Kwa nini Wasabato hawaruhusu wanawake kuwa wachungaji wakati mwanzilishi Hellen White mwanamke?

Kanisa la sabato mwanzilishi mwanamke. Vitabu wanavyotumia vya huyo mwanamke Helen White. Kwa nini hawawapi uchungaji wanawake? Wakati huyo Mama White ndie mhimili wa imani Ya kisabato?
Umeshawahi kukutana na Sheikh mwanamke mkuu?
 
Sio tu kuwa mchungaji. Mwanamke akiwa kwenye siku zake utakiwi kumsongelea. Sembuse kuwa mchungaji
 
Mwite vyovyote utakavyo ninachojua Alikuwa kiongozi mkubwa wa kisabato ambaye mafundisho yake ndio msingi wa sabato. Swala lini sabato watawapa wanawake nafasi za uongozi za juu za kuwa viongozi wakuu wa sabato kanisani mkoani au taifa au duniani Kama wachungaji maaskofu nk ambao wanawasimamia na wanaume yaani vidume vinapiga saluti kwao Kama ambavyo wanapiga saluti kwa mwanamama hellen White. Kama mwanamama Helen white anaweza kwa nini binti zake wasipewe nafasi za kuonyesha uwezo wao?
Usilolijua ni usiku wa giza
 
Wasabato ni kutoka Eden siyo kikundi Mtani kauli yako si nzuri
Eti ehh...Ndio maana tunasema Wasabato siyo Wakristo...Ni kikundi kinachopenda kujiita na kujifananisha na Wakristo

Ngoja nikuweke sawa
Waanzilishi wa Kikundi cha Kisabato
William Miller(1843)
Joseph Bates na Hiram Edson
John Snow......Kisha Wakafuata hawa

James White na Mkewe Ellen G White

FYI: hao viumbe niliowataja hapo juu hakutokea wenyewe, walikuwa kwenye makanisa yao ya Awali ya Baptist na Methodist

Sasa hiyo Eden yako ni ya wapi...?? Au kule Massachusset alikozaliwa Miller ndo Eden...??
 
Wasabato ni kutoka Eden siyo kikundi Mtani kauli yako si nzuri
Kingine , Wasabato ni muunganiko wa Vikundi vitatu vya Kiharakati(The Millerite mvt, Joseph na Hiram Mvt, Kisha EGW Mvt)

Vikundi hivyo vikaungana kutengeneza Kikundi Kimoja kilichoitwa SDA....Hivyo SDA siyo Kanisa ni Kikundi..
 
Uwe makini kwani hata Yesu hakua na mtume mwanamke, huenda dini zimesukwa tu, samahani kwa kusema kikundi cha brotherhood
 
WAROMA MTAENDELEA KUBURUZWA MAANA MNAFUNDISHWA NA WALEVI ,

BIBLIA INASEMA SABATO NI YA BWANA, HIVO KANISA LA SDA LIPO TOKA EDENI

SIKU YA BWANA NI IPI?
Siku ya Bwana ni jumamosi. Ufunuo.1:10 Yohana alipata maono ya kitabu cha ufunuo katika siku ya BWANA, anasema, “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu kama sauti ya baragumu.” siku ya Bwana inayozungumziwa hapa ni jumamosi si jumapili maana Yesu anajiita kuwa yeye ni BWANA WA SABATO. Mark.2:28, “Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.” Katika Isaya.58:13 biblia inasema “Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA ya heshima; ukiitukuza kwa kutozifanya njia zako mwenyewe, wala kuyafata yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe.” Pia katika Kutoka.20:10, inaongeza kuwa ”lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako,…..” katika mafungu haya ni wazi kuwa agano la kale na jipya liliitaja siku ya jumamosi kama siku ya BWANA wala si siku nyingine yoyote. Jumamosi ni siku ya Bwana, ni siku ya utakatifu wake, ni sabato ya BWANA, Mungu wetu.

d3d43788609a23b5dc711fa4c7c9a0c9.jpg
 
Mimi nimezaliwa na kukulia katika imani hii ya kisabato ila kuna kipindi kilifika nikawa najaribu kujihoji kuna vitu nikawa sivielewi.Inshort wasabato wengi ni watu ambao ni kama wana mental slaves na conferences zikiwa slave masters.kitu kilichonikera zaidi kwa wasabato mpaka nikapunguza kwenda kanisani ni kushindwa kumuhubiri Mungu na neno lake badala yake ni kupondaponda makanisa mengine especially RC.kuna siku nilicheka mchungaji alisema eti papa amemukufuru yesu kwa kusema kazi ya yesu msalabani ilifeli ila nilipoitafuta kauli ya papa Francis ni kweli alisema ila alichokuwa anamaanisha ni tofaut na upumbavu ambao mchungaji aliwaaminisha mental slaves wengi wa kisabato

Sent using Jamii Forums mobile app
watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa NO RESEARCH NO TALK. Unapotoa.hoja toa na udhibitisho uzuri Dini zote ni recorded jaribuni kumuomba mungu mwenyew awape ukweli lkn mda si mrefu haya yatakuwa ndo ushahidi mbele za mungu
 
Back
Top Bottom