Kwa nini vijana wa kibongo hamfikiri?

hata pesa zenyewe wakipata wanaishia kuzitumia kwa anasa tu bila kujijenga kimaisha.
 
Kuna mpuuzi mmoja humu leo eti kaniambia Sharo Millionea ndio role model wake, sasa usitalajie kitu cha maana kutoka kwa hawa Watoto.
arifu inasikitisha sana....na hao ndio utasikia jamaa kaenda shule huyo tena udsm kafaulu vizuri na first class ana background nzuri ya spesho skuli ilboru.....arifu unategemea kijana huyo atakaa na kijana wa korea au malaysia wakajadiliana kitu?mwenzakea anawaza ni vipi kama web developer atampiku Jack Dorsey twitter founder.....yeye msomi wa tanzania anawaza kuwa role model wa sharo milionea...ukimtazama huyo kijana atakuwa kavaa mlegezo kama role model wake....kavaa heleni anaongea kama kashuka marekani leo ili tu aimpress jamii fulani mtaani kwake..tunarudi kule kuleeeee apate mashori ajamiane nao atambe street basi tu......ujinga mtupu....

hivi tanzania tuna graduate wa MIT?
 
arifu inasikitisha sana....na hao ndio utasikia jamaa kaenda shule huyo tena udsm kafaulu vizuri na first class ana background nzuri ya spesho skuli ilboru.....

Hivi kuna 'special schooler' yeyote aliyesoma kwenye hizo 'special schools' za bongo aliyevumbua chochote? Halafu hizo 'special schools' zenyewe ukiziona hali zake....hmmmm.....ni spesho kweli kweli.

hivi tanzania tuna graduate wa MIT?

Nipo arif....MIT class of 2001, summa cum laude.
 
Hivi kuna 'special schooler' yeyote aliyesoma kwenye hizo 'special schools' za bongo aliyevumbua chochote? Halafu hizo 'special schools' zenyewe ukiziona hali zake....hmmmm.....ni spesho kweli kweli.
arifu wapo wengi mfano si mwigulu nchemba nasikia nae kasoma spesho skuli si unaona uvumbuzi wake arifu....wapo na wengine wengi tu fuatilia thread https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/20884-tujikumbushe-ilboru.html kisha angalia post za wana ilborian humu JF.....
 
Hapo umesema kweli mkuu, ila na elimu yetu nayo inachangia vijana kutokuwa wabunifu. Wengi wetu tunasomea kupata vyeti na sio ujuzi.
 
Yo Yo leo umetisha aise. Nakubaliana na wewe kabisa
Matola mkuu umeua aise role model wake ni sharo ina maana mpaka kuvaa au kutembea
Kwa nini isiwe Mark mwanzilishi wa facebook au Bill au Mandela au usiende mbali vijana kama John Mnyika au January Makamba hata kama si kwa kufuata itikadi zao ila at least kuwazia siku moja kuwa kama wao kimaisha kwa kupambana
Unawaza kuwa kama sharo zaidi ya kunywa na kutembea na wawake wengi na kuwaza kuwa na kiGX100 na chumba cha kupanga mitaa ya sinza ni nini
 
Last edited by a moderator:
ni kweli ndugu ila huu mfumo wa elimu wa kizungu umetuathiri sana, yaani kila mtu anawaza kuajiriwa(essp. graduates). na jamii ikimuona graduates either amefungua duka au saloon au hata kuuza mkaa wa jumla inamshangaa eti hizo sio kazi za wasomi, matokeo yake wasomi wamebakia kunywa pombe na mademu, mkuu umeongea ukweli na wengi umewagusa hata humu jf, ila kwa kujishaua wanajifanya eti wanakupa tano.
 
mkuu yoyo nimekupata vizuri sana..ni ujumbe mzuri

hii mada ni pana sana na umegusa maeneo mengi ambayo ni nyeti..kwa kifupi maisha hayana formula maalum..ingawa mara nyingi kwa nature ya binadamu hasa wa nchi maskini kama ya tanzania tunastrive kupata zile basic needs kwenye level isiyo sahihi (graduate) imagine hadi unamaliza chuo hukuwahi kushika gari,kumiliki japo chumba kimoja cha kupanga na mambo mengine kama hayo..........so graduate anatumia muda mwingi kupata iyo basic need ambayo mtu wa chini maskini asiye na elimu hakupata..... tunatumia muda mwingi kujipanga na kutimiza basic needs kutokana na nature ya maisha yakimaskini na utegemez yanayotuzunguka...imagine amepata kazi,ajipange basic needs,may be aoe,atafute kiwanja ajenge..akishajenga alee watoto including kuwasomesha apo bado una ndugu lukuki wanakusubiri...ni saa ngapi utatuliza kichwa purposely kufikiri kwa namna iliyo positive...si kwamba haiwezekani kuwaza na kucreate,ila maisha halisi yanawabana walio wengi..unakuja kupata akilia sahihi may be at ur level...ukute yoyo maisha yashamshinda anabaki na stress!!.........nina mengi ya kuweka apa...ila muda...kuna vijana ni wala bata mwanzo hadi uzee wao..wewe unaewaza creativity unakufa njaa na familia yako.life aint fair sometimes
 


kwani walioko maofisini wote....wanaovaa shati na tai..na wanaenda posta .wana akili za chuo .....hebu acheni ushamba kuna watu hawajasoma hata darasa moja na ni ma boosii maofisini
 
Ni kweli mkuu,hawa vijana wana matatizo makubwa! Umewapa makavu ya ukweli bt toa solution mkuu!
 
Not that I totally disagree with Yo Yo...

But I agree more with "Do You" my ninja.

Mtu akiamua kujinywea mipombe kivyakevyake poaa tu, almuradi haniingilii anga zangu. Pombe - za kweli, mi Johnny black, sio vi bordeline orange juice bia vyenu hivi- kazinywa Mkapa mpaka kalala fofofo Sea View pale, huku Mwinyi anamsubiri DIA. Kwenda state visit Saudi Arabia no less. Na kasubiriwa na head of state, hakufanywa lolote sanasana kazawadiwa urais. Na leo elder statesman anaitwa kusuluhisha migogoro.

Mtu kazi kafanya mwenyewe, hela zake mwenyewe, siwezi kumpangia maisha. Kama kaiba that's another matter, kama anavunja sheria that's another matter, lakini kapata kihalali? Hata akienda cordless bungee jumping kwenye concrete parking lot poa tu.

Nitampangiaje maisha wakati sijui kama anataka kuishi maisha marefu au hataki?

Sio kila mtu anataka kuishi mpaka awe mzee, wengine wanataka kuishi maisha ya ki 2Pac, mafupi halafu matamu, wawaachie wengine, in keeping with ethical environmental recycling standards.

Or simple Darwinian instincts, which should mean teir "suicide by alcohol" is to be celebrated, it leaves you who want to live long with more.

Kikwete kawaambia muache kuzaliana juzi hapo, labda wengine wanataka kumsaidia kwa kujiua kwa mipombe na minyama na mingono zembe na mijivuno iso msingi etc.

Just do you already.

Else they will call you a hater, rightfully.

Enough with the preaching.

Take it from Papa Kiranga Makarios Pazi himself.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…