Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Katika hali ya kawaida bunge letu linapashwa kuwa ndicho kielelezo cha demokrasia ya kweli hapa nchini. Lakini mambo ni tofauti; hivi sasa Spika anadiriki kuwakemea wabunge kama kwamba ni watoto wa chekechea. Kwa mfano, leo hii asubuhi, baada ya waziri mkuu kumaliza kujibu maswali ya moja kwa moja, kuna mbunge aliyeomba mwongozo wa spika akitaka kujua ni hatua zipi mbunge anaweza kuchukua, iwapo kiongozi wa ngazi ya juu kama waziri mkuu, atalidanganya bunge. Badala ya kumjibu swali lake, spika alianza kumshambulia yule mbunge, akihoji iwapo mbunge yule alikuwa na maana ya kuwa waziri mkuu ameliongopea bunge; na kuongeza kuwa kama ni hivyo aiweke kimaandishi. Ni maoni yangu kuwa huo ni ubabe tu, maana muuliza swali hakusema kuwa hali hiyo tayari imejitokeza, alichotaka kujua ni kama hali hiyo ikijitokeza mbunge anaweza kuchukua hatua gani.