Hakuna asiyewapenda wana usalama isipokuwa wananch wanawaogopa polisi na sio kuwachukia,sababu ni nyingi sana,kwa uchache tu ni kwamba polisi wamekuwa wababe wanajiona wao ndio wenye nchi hasa wanapoingilia mikusanyiko halali kama maandamano na kadhalika.Wanapo amrishwa kufanya jambo fulani huonekana kutotumia busara zaidi ni nguvu kupita kiasi ,hii hupelekea kuogopwa sana na wananchi hata katika mazingira ya kawaida,wanaonekana watu wasio jiendesha wenyewe,wanaweza kukugeuka wakati wowote wanapopewa amri na wakubwa wao.Mnaweza kuwa katika maongezi lakini ghafla anaweza kukugeuka anapopewa amri ya kufanya lolote.