Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

swala hili limejitokeza kwa wachangiaji wengi natarajia wanaweza kulisoma hapa

jua halizami wala haliendi chini ya dunia,linazunguka juu ya uso wa dunia, mzunguko mmoja unachukua masaa 24,ki ilivyo hasa kila kitu kipo kama tunavyokiona na tunavyokihisi, hatuhisi dunia kuzunguka hivyo ndio ilivyo haizunguki,jua lipo juu ya utosi hivyo ndio ilivyo jua haliko 93 mil miles,lipo juu ya utosi.

ngoja nitoe mfano mmoja hapa wa kuchemsha bongo,wengi wetu tunaweza tusifahamu lakini tujaribu

umbali wa jua kutoka duniani ni 93mil miles
mwangaza wa jua kufika duniani unachukua 8 mitutes, kwa hio umbali wa jua ni 8 light minute
tuchukulie kama jua lina umbali wa mara mbili zaidi 93x2=186mil mile, hapa tutaliona jua nusu ya lilivyokuwa kabla,ambapo umbali wake utakuwa 8x2=16 light minutes away
tukifanya umbali wa mara tano ya hio hesabu jua hatutaliona kabisa 93x5=465 mil miles away, sawa sawa na 8x5=40 light minutes away

swali linakuja hapa
katika nyota zote zilizo angani ambazo tunaziona,iliyo karibu sana ni 4.2 light years away

ikiwa tungeshindwa kuliona jua kwa umbali wa 40 lights minutes away, tunaziona vipi vyota zilizo na umbali wa 4.2 light years away
Labda na Mie niongezee,vingine sina wasiwasi navyo wacha Tu waniburuze, lakini Shaka yangu ni ndogo tu..Ni juu ya kipimo cha Mwangaza, yaani kina uhakika asilimia ngapi?!
Kwa maana wanasema mwangaza unasafiri megamita 300/ sekunde, sikatai ila labda kulingana na Jua letu.
Swali na Shaka langu ni Je vipi kuhusiana na nyota zilizo Mbali na Jua letu..?!
1)kwani zinawaka Kwa kiwago Sawa na Jua letu?
2)Na kama sivyo,ina maana mawimbi ya mwangaza yatatofautiana Kati ya Yale yanayopimwa kwenye Jua letu na nyota zengine. Halafu
3) vipi kuhusiana na ukinzani wa Minurisho ya mwangaza kutoka kwenye nyota za Mbali inayopita kwenye mawingu mazito(Nebula)mpaka kutufikia wanakadiriaje..?!Mtoa mada na wengine wajuzi naomba mnijuze tena maelezo mepesi Tu.
 
Ninakushukuru kwakutupatia ufahamu kuhusu Galaxy yetu, ambayo kwa kiswahili inaitwa Kilimia. Na hiyo inatufanya sisi binadamu tujione kuwa duni sana hata kama tunajiona tumevumbua mambo mengi. Na hiyo inatulazimisha kuamini kuwa Yehova Mungu Aliyeumba mbingu na ARDHI YUPO
 
elimu ya science ya ulimwengu ni elimu ya kusadikika haina ukweli wowote wala haiingii akilini kama tutakuwa na uwezo wa kufikiri,binadamu hatuwezi kuishi kwenye dunia yenye shepu ya chungwa,na kama ingekuwa kweli tungekuwa tunaweza kuishi kwenye milima mikubwa kwa kuganda pembezoni mwa milima bila ya kuanguka.

dunia haiwezi kuwa duara na maji kuganda nje ya dongo la dunia na kisha iwe inaruka angani kwa speed na masafa tunayoambiwa hii haiwezekani kabisa,katika uhalisi wa maji hayawezi kupinda kufata umbo la nje la kitu chochote,maji popote yalipo ni lazima yawe level hio ndio sifa kuu ya maji,na ndio mana tunatumia lever za maji kujengea majumba ili kupata usawa wa nyumba

jua na mwezi ni vitu vipo sawa sawa na umbali wake kutoka ardhini ni sawa sawa kama tunavyoviona,pia kama utaangalia jua na mwezi utakuta vipo ndani ya wingu la blue havipo umbali wanaosema,pia mwezi hauna ardhi ya watu kwenda kutua,tukiwa hapa tunauona kuwa mwezi ni kitu kinapitisha mwangaza(transparent),utazame mwezi mchana utaliona wingu la buluu kwenye mwezi na usiku utaona wingu jeusi kupitia kwenye mwezi.

tumefundishwa gravity ndio inayotuzuia tusipeperushwe na speed ya dunia hiki ni kichekesho kikubwa,kwanini gravity haiwezi kuzuia mabofu na mifuko ya plastic na ni vyepesi sana, kwa ufupi hakuna gravity ni vitu vizito vinabaki ardhini na vyepesi vinakwenda angani

hatuwezi kufahamu kila kitu lakini upo uwezekano kuwa ukubwa wa dunia ndio hauna mwisho(infinity) wala sio duara na haizunguki wala kuruka,uhalisi ni kama tunavyoona kila siku dunia ipo tuli imetulia.
Una kifaa cha kuthibitisha hoja yako? Tueleze kinaga ubaga kwanini jua linachomoza mashariki na kuzama magharibi kwa kwa mzunguko huo kama dunia sio duara?
 
Source mtoa post otherwise unafanya plagiarism
 
Wanasayansi wengi wamekuwa wakielezea ulimwengu wetu kuwa ni dude kubwa mno lisilo kuwa na mwisho(means the universe size is almost infinity)
Leo hebu tuchambue na kuangalia ukubwa wa dunia yetu
Kabla ya kuendelea naomba kuelezea kidogo kuhusu Galaxy, huu ni mkusanyiko wa nyota,sayari na vyote vilivyoko katika ukanda husika,Galaxy hutofautiana sana kwa ukubwa ila ya kati inakadiriwa kuwa na nyota bilioni 400 na mabilioni ya sayari,Galaxy yetu inaitwa milky way ambayo ina mabilioni ya sayari na na nyota,hebu sasa twende kwa picha
1.Hii ni dunia yetu,sehemu tunamoishi
e7986b4df1a6dcfd7bd4dbac927c3958.jpg

2:Huu ni mfumo wetu wa jua,solar system
c9cc15d9ceacb485408d64d38227c771.jpg

3.Huu ni umbali kutoka duniani mpaka mwezini
6648e54ecb397ba1b7796197f9719faf.jpg

katika umbali Huu wa mwezini mpaka duniani waweza Panga sayari Tisa na zikaenea!
b9d1c30e8299e0fe4170436c29090c2e.jpg

4.Hii ni sayari ya Jupiter ni kubwa sana
0b66cffcacac5cd083e22849f048212a.jpg

Hicho kidoti kidogo ni nchi ya kiduku(korea kaskazini)
a4af9f3b32530281e4184ea8d20c8193.jpg

5.Huu ni mwonekano wa Saturn ukiweka dunia katika ringi zake,mwonekano wa dunia sita katika ringi zake
d363ce0def4d123c246389f455408808.jpg

6.Hebu tulinganishe Jua na dunia,
Jua 1=dunia milioni 1!!!,yaani dunia kwenye jua inaingia mara milioni 1
b18457c5d884695615d8095dcc497ccb.jpg

7.Hii ni picha maarufu ya dunia iliyochukuliwa kutoka maili bilioni 4 ,hicho kidoti kidogo ni dunia
5d5ee427832ee423816e3dbd1bc9772d.jpg

8.Tuliangalia kuwa katika jua dunia huingia Mara milioni moja
fcb3df21189b9d9ea6926a457d1042a6.jpg

Hebu tulinganishe jua na nyota zingine
9.Kuna nyota inaitwa Articus ni Mara 16,000 ya jua,hicho kidoti kidogo ni jua
64b433d6d1d3b05c1731f809a5063a62.jpg

10:Kuna nyota inaitwa Alpha scropti ni kubwa Mara 690 milioni kuliko jua,hicho kidoti kidogo ni jua
a2b368b17cdfd5177a52ac4d12436df6.jpg

11.Kuna nyota inaitwa VY Canis major ni kubwa Mara bilioni 2.9
Kuliko jua,hapo usisahau kulinganisha jua na dunia!
fef7532d17719d0420b80a1a605613da.jpg

Hicho kidoti kidogo cha mwisho ni jua
12.Hebu tuangalia galaxy yetu,ni ukanda wenye nyota zaidi ya bilioni 400 pamoja na sayari zake
Ndani ya sekunde moja mwanga huzunguka dunia Mara saba na nusu,ukienda kwa speed hiyo ulitakuchukua miaka 100,000 kutoka katika ukanda wetu(milky way Galaxy)
13:milky way Galaxy ni kubwa sana,na hyo doti ya njano ni nyota tyu ambazo unauwezo wa kuziona kati ya mabilioni ya nyota
cb99f170004423544bae1d96e9f873eb.jpg

Najua umeshawishika kuona milky way Galaxy(ukanda wetu wa nyota ni mkubwa sana lakini nikuambia kuwa ni kidude kidogo sana ukilinganishwa na dubwasha kubwa la Galaxy liitwalo 1C1011,galaxy Hii ukienda na speed ya mwanga ambayo nilikueleza kuwa itakuchukua miaka 6,000,000
2e1681e59adcd87b3035e72beebb87d0.jpg

Milky way ni hicho kidoti kidogo kulinganisha na 1C1011 Galaxy

14.Hebu tuchukue Hubble telescope, picha Hii ina mabilioni ya Galaxy na kila Galaxy ina mabilioni ya nyota na sayari mabilioni pia
270ca90c1ef5a2a0ab539407f434105a.jpg

Oooh umechoka ,subiri
Hii ni dunia
06314a6385d6488cc978c347e1c4ca27.jpg

Tukizoom zaidi Hii ni solar system
07554949025788fdc0f74b2d2fe6e3a9.jpg

Tukizoom tena tunaona majirani katika solar system katika picha nzima ya galaxy
f6bb8c4146cf6f0f0ef7117edcc249d1.jpg

Tukizoom tunaona milky way galaxy ni hicho kidoti!
d1d08b6ad4f60041a5ab3166a3e29af2.jpg

Itaendelea...
Mkuu bila kusaha hayo yoote yanaeleaa katika arshii ya Mungu je arshii ya Mungu inaukubwa gani?
 
elimu ya science ya ulimwengu ni elimu ya kusadikika haina ukweli wowote wala haiingii akilini kama tutakuwa na uwezo wa kufikiri,binadamu hatuwezi kuishi kwenye dunia yenye shepu ya chungwa,na kama ingekuwa kweli tungekuwa tunaweza kuishi kwenye milima mikubwa kwa kuganda pembezoni mwa milima bila ya kuanguka.

dunia haiwezi kuwa duara na maji kuganda nje ya dongo la dunia na kisha iwe inaruka angani kwa speed na masafa tunayoambiwa hii haiwezekani kabisa,katika uhalisi wa maji hayawezi kupinda kufata umbo la nje la kitu chochote,maji popote yalipo ni lazima yawe level hio ndio sifa kuu ya maji,na ndio mana tunatumia lever za maji kujengea majumba ili kupata usawa wa nyumba

jua na mwezi ni vitu vipo sawa sawa na umbali wake kutoka ardhini ni sawa sawa kama tunavyoviona,pia kama utaangalia jua na mwezi utakuta vipo ndani ya wingu la blue havipo umbali wanaosema,pia mwezi hauna ardhi ya watu kwenda kutua,tukiwa hapa tunauona kuwa mwezi ni kitu kinapitisha mwangaza(transparent),utazame mwezi mchana utaliona wingu la buluu kwenye mwezi na usiku utaona wingu jeusi kupitia kwenye mwezi.

tumefundishwa gravity ndio inayotuzuia tusipeperushwe na speed ya dunia hiki ni kichekesho kikubwa,kwanini gravity haiwezi kuzuia mabofu na mifuko ya plastic na ni vyepesi sana, kwa ufupi hakuna gravity ni vitu vizito vinabaki ardhini na vyepesi vinakwenda angani

hatuwezi kufahamu kila kitu lakini upo uwezekano kuwa ukubwa wa dunia ndio hauna mwisho(infinity) wala sio duara na haizunguki wala kuruka,uhalisi ni kama tunavyoona kila siku dunia ipo tuli imetulia.
Naomba unijibu haya maswaili
1. Kwann sayari nyingine zipo kama tufe what is so special dunia ikatae law hiyo.

2. Kwa nadharia yako na michoro niliezee kupatwa kwa jua na mwezi.
 
Tusaidiane ukubwa wa Jua ulipimwa na nini, mpaka Dunia yetu iingie Mara Million 1?
Hata kwa Telescope ya kawaida tu unaweza kuona venus na zebaki zinapokatiza mbele ya jua,hapo ndipo unapata hesabu
 
Back
Top Bottom