Kwa nini watu wengi sio waaminifu?

Kwa nini watu wengi sio waaminifu?

sanalii

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,743
Reaction score
6,237
Ni jambo la ajabu na linatia hasira sana.

Unapita sokoni unamwambia muuzaji niwekee nyanya au machungwa nk, usipoangalia unafika home nyingi zimeharibika kabuvisha.

Mama ntilie anakuuzia maziwa ukitia mdomoni ni maji tu hamna kitu. Kwanini asiwe bei kubwa ila maziwa ya kueleweka?

Fundi magari, kwa mfano unapeleka gari kwa fundi, tatizo ni break, anagundua labda fuse ya magneto ndio imeungua ila atafungua valve yote na huenda akakupiga bei ya valve mpya kabisa.

Fundi ujenzi anasema mifuko ya siment 20 then anatumia 10 au 15 mitano yake, nondo bati ndio usiseme, unaweza wekewa nondo mbili wakati hesabu ni nondo nne au tatu.

Hii sio kwa kampuni wala watu binafsi, wengi wao ni shida tupu.

Kwanini hivi? Binafsi ni bora uniuzie kitu bei kubwa ila usinifanyie magumashi huwa nakuwa na hasira sana. Kuna muda hadi natamani niwe na gun 🔫
 
Huwa inaumiza sana, mie kama nanunua ni sokoni namwambia nimeacha watu wengi nanunua kwako sasa niwekee malimbofu siku nikija hapa nakupasha na sinunui tena!
 
Mfanyabiashara huyu mdogo anaona jinsi wakwapuaji wa rasilimali zetu wanavyolindwa, wapiga-dili, wahujumu-uchumi, wazembe kazini, wabadharifu wa mali za umma, wachochezi, madalali, makuwadi, mamluki, vibaraka, wapiga-upatu wa mabeberu na wanyonyaji wanavyotetewa tena na self-proclaimed mawakili nguli --- sasa hilo linawakasirisha sana sana sana wafanyabiashara wetu wadogo. And it's quite understandable when you really think about it.
 
Unaweza kuwa umekulia kwenye mazingira magumu sana na bado ukawa mwaminifu
Huo ni ujinga tu na kutokua na hofu ya mungu
Kuna sehemu nimesema mtu akikulia kwenye mazingira magumu ndio anakua sio muaminifu?

Au wewe unajua watoto wa kishua ndio wenye maadili?
 
Mifumo yote Karibia ndivyo ilivyo mwajiri kila kila kukicha anapanga amdhulumu mwajiriwa, mfanyabiashara anapanga amdhulumu mteja na mteja anapanga amdhulumu mfanyabiashara, mtoa haki anapanga kumnyima haki anayestahili, mfanya maamuzi analenga awakandamize watu wake manufaa yaende upande wake. Hivyo ndivyo ilivyo.
 
Hata wewe sehemu yako ya kazi yawezekana unapindisha baadhi ya mambo ili ujipatie kipato/faida zaidi. House girl nyumbani kwako pia anafikiria atakupiga vipi anapoenda kununua mahitaji sokoni.
 
Hata wewe sehemu yako ya kazi yawezekana unapindisha baadhi ya mambo ili ujipatie kipato/faida zaidi. House girl nyumbni kwako pia anafikiria atakupiga vipi anapoenda kununua mahitaji sokoni

Ni mwendo wa "kupigana" tu kila mtu anapopata nafasi. Ki msingi jamii yote imeharibika, yawezekana hata huyo mleta mada ni mpigaji mzuri katika anga zake. Mwizi aibe yeye lakini asiibiwe yeye, mkuki kwa nguruwe.

Tumuulize kama akiokota sh 50,000/= njiani ataipeleka wapi? Nataka naye tumpime uaminifu wake.

"Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake".

Ni ✊🏻 tena.
 
Na malezi yenyewe ya fimbo asubuhi mpaka jioni lakini maadili bado ni sifuri!!

Mi huwa najiuliza wachina na wajapan waliweza vipi kuwafanya watoto wao wawe na adabu bila kutumia fimbo?
Kama baba mama wote ni waadilifu na wakatekeleza jukumu la malezi kwa uadilifu, hata watoto watakuwa waadilifu.
 
Kama sarikelo(popote dunian) ilioundwa na jamii na yenye watu pevu kuliko waliowengi, na ndio inayotegemewa kusimamia haki, kuwalinda wanyonge, au maskini na ni ya wananchi wenyewe inaamua kufanya ulaghai(rushwa, deal) wa mchana kweupe mbaya zaidi kwa wananchi wake

Je, huyo mtu mmoja mmoja atafikia wapi?
 
Na malezi yenyewe ya fimbo asubuhi mpaka jioni lakini maadili bado ni sifuri!!

Mi huwa najiuliza wachina na wajapan waliweza vipi kuwafanya watoto wao wawe na adabu bila kutumia fimbo?
Huitaji fimbo wala. Mi sijapigwa pigwa utotoni ila nidhamu ninayo sana esp. nikikutana na watu waliostaarabika.
 
Siku hizi mtu anaweza akaiba kazini kufika nyumbani anajisifu mbele ya waif na watoto. Unategemea Nini kutoka kwa hao watoto.
Mke anachepuka Kisha anajisifu kwa ma shosti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom