Kwa tabia hizi chafu za Viongozi na Mashabiki wa Yanga, TFF wakizinduka tutaadhibiwa

"Kwa sasa TFF tushukuru wamelala au wana woga. Kitendo tulichofanya juzi uwanja wa Sokoine hakikuwa sahihi. Ifikie hatua tuwe wakweli. Ifikie hatua tuangalie mpira na mchezo wa Mpira na si Ushabiki.

Goal tulilopata kiukweli halikugusa mstari lakini refa kama binadamu alitupatia goal hilo na tukashukuru. Mbeya City penalty yao haikuwana utata why tuchochee fujo? Kwa nini hizi team kubwa zinaamini zenyewe tu zinatakiwa kushinda?

Mi nakumbuka penalty tuliyopata dhidi ya Simba mwaka jana haikuwa halali. Simba mbona hawakufanya fujo? Faulo ilifanyika nje ya box refa akaingiza ndani iwe penalty.

Simba walitulia na Onyango akaja kusawazisha dakika za jioni kwa kichwa. Simba hawakufanya fujo. Kwa nini sisi huwa tunapenda kulazimisha kila kitu?

Na makocha wameshajua saikolojia ya wanayanga. Huwa wanajifichia humo. Nao wnakimbilia kulaumu marefa ili kuficha udhaifu wa mbinu zao. Juzi ukiangalia ile match kocha aliingia na mbinu gani?

Tukumbushane kombinesheni ya Kisinda na Fiston ilikuwa ime-fail. Sarpong alikuwa anafanya mambo ya hovyo tu uwanjani. Hivi ni matches ngapi tumebebwa katika ligi mpaka kufika hapa tulipo?

Ifikie hatua tuelezane ukweli. Kama TFF inaogopa basi tusijizoeze hivi matches za kimataifa tutaumia sana. Maana hii tabia sasa ni kama inaota mizizi. Mashabiki, wachezaji na viongozi wanalazimisha ushindi au wanaamini ni lazima washinde.

Inapotokea kinyume watu wanapanic. Na malalamiko ya kipuuzi huku ukweli ni kuwa team yetu ni mbovu. Tuelezane ukweli tu.

Kama ntaonekana mimi si Yanga kwa kuandika hivi acha iwe hivyo. Niiten majina yote ila ukweli ndo humu. Na kwenye group mkitaka kunitoa mnitoe tu. Ila ukweli ntausema."
stupid from Simba!
 
Sisi Kama kamati ya saa 72 tutafanya kazi yetu...nawashauri yanga waandae muamala mapema...wao si wanajiona anorld shwaziniga..
 
Back
Top Bottom