Kwa trend hii, kweli ipo dhati ya kuboresha huduma zetu za kijamii hasa shule na hospitali?

Mat.E

Member
Dec 28, 2010
66
13
Baada ya kuwa mshiriki wa jukwaa hili kwa muda bila kuchangia, Wakuu nimelazimika kushiriki moja kwa moja hii ni kutokana na yanayoendelea hapa kwetu Tanzania.
Wakuu tumekuwa tukishuhudia viongozi wetu mbalimbali tuliowapa dhamana ya kututumikia wakikwepa kutumia kile wanachokitengeneza wenyewe,Yaani wanatumia kile wasichokitengeneza na wanatengeneza kile wasicho kitumia!, kwa mfano, wanapotujengea shule watoto wao wanawapeleka nje ya nchi kujipatia elimu bora, wanapotujengea hospitali wao wenyewe wanakuwa siyo wateja wake, wanakimbilia ng'ambo ( kwa kisingizio cha kupata matibabu zaidi) ( tena hili liko bayana kabisa kwani hadi sasa kuna vigogo wetu wamepelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi) nk. Kwa trend hii hivi kweli utakuwepo udhati wa kuboresha huduma hizi ili Wa tz wote tunufaike nazo? Jamani Kwa kuwa kuna mchakato wa katiba mpya naona bora wabanwe na katiba tubanane hapahapa, hakuna cha kupeleka mtoto wa Kiongozi kusoma nje ya nchi au Kiongozi kutibiwa nje ya nchi. Hii mi nadhani itakuwa changamoto kwao watakuwa na uchungu, wataboresha mashule yafanane na ya kule wanakokimbilia kuwapeleka watoto wao, wataboresha hospitali, yafanane na ya India.Pia wataogopa kukimbilia uongozi, wataacha kupishana kwa wachawi kutafuta uongozi! Au wadau mwasemaje kwa hili? Nawasilisha.
 

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
347
100
mmh, labda sio nchi hii, nakumbuka kuna wakati Makamba alikwenda India, aliporudi kuna redio moja hapa nchini ilimhoji kuhusiana na safari yake hiyo, swali ninalokumbuka ni kwamba aliulizwa kwa nini alienda nje na asitibiwe nchini, alijibu ' khaaa sasa ulitaka nikatibiwe Mwananyamala?' as if wanaokwenda pale ni wanyama, ilinisikitisha sana kauli hiyo
 

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Mar 22, 2006
1,838
698
Mimi nadhani WaTZ kwa sababu ambazo mpaka sasa sijaweza kuzibaini tuna tatizo moja ya kutojali quality. Siyo kwa viongozi tu bali wananchi wote kwa ujumla. Tumejenga imani kuwa vitu bora haviwezi kupatikana hapa bali kwa wenzetu tu. Kwa mfano, tunaamini kuwa nguo bora ni ile iliyotoka nje ya nchi. Huduma bora ya kibenki inapatikana Barclays, Std. Chartered, etc. na siyo CRDB au NMB. Tunaona fahari tunapokunywa Heineken na siyo Kili, Safari au Serengeti. Tunanunua ndizi zilizosinyaa kutoka Shoprite tukiziona za Ubungo au Buguruni ambazo ni fresh siyo bora. Orodha ni ndefu. Kwa hiyo vigogo wetu kutibiwa nje au kuwapeleka watoto wao kusoma nje ni extension ya mentality hiyo hiyo. Huenda hata ukimleta bingwa yule yule kutoka India aje kutolea huduma yake hapa hapa vigogo hawataamini kuwa hiyo huduma ni bora. Ni kwa sababu hiyo WaTZ tunakubali vitu vya hovyo hovyo badala ya kudai vilivyo bora. Tumeishajiaminisha kuwa hivyo ndivyo viwango vyetu. Tunakubali kupanda mabasi mabovu/machafu, tunakubali huduma mbovu, tunakubali kukaa kwenye mazingira ya hovyo, tunalipia huduma tusizozipata (maji, umeme, n.k.). Tusilaumu vigogo peke yake, tujitazame na sisi wenyewe. Kama tungekuwa na hizo fursa tungefanya vinginevyo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom