Kwa nini watu wengi sio waaminifu?

Kwa nini watu wengi sio waaminifu?

Huitaji fimbo wala. Mi sijapigwa pigwa utotoni ila nidhamu ninayo sana esp. nikikutana na watu waliostaarabika.
Haha. Eti una nidhamu na wewe kumbee? Basi kama ndivyo hakuna mtu asiyekuwa na nidhamu.
 
Siku hizi mtu anaweza akaiba kazini kufika nyumbani anajisifu mbele ya waif na watoto. Unategemea Nini kutoka kwa hao watoto.
Mke anachepuka Kisha anajisifu kwa ma shosti.
Pointi sana. Ubabe umekuwa sifa ya kujivunia
 
Mifumo yote Karibia ndivyo ilivyo mwajiri kila kila kukicha anapanga amdhulumu mwajiriwa, mfanyabiashara anapanga amdhulumu mteja na mteja anapanga amdhulumu mfanyabiashara, mtoa haki anapa ga kumnyima haki anayestahili, mfanya maamuzi analenga awakandamize watu wake manufaa yaende upande wake.Hivyo ndivyo ilivyo.
Yaani upigaji kila engo sijui tukimbilie wapi siye wanyonge

Aliimba msanii mmoja hivi wakuitwa Jaguar, wimbo unaitwa kigeugeu
 
Kuna huyo fundi ambae mama kajenga imani naye lakini jamaa linamnyonya kishenzi asee

Wee fikiria mtu anamwambia bi mkubwa eti mifuko 30 kupiga nje na ndani plasta, matokeo ananunua mifuko 15 hii mingine imeenda wapi sijui.

Yaani mtu mweusi kakaa kipigaji hakuna huruma mbele ya hela hata kama unaungua na moto ili upate hela lakini mtu haoni huruma

Imani imekwisha kwakweli
 
Dunia ina mengi na huwa kuna mambo yanajirudia nafsini mwetu...."watu wanatafuta watu waaminifu lakini cha kushangaza wao wenyewe hawajaamua kuwa waaminifu sasa je uaminifu tutaupataje kwenye jamii"
 
Tatizo hapo ni kutojitambua

Mimi ni mfanyabiashara na ni mwaminifu haswaa

Miaka ya nyuma nilimtapeli mtu 20,000 kilichotokea nilipoteza the same amount tangu siku hiyo niliapa kutodhulumu cha mtu hasa kiasi kikubwa cha pesa maana malipo ni hapa hapa Duniani.

Kuna siku nilipata wateja 2 wa mkoani walikuwa wanataka bidhaa zangu, mteja wa kwanza mimi nilikuwa dalali mwenye mali alikuwa anataka 200,000 me nikazidisha 50,000 mteja akatuma 275,000 pamoja na ya usafiri na ya kutolea nilishangaa alivyoniamini simjui hanijui aliona tu tangazo langu mtandaoni na mzigo aliupata.

Mteja wa pili simjui hanijui katuma pesa ya awali Tsh 200,000 nimfanyie kazi yake baada ya siku 3 akamalizia 100,000 alafu akanielekeza ndugu yake aishie hapa Dar aupate huo mzigo alafu yeye ndio atautuma mkoani.

Cha mtu mavi
 
Huitaji fimbo wala. Mi sijapigwa pigwa utotoni ila nidhamu ninayo sana esp. nikikutana na watu waliostaarabika.
Lakini wabongo fix Sana!yaani huu uzi utafikisha comment hta 500 na wachangiaji wote watakuwa wanalalamika ukosefu wa uaminifu kwenye jamii zetu.

Sasa hapo huwa najiuliza hao wasio waaminifu wako wapi ikiwa humu JF kila mtu anadai ni mwaminifu?
 
Lakini wabongo fix Sana!yaani huu uzi utafikisha comment hta 500 na wachangiaji wote watakuwa wanalalamika ukosefu wa uaminifu kwenye jamii zetu.

Sasa hpo huwa najiuliza hao wasio waaminifu wako wapi ikiwa umu jf kila mtu anadai ni mwaminifu?
Hahahahah haufiki hata comment 100 huu.
 
Mbaya zaidi. Makanisani wazee wakihesabu sadaka wanatenga kabisa za kwao za kugawana. Kama Kuna Padre wa RC au mchungaji wa KKKT jumapili hii astukize tu achague watu watatu ambao hawajazoeana mmoja awe mwanamke, wahesabu sadaka.

Utaona sadaka itakua Mara mbili ya iliyozoeleka. Ubishi sitaki. Kama Kuna Padre au mchungaji afanye hiyo experiment mabishano alete baada ya zoezi.

Kuna wazee wengine wakihesabu sadaka lazima wakanunue soda na chips kwa hiyo kazi ya robo saa.
 
Lakini wabongo fix Sana! Yaani huu uzi utafikisha comment hta 500 na wachangiaji wote watakuwa wanalalamika ukosefu wa uaminifu kwenye jamii zetu.

Sasa hpo huwa najiuliza hao wasio waaminifu wako wapi ikiwa umu jf kila mtu anadai ni mwaminifu?
Wasio waaminifu wako FB.
 
Mbaya zaidi. Makanisani wazee wakihesabu sadaka wanatenga kabisa za kwao za kugawana. Kama Kuna Padre wa RC au mchungaji wa KKKT jumapili hii astukize tu achague watu watatu ambao hawajazoeana mmoja awe mwanamke, wahesabu sadaka.
Utaona sadaka itakua Mara mbili ya iliyozoeleka. Ubishi sitaki. Kama Kuna Padre au mchungaji afanye hiyo experiment mabishano alete baada ya zoezi.
Kuna wazee wengine wakihesabu sadaka lazima wakanunue soda na chips kwa hiyo kazi ya robo saa.
Ushauri unaletwa na Mr Deceiver! ^Dunia ina mambo!^
 
Kwenye bei pia mtu anauza kitu 5000 anakukadiria usoni anakwambia 15000

Ukilegea unatoa ila mie nataja mara moja tu hataki basi.
 
Na malezi yenyewe ya fimbo asubuhi mpaka jioni lakini maadili bado ni sifuri!!

Mi huwa najiuliza wachina na wajapan waliweza vipi kuwafanya watoto wao wawe na adabu bila kutumia fimbo?
Wenzetu wana Informal education inayoendana na tamaduni zao,
Kule wanajifunza kuwa na nidhamu ya hali ya juu,

Nilibahatika kujifunza elimu yao fulani ila kupenetrate hapa Tz ikawa ngumu,Mwenzangu wa Rwanda serikali imempa go ahead, Watatoa watoto very strict
 
Ushauri unaletwa na Mr Deceiver! ^Dunia ina mambo!^
Kaka mie Nina dhambi kweli na nazijutia dhambi zangu Ila kwenye kuiba sadaka, ama kumdhulumu mwanamke au yatima au yoyote aliye mnyonge kuliko Mimi count me out.
Kuna washenzi naweza kuwafanyia ushenzi lkn sio kundi Hilo hapo juu.
 
I get you. Ila hata hizo ndogo siyo ndogo kama unavyodhani. Afadhali zifanyie mchakato mapema tu.
 
Dawa ni kuweka sheria kali kama China ukithibitika umefanya udanganyifu ni kunyongwa tu. Tutaishi kama peponi
 
Dawa ni kuweka sheria kali kama China ukithibitika umefanya udanganyifu ni kunyongwa tu. Tutaishi kama peponi
Mkuu kwa Tz utaumiza wengi wasio na hatia.
Wewe angalia hizi kesi dhidi ya wapinzani.
Angalia bomoa bomoa ya Mbezi Kibamba, wangapi hawakuwemo? Ingekua kunyongwa?
 
Ni jambo la ajabu na linatia hasira sana.

Unapita sokoni unamwambia muuzaji niwekee nyanya au machungwa nk, usipoangalia unafika home nyingi zimeharibika kabuvisha.

Mama ntilie anakuuzia maziwa ukitia mdomoni ni maji tu hamna kitu. Kwanini asiwe bei kubwa ila maziwa ya kueleweka?

Fundi magari, kwa mfano unapeleka gari kwa fundi, tatizo ni break, anagundua labda fuse ya magneto ndio imeungua ila atafungua valve yote na huenda akakupiga bei ya valve mpya kabisa.

Fundi ujenzi anasema mifuko ya siment 20 then anatumia 10 au 15 mitano yake, nondo bati ndio usiseme, unaweza wekewa nondo mbili wakati hesabu ni nondo nne au tatu.

Hii sio kwa kampuni wala watu binafsi, wengi wao ni shida tupu.

Kwanini hivi? Binafsi ni bora uniuzie kitu bei kubwa ila usinifanyie magumashi huwa nakuwa na hasira sana. Kuna muda hadi natamani niwe na gun [emoji379]

Hii ni tabia yetu waafrica na inaturudisha nyuma sana. Tumelelewa hivyo na tunawarithisha wototo wetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom