Haya mambo hayana jibu moja.
Kupigwa kwa mwanamke hutokana na sababu na vigezo vingi vyote ambavyo hubebwa tokana na mwanaume mwenyewe (mpigaji) na mwanamke mwenyewe (mpigwaji).
Hasira na namna ya kutatua matatizo hutofautiana kwa kwanaume. Kuna wale ambao akikerwa unavunja vyombo, kuna anae peleka hasira kazini, kuna anae zielekeza kwake mwenyewe na kujilaumu kua na mwanamke kama huyo na kuna anae zipeleka kwa mkewe mwenyewe (kwa kumdunda).
Kumbuka pia kua hasira zimetofautiana. Kuna yule ambae akiwa na hasira uwezo wa kupima matendo huwa ndogo sana, sawa na akilewa, yaani yeye hu react mara moja na hujikuta tu kisha piga na baadae kujutia tendo la kupiga; ingawa wengine hufurahia na kuona ni sawa tu kupiga.
Ukija kwa wanawake ambao wanapigwa, wengi ana huonewa sababu tu hawana nguvu ya kujikimu kuto kupigwa na hali hapo hapo kuna wanawake wanamaudhi hata mwanamke mwenzie watamani umchape kama mtoto mdogo.
All in all nadhani kuwa makuzi, mazingira, malezi, Uwezo, mila na desturi ni maeno tuliyokulia huchangia sana mwanaume kuwa mpigaji ama kutokua mpigaji. Mwisho wa siku its not black and white - haina majibu ya moja kwa moja, kila case ina sababu zake.