu wa kutaka kila jukumu wafanye wao historia inaonyesha ziko program nyingi ambazo zimeshindwa kufikia lengo kutokana na ulafi wa viongozi kama vile program ya chadema ni msingi,operesheni sangara,na leo tuna program ya M4C,pamoja na uwingi wa majukumu haya na pesa nyingi ya chama inayotumika,hawataki kugawa majukumu haya ktk mikoa na wilaya wanachoamini ni kwamba pekee makao makuu ndio wanao weza kila kitu,bila kujua kwamba wao wanajiona wanaweza kutokana na pesa wanayotumia na hao wanaowaona hawawezi ni kutokana na kukosa pesa,mods naomba ujumbe wangu huu musiuondoe uwafikie wahusika najua wapo hapa,mh mbowe,dct slaa,zitto,mnyika na wengine hebu jitokezeni mutupatie majibu
Nawasilisha.
Ile sakata ya Morogoro niliona katibu wa CDM kule mambo yaliyokuwa yaanzie ndiye alikuwa mpambanaji sana na pia alitakiwa kuhakikisha mambo yanakwenda kama yalivyopangwa,nafikiri viongozi wakuu huwa wanaacha mambo ya msingi yafanywe na wahusika na viongozi wa makao makuu huwa wanatia nguvu na kuhakisha kilichokubaliwa katika programu kinafanikiwa,wakati mwingine viongozi wa juu huingilia kutokana na uzito wa tukio.
Utaratibu huu nafikiri upo kila mahali pa kazi na vyama vyote huwa tunashuhudia hilo.
JK akitembelea Muheza kwa shuguli ya kichama watu makao makuu ni lazima wasaidie na kama kuna haja ya katibu mkuu kwenda kwenye tukio hasa kutokana na unyeti wake ni lazima atahusika mwanzo mwisho.
Tuwaache viongozi wafanye kazi kulinga na wanavyoona inafaa ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.
Tujiulize ni kila jambo wanalifanya viongozi wa makao makuu?tuwe wakweli jamani.