Kwa nini Wasabato hawaruhusu wanawake kuwa wachungaji wakati mwanzilishi Hellen White mwanamke?

Soma Timotheo wa kwanza sura ya 3(soma sura nzima), wanapenda kuitumia sana.
Mwanamke kuhubiri si lazima asimame madhabahuni aweza hubiri kupitia mahubiri aliyoandika. Sasa Kama wanatumia mahubiri aliyoandika kwenye vitabu vyake Kama yalivyo si ni huyo Mama anahubiri? Ni sawa na kuandikiwa hotuba ya kiongozi ukaambiwa uisome kwa niaba yake!!! Sasa Kama kila sabato inasomwa hotuba ya Mama kwa nini wasiruhusu Mama Na akina Mama wenyewe wasimame wahubiri badala ya mahubiri yao kusomwa kwa niaba Yao na wanaume yawe ya Hellen White au mwanamke yeyote?
 
samahani sijaelewa

Kwamba Wasabato wanatumia maandiko ya mwanzilishi wao na siyo Biblia?
Wanatumia Biblia na vitabu vyake huyo Mama kwa pamoja. Kuijua imani ya kisabato lazima usome vitabu vya mheshimiwa Mama Helen White hutakiwi kusoma biblia tu.Lazima ujipinde hasa usome vitabu vya huyo Mama. Na kila msabato lazima asome vitabu vya Mama iwe kanisani au vyuo vya Sabato.
 
Elewa vizur Helen hakuwa mchungaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwite vyovyote utakavyo ninachojua Alikuwa kiongozi mkubwa wa kisabato ambaye mafundisho yake ndio msingi wa sabato. Swala lini sabato watawapa wanawake nafasi za uongozi za juu za kuwa viongozi wakuu wa sabato kanisani mkoani au taifa au duniani Kama wachungaji maaskofu nk ambao wanawasimamia na wanaume yaani vidume vinapiga saluti kwao Kama ambavyo wanapiga saluti kwa mwanamama hellen White. Kama mwanamama Helen white anaweza kwa nini binti zake wasipewe nafasi za kuonyesha uwezo wao?
 
Mwanamke kuhubiri si lazima asimame madhabahuni aweza hubiri kupitia mahubiri aliyoandika. Sasa Kama wanatumia mahubiri aliyoandika kwenye vitabu vyake Kama yalivyo si ni huyo Mama anahubiri? Ni sawa na kuandikiwa hotuba ya kiongozi ukaambiwa uisome kwa niaba yake!!! Sasa Kama kila sabato inasomwa hotuba ya Mama kwa nini wasiruhusu Mama Na akina Mama wenyewe wasimame wahubiri badala ya mahubiri yao kusomwa kwa niaba Yao na wanaume yawe ya Hellen White au mwanamke yeyote ?
Hiyo sura imeisoma lakini?
 
Kibiblia Mwanamke Hana jukumu la Kufundisha.
Ila shetani amekuwa akiongoza makanisa kwenda kinyume na maandiko.
Hellen Gould White alitabiriwa Katika Ufunuo 2:20 Hata hivyo, nina jambo hili dhidi yako, kwamba unamvumilia yule mwanamke Yezebeli, anayejiita nabii, naye anafundisha na kuwapotosha watumwa wangu wafanye uasherati na kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu
 
Wasabato sio kwamba wanatumia vitabu vya Mama Ellen White Kama mbadala wa biblia, bali vinatumika kama vitabu vya ziada kutoa uelewa wa mambo yaliyo kwenye biblia. Ni sawa na mwalimu wa phyisics kuandaa notes kwa lugha rahisi toka kwenye abbot. Then wasabato wanawake wapo wanaopanda mimbarani na kuhubiri. Kwa Mfano pale magomeni mwembechai jumamosi ya tarehe 26 August alihubiri mwanamke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke kuhubiri si lazima asimame madhabahuni aweza hubiri kupitia mahubiri aliyoandika. Sasa Kama wanatumia mahubiri aliyoandika kwenye vitabu vyake Kama yalivyo si ni huyo Mama anahubiri? Ni sawa na kuandikiwa hotuba ya kiongozi ukaambiwa uisome kwa niaba yake!!! Sasa Kama kila sabato inasomwa hotuba ya Mama kwa nini wasiruhusu Mama Na akina Mama wenyewe wasimame wahubiri badala ya mahubiri yao kusomwa kwa niaba Yao na wanaume yawe ya Hellen White au mwanamke yeyote ?
Mchana kuna mtu alianzisha Uzi "Ungependa kuonana na mwanaJf gani kabla ya kifo chako?" Nilikutaja kwa sababu nataka niongee na wewe live nipime kama udhaifu unaouonyesha kwenye maandiko ni huohuo hata kwenye maongezi? Yaani hoja yako ni kwamba Hellen G. White vitabu vyake vinaposomwa makanisani anakuwa amehubiri yeye? Hoja dhaifu kiasi gani hii!! Wakatoliki hawana Padri wala askofu mwanamke, lakini kuna siku wanasoma maandiko katika kitabu cha Esther , Je. Hapa Esther anakuwa Padri Wa Kikatoliki? Ninachojua Wasabato wanamchukulia Hellen kama nabii na siyo kuhani. Kasome maana na majukumu ya nabii na kuhani upate tofauti zake halafu rudi tena.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Back
Top Bottom