Kwa tulipofikia, jukumu la kusimamia maadili siyo la wazazi tu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
4,102
4,228
Tumefikia hatua ya hatari sana kimaadili na tusipochukua hatua za dhati na za haraka kwa pamoja tutajikuta katika matatizo ambayo hayajawahi kufikia hatua au kiwango tutakachokiona.

Imezoeleka kuwa jukumu la malezi ili kuadilisha ni la Wazazi kwa kiasi kikubwa na taasisi nyingine kama Dini (makanisani na misikitini), Elimu (mashuleni pia tunaona lawama wakitupiwa walimu lakini tukiangalia kwa umakini suala la malezi linahitaji mawanda mapana mno ya kiuangalizi kwa kuwa maadili huathiriwa na huathiri jamii pana na kwa maana hiyo malezi yanayotoa elimu ya maadili yanapaswa kutolewa na kila mwanajamii wa eneo husika na Serikali nayo inapaswa kulitilia mkazo na kuonesha udhati juu ya suala la maadili.

Tunaposema maadili yameporomoka kwa maana pana na rahisi ni kwamba kila mmoja wetu ameshindwa kutekeleza wajibu wake kuadilisha jamii inayomzunguka kwa sehemu yake.

Ieleweke wazi kuwa Taifa linaloshindwa kusimamia maadili yake ni Taifa linaloelekea kufa "rogue nation"na kwa picha halisi uozo wa kimaadili ndiyo unaolitia Taifa hasara kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri.Mathalani ukiangalia suala zima la ufisadi na uhujumu vinatokana na kuporomoka kwa maadili,kukosekana kwa uzalendo ni zao la maadili mabovu katika jamii yetu.

Sitakosea nikisema hata umasikini unaoonekana Nchini ni zao la maadili mabovu mathalani suala la Wafanyakazi hewa hivi waajiri wangesimamia na kusimamiwa kimaadili wangelitia Taifa letu hasara kubwa kiasi hicho?maadili yanapaswa kusimamiwa na kila mmoja wetu kwa sehemu yake na kwa dhati kinyume na hapo tutajiaminisha katika jambo lisilo na usahihi.

Hakuna wa kumlaumu ila kila mmoja anapaswa kujilaumu kwa sehemu yake juu ya hali ilivyo na kuchukua hatua za dhati kuamua kubadilika tuiangalie miiko na maadili yetu ipo namna gani na inatjutaka tuwe Watu wa aina ipi?

Tumefikia hatua ambayo kila jambo hata kama ni la kimaendeleo linalofanywa na Serikali yetu huliingizia Taifa hasara kutokana na maadili mabovu.
 
Zamani ilikuwa ukikosea mtu yeyote anakuchapa hata barabarani leo hii hata mtoto akikutukana ukamchapa unalo kwanini maadili yasishuke. Yaani siku hizi binti kwenda ni kawaida kama anaenda chumbani kwake aacha wabakwe.
 
Leo tunambiwa ukimuadhibu Mtoto aliyeonesha ubovu kimaadili eti kuna haki za binadamu na kwa bahati tunazitumia haki hizo kupotosha uhalisia.
Hali ni mbaya kila mahali maadili yameporomoka poromoko kuu Taifa linashuka hadi kila uchao,hasara inatisha lakini bado hatuambiani ukweli kwa dhati na kuusimamia ukweli huo
 
Back
Top Bottom