Ujumbe kwa viongozi na mashabiki wa Simba SC

political monger senior

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
1,801
5,788
WATAKATAA KUSAJILIWA SIMBA
.
Itafika Stage Wachezaji Wazawa Watakataa Kusajiliwa Simba, Labda Kwa Yule Anayehitaji Pesa Kuliko Kucheza Mpira.

Yuko Wapi Kapama , Mwanuke ? Hivi Hawa Wachezaji Wazawa Wanasajiliwa Simba Ili Kutimiza Idadi Au Kufanyaje?

Rotation Iko Wapi?

Friendly Match Kapombe, Zimbwe Simba Day Kapombe, Zimbwe Mechi Za Mashindano Kapombe, Zimbwe, Zimbwe Na Kapombe Ni Best Fullback In Tanzania Ila Na Wao Ni Binadamu Wanachoka Wamekuwa Bora Na Bado Wako Bora Ila Wamechoka Wanatakiwa Kupumzika pia.

Kikosi Kipana Kiko Wapi? Duchu , Kazi , Mwenda , Ni Kizazi Cha Kina Job Lakini Angalia Stage Aliofikia Wao Wanapigwa Reserve,

Simba Inafanya Rotation Mchezaji Akiumia Sasa Unakuta Mchezaji Hajacheza Mechi 10 Alafu Bahati Mbaya Mwingine Kaumia Unataka Yule Ambae Hajacheza Mechi 10 Unataka Afanye Vizuri?

@robertinho7.coach Ulituambia Una Mifumo Mitatu Iko Wapi? Rotation? Mpira Wa Speed Uko Wapi?

Mechi Ijayo Ya Coastal Union Utashangaa Zimbwe Na Kapombe Wapo Badala Uwapumzishe Wajiandae Mechi Ingine Wape Chance Hawa Vijana Wengine Mwenda
Duchu Kazi Ni Wachezaji Wazuri Na Wanaweza Kufanya Vizuri Usikariri Kikosi Tuna Mashindano Mengi Sana Angalia Yanga Kuna Rotation Kila Mchezaji Anapata Chance Ya Kucheza Hii Inapunguza Pia Mambo Ya Kupigana Misumari.

Uongozi Kama Mambo Yataendelea Hivi Itafika Muda Wachezaji Wakifuatwa Na Simba Na Yanga, Atachagua Yanga Kuliko Simba Kwa Sababu Atakuwa Na Uhakika Wa Kucheza, Ifike Hatua Kusiwe Na Mchezaji Anayemiliki Namba Yake,

Miaka Ya Hivi Karibu Hakuna Mzawa Aliefanikiwa Pale Simba Lakini Angalia Yanga Mudathiri, Mzize, Bacca, Kibwana, Sureboy,Farid Na Sasa Kibabage Licha Ya Uwezo Wa Lomalisa Ila Anapata Namba Anacheza Sisi Huku Kwetu Mpaka Majeruhi Mchezaji Zinapita Mechi 10 Hajacheza Wala Hana Tatizo Lolote,

N.B
Mwanzoni Sikumuelewa Kocha Wa Taifa Stars Sasa Nimemuelewa.

MNASEMAJE
 
MTATOA KILA KILIO.
NILIPOKUWA NATOA MAONI KABLA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA.

Nilidharaulika.
Nilichekwa.
Nilitukanwa.

Mtalia Hadi muimbe Po
Niliwataadharisha mjiandae KISAIKOLOJIA lakini wapi.

Ile team changamoto ipo katika jopo la viongozi, hawana maono na uthubutu wowote juu ya mchezo wa mpira. Mtu kama Mangungu ana uwezo gani wa kukuletea mageuzi ya kimpira?

Na uongozi wote wa pale kwa asilimia kubwa umejaa watu wa aina hiyo ya Mangungu.
 
Ningetamani sana kama Jamii Forum ingekuwa ni sehemu ya VIONGOZI WA Kila SEKTA kuja na Kuokota Mawazo.

Kama mashabiki WA Simba tungeadhimia kwa pamoja mapendekezo na Ushauri wetu kwa Klabu ya Simba, Tungetoa andiko Moja na Kulikabishi kwa Uongozi WA CLABU.

Lakini Jamii Forum kwa sasa Imevamiwa pakubwa mno.

WATU tumejaza Upuuzi, UJINGA na UPUMBAVU Mwingi.
 
Ni kweli Simba ina changamoto kwa sasa.

But I think mashabiki wa Simba sasa tunachangamoto kubwa kuliko hata timu. In short hatujui tunataka nini?

1. Kocha gani hata first eleven, hapo hapo wanadai rotation ya timu.
2. Hapo hapo na nyimbo zetu;
. We want phiri😄, Hatumtaki Kibu😬
. Kocha aingie kwenye mfumo wa Chama, hapo wanataka mpira wa kasi😄
. Leo wanadai akina Mwanuke(bila kuathiri uwezo wake) ila kweli? Mechi gani ungetaka acheze? Nusu fainali na Singida? Fainali na Yanga? Mtibwa(A) PD(A)?

Swali: Zile nafasi zingetumika vyema dhidi ya P. D kungekua na kelele hizi?
 
Hapa ndipo mashabiki wa simba mnaponifurahisha. Ikitokea kocha akafanya hayo mabadiliko ya wachezaji, halafu ikafungwa! Au hata kutoa tu sare!

Mnamgeuka tena kocha kwa nini kamuacha Kapombe, Zimbwe, Chama na Kibu nje!! Mtamtumtukana na kutaka afukuzwe kazi!! Kwa hali hii lazima kocha apange kikosi kwa ajili ya kupambania ushindi.

Maana nyinyi mashabiki wa simba hamna uvumilivu hata kidogo! Halafu ni wepesi wa kulalamika. Hata timu ikishinda, bado mnalalamika!!
 
Ni kweli Simba ina changamoto kwa sasa.
Si kubwa, Kwa takwimu zipi mbaya msimu huu zinazoonyesha hizo changamoto?
But I think mashabiki wa Simba sasa tunachangamoto kubwa kuliko hata timu. In short hatujui tunataka nini?
Changamoto si kubwa kwa kiwango cha juu, ni hofu tu sababu utopolo wametuzidi kelele kuwa wana timu kubwa ila rudi kwenye takwimu.
1. Kocha gani hata first eleven, hapo hapo wanadai rotation ya timu.
2. Hapo hapo na nyimbo zetu;
. We want phiri😄, Hatumtaki Kibu😬
. Kocha aingie kwenye mfumo wa Chama, hapo wanataka mpira wa kasi😄
. Leo wanadai akina Mwanuke(bila kuathiri uwezo wake) ila kweli? Mechi gani ungetaka acheze? Nusu fainali na Singida? Fainali na Yanga? Mtibwa(A) PD(A)?
Hahaha
Swali: Zile nafasi zingetumika vyema dhidi ya P. D kungekua na kelele hizi?
Hapana. Ndo maana nakwambia ukirudi kwenye takwimu tatizo si kubwa hivyo.
 
Tunataka rotation ndani ya kikosi
MTATOA KILA KILIO.
NILIPOKUWA NATOA MAONI KABLA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA.

Nilidharaulika.
Nilichekwa.
Nilitukanwa.

Mtalia Hadi muimbe Po
Niliwataadharisha mjiandae KISAIKOLOJIA lakini wapi.

Pole mkuu
Asante..
Ni kweli Simba ina changamoto kwa sasa.

But I think mashabiki wa Simba sasa tunachangamoto kubwa kuliko hata timu. In short hatujui tunataka nini?

1. Kocha gani hata first eleven, hapo hapo wanadai rotation ya timu.
2. Hapo hapo na nyimbo zetu;
. We want phiri😄, Hatumtaki Kibu😬
. Kocha aingie kwenye mfumo wa Chama, hapo wanataka mpira wa kasi😄
. Leo wanadai akina Mwanuke(bila kuathiri uwezo wake) ila kweli? Mechi gani ungetaka acheze? Nusu fainali na Singida? Fainali na Yanga? Mtibwa(A) PD(A)?

Swali: Zile nafasi zingetumika vyema dhidi ya P. D kungekua na kelele hizi?
Umesoma nilichoandika? Mimi ninachotaka iwepo rotation angalau zimbwe na kapombe wapumzike kidogo ili na wengine wapate match fitness haiwezekani adi friend match wanacheza wale wale tu ..
 
Tunataka rotation ndani ya kikosi

Asante..

Umesoma nilichoandika? Mimi ninachotaka iwepo rotation angalau zimbwe na kapombe wapumzike kidogo ili na wengine wapate match fitness haiwezekani adi friend match wanacheza wale wale tu ..

Soma vizuri nilichoandika
Hii rotation unayoitaka isipozaa matunda, utarudi tena kumlalamikia kocha kwa nini amechezesha kikosi dhaifu na kuwaacha wachezaji wazuri nje!

Yaani mashabiki wa simba mnatakiwa mkubali tu timu yenu kwa msimu wa 3 huu haina kikosi kipana kama kile cha Yanga. Hivyo mwacheni tu mwalimu afanye vile anavyo ona inafaa. Muhimu timu inapata ushindi.
 
Tunataka rotation ndani ya kikosi

Asante..
Wana-quality na Maturity ya kutoa kile wanachotoa hawa jamaa.

Guys, ndio kwanza Msimu umeanza. Hii timu bado ina-pressure kubwa sana kutoka kwa mashabiki, hawa watoto natamani waendelee kujifua taratibu hadi pale timu itakapokua sawa au katika mechi nyepesi ndipo watacheza, otherwise wataishia kutukanwa tu, maybe utakua mwanzo wao katika safari ya kupotea kabisa.
 
Si kubwa, Kwa takwimu zipi mbaya msimu huu zinazoonyesha hizo changamoto?
Changamoto yangu kubwa na Simba ni kukosa Courage(Not Match fitness, Just Courage)or Fighting Spirit au naweza sema Wana U-father mwingi sana.

Hii kitu inafanya Simba ionekane mbovu sana.

Pia kuna changamoto Kidogo kwa robertinho, Sio mbinu wala kufundisha mpira bali Mentality yake ndiyo inamuangusha pale Simba.

Ipo hivi, wenzetu wanaamini ukitaka upate full potential ya mfanyakazi au mtu yeyote basi usim-punish kwa kosa lake ila mu-encourage kuwa bora zaidi ya pale, mfanye ajihisi ni more important kwako ....list inaendelea.

Hivyo huamini kupitia njia hii unaweza kupata vitu bora sana kwa watu hata wale ambao walibezwa na kupuuzwa na Wengi.
Angalia Mfano alichokua anafanya kwa Kibu(alikua very positive plus Zawadi juu) Tumeona matunda yake, Kibu wa sasa kila mtu amemuona.

Ila nimetambua hii njia sio bora sana na mara nyingi haifanyi kazi kwa wachezaji wengi wa kiafrika, hasa hawa wakubwa(Ki-umri).

Ukitumia hii positive approach bila kupiga kelele au kuwafokea
mbona watakuona "AUNT" watafanya wanachotaka, watacheza wanavyotaka.
Ila ukiwa mkali, kosoa, tisha au adhibu kidogo utapata matunda tu watake wasitake: angalia Sven, Gomez walikua hawataki masikhara na mambo yalikua yanaenda. Kocha wa Al ahly amefika hatua hataki hata wachezaji wake watumie Simu hasa social media kama adhabu, angalia vitisho anavyotoa Hersi kwa wachezaji wa Yanga ambao hawatajituma. Zamaleck(Kama sijakosea) wamefutiwa hadi bonas na kukatwa mshahara kabisa wachezaji. e.t.c

Hii ndio changamoto kubwa ya Robertinho, na akiendelea hivi au kushindwa kupata Support juu, Wachezaji wasimba watacheza Ki-father sana hadi pale atakapofukuzwa.

Nitakua wa Mwisho kukubali bakora zifutwe shuleni hapa Afrika. 😄
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom