Baada ya kuwa mshiriki wa jukwaa hili kwa muda bila kuchangia, Wakuu nimelazimika kushiriki moja kwa moja hii ni kutokana na yanayoendelea hapa kwetu Tanzania.
Wakuu tumekuwa tukishuhudia viongozi wetu mbalimbali tuliowapa dhamana ya kututumikia wakikwepa kutumia kile wanachokitengeneza wenyewe,Yaani wanatumia kile wasichokitengeneza na wanatengeneza kile wasicho kitumia!, kwa mfano, wanapotujengea shule watoto wao wanawapeleka nje ya nchi kujipatia elimu bora, wanapotujengea hospitali wao wenyewe wanakuwa siyo wateja wake, wanakimbilia ng'ambo ( kwa kisingizio cha kupata matibabu zaidi) ( tena hili liko bayana kabisa kwani hadi sasa kuna vigogo wetu wamepelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi) nk. Kwa trend hii hivi kweli utakuwepo udhati wa kuboresha huduma hizi ili Wa tz wote tunufaike nazo? Jamani Kwa kuwa kuna mchakato wa katiba mpya naona bora wabanwe na katiba tubanane hapahapa, hakuna cha kupeleka mtoto wa Kiongozi kusoma nje ya nchi au Kiongozi kutibiwa nje ya nchi. Hii mi nadhani itakuwa changamoto kwao watakuwa na uchungu, wataboresha mashule yafanane na ya kule wanakokimbilia kuwapeleka watoto wao, wataboresha hospitali, yafanane na ya India.Pia wataogopa kukimbilia uongozi, wataacha kupishana kwa wachawi kutafuta uongozi! Au wadau mwasemaje kwa hili? Nawasilisha.