Kwa tabia hii mwanamke usitafute mchawi kwanini huolewi

Kwa tabia hii mwanamke usitafute mchawi kwanini huolewi

Kifurukutu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
4,699
Reaction score
6,825
Hivi karibuni nimekutana na jamaa yangu wa siku nyingi katokea huko Arusha kaja jijini kwa ziara kikazi

Akaniambia mambo mengi na zaid zilikuwa ni story kwa nini muda wote huu jamaa hajaoa, hapo akaniambia soon atatutangazia amekwishampata mwanamke wa kumuoa na hivi akaniambia wikiend ya leo tutaingia sokoni kumtafutia pete ili jamaa akirudi huko kwao akamsaprize!

Ajabu sasa, huyo mwanamke amemnunia jamaa simu hapokei wala meseji hajibu! Sababu jamaa ananiambia ile siku tumekutana jamaa alirudi huko lodge alikofikia akiwa amechoka basi mida ya saa 3 usiku akalala usingizi fofofo, hapo ndio game ilianzia hapo

Yule demu wake amempigia simu mida ya saa 4 jamaa amelala ashindwe kupokea

Kuamka asubuhi jamaa anampigia demu kanuna! Ajibu wala kutuma sms, eti hii nayo ni sababu ya demu kununa

Jamaa kajitahidi kumtafuta hata kwa namba mpya eti demu hataki hata kumskia

Isitoshe, huyo mwanamke wameishi nae kwa muda na hatua za utambulisho katika familia zao umefanywa hivyo wanaelekea ndoa

Hapa nimeongea na jamaa vipi ule mpango wa kwenda kutafuta pete, jamaa kaghaili hataki tena

Ndio nipo najiuliza hivi huyu binti tena ameshaifikia miaka 30 akiikosa hii ndoa atamtafuta mchawi kwa huu uzwazwa wake?

"mwanaume mashine"
 
Ivi kweli ukiwa 30 ndio hata kama mwanamme akufanyie ukiritimba unyamaze tuu au kama mwanamme hafai pia uolewe tuu kisa umefika30 yrs? ni ivi mwambie na huyo jamaa nae kua awe mwanamme muelewa kama anamuona anamfaa kwenye maisha aendelee nae la hamfai ruksa kwenda, ndoa huandikwa mbinguni kama rizki yake atamuoa la ameandikiwa
kuoa mke mwengine pia sawa...
 
Always too much is harmful and harmful results into body damage.

Aendelee kudeka ukute tena ni japanese used car au second hand. [emoji3]

Mwanaume mashine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikubwa alichobugi alipaswa kujiongeza kutopokea sim sio kua mtu ana cheat bana lakini pamoja na juhudi za kumpigia na bado hakutaka kupokea hiyo siyo tena deko huo unaitwa ujinga ina mana hakumpa hata nafasi ya kujitetea?

Madame S
 
Ivi kweli ukiwa 30 ndio hata kama mwanamme akufanyie ukiritimba unyamaze tuu au kama mwanamme hafai pia uolewe tuu kisa umefika30 yrs? ni ivi mwambie na huyo jamaa nae kua awe mwanamme muelewa kama anamuona anamfaa kwenye maisha aendelee nae la hamfai ruksa kwenda ndoa huandikwa mbinguni kama rizki yake atamuoa la ameandikiwa
awe mkewe basi yataisha na atamuoa..
Sawa mkuu

"mwanaume mashine"
 
Msimlaumu Dada wa watu...

Huenda anawajua vema wadada wa dar es salaam. Wakikupata kwenye 18 zao huchomoki.

Mwacheni tuu amaind
Pamoja na hayo, lakini hawa wamefikia hatua nzuri hakupaswa kumwekea mawazo mabaya hivo, wote n watu wazima kila mtu atajichunga mwenyewe

Madame S
 
Jamaa inabidi ashukuru kwa kuwa mwanamke ameonyesha tabia yake halisi mapema, hivyo mapema tu afanye maamuzi ya kuendelea au la.
 
Ivi kweli ukiwa 30 ndio hata kama mwanamme akufanyie ukiritimba unyamaze tuu au kama mwanamme hafai pia uolewe tuu kisa umefika30 yrs? ni ivi mwambie na huyo jamaa nae kua awe mwanamme muelewa kama anamuona anamfaa kwenye maisha aendelee nae la hamfai ruksa kwenda ndoa huandikwa mbinguni kama rizki yake atamuoa la ameandikiwa
awe mkewe basi yataisha na atamuoa..
Unayoelezea ni kweli lakini upande mwingine bi dada anakosea, kwanini asipokee simu ili ajue kunani? Haya sms hajibu ndio tabia gani sasa? Ni muhimu ukishaamua kuwa kwenye mahusiano ukubali kuwa na subra, hekma, kiasi, kusamehe, heshima, adabu na utii.

Niliwahi kuchumbia bidada mmoja mrembo mzuri tu ,tatizo lake ana hasira anaweza akakukata hata na kisu, na kwa urembo wake alikuwa mjeuri sana- kwa kisa kama hicho hicho cha mleta mada hakupokea simu wala kujibu sms zangu wiki tatu niko safarini. Siku nimerejea hataki hata kukaa na mimi tuongee, pamoja na kumbembeleza saaana na kumsihi aliishia kuniambia nanukuu " mimi huwa siachwi naacha" nikaona basi isiwe tabu. Nikashika yangu baada ya kuumia sana.

Tulikaa hivo kwa takribani miezi mitatu kimya kimya, nikaizoea ile hali maisha yakaendelea. Asianze kunitumia sms ananiuliza ina maana ndio nimeachwa au? Nikawa mpole tu namjibu vizuri tu.

Ikawa akinitafuta yy poa tu nikimtafuta analeta mapozi, mwaka unakatika haeleweki mguu ndani mguu nje. Siku nilipompata wa kunifaa ndio akili zikamkaa sawa. Sio kwa kulaumu kule hadi leo hajaolewa ameishia kuzalishwa watoto watatu kila mmoja na baba yake. Eti mimi ndio nilimpa mkosi haolewi umri unaenda tu - kwendaaaaaaaaaa.

Hekima ni jambo jema sana
 
Ivi kweli ukiwa 30 ndio hata kama mwanamme akufanyie ukiritimba unyamaze tuu au kama mwanamme hafai pia uolewe tuu kisa umefika30 yrs? ni ivi mwambie na huyo jamaa nae kua awe mwanamme muelewa kama anamuona anamfaa kwenye maisha aendelee nae la hamfai ruksa kwenda ndoa huandikwa mbinguni kama rizki yake atamuoa la ameandikiwa
awe mkewe basi yataisha na atamuoa..
Riziki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom