kwa nini Tunaoa/kuolewa?

Nikianza na kidini kwa sisi waislamu katika Quran tukufu kuna aya inasema kabisa kwamba "Wao (wanawake) ni vazi lenu nyinyi wanaume na nyinyi (wanaume) ni vazi lenu hao(wanawake)"..sasa vazi kazi yake ni kusitiri hakuna asiyelijua hilo..kwa hiyo hii inamaanisha kwamba ili usitirike katika hii dunia lazima binaadamu apate mwenzi wake kwa uhalali wa ndoa kwani bila ndoa pia hakuna sitara na hii inathibitishwa na hata jamii yenyewe. Mfano wasiooana majina kama vimada, ana nyumba ndogo n.k hutumika kuonyesha ubaya wa haya na athari ya kipatikanacho pia yaani mtoto hupewa jina la mtoto haramu au wa nje ya ndoa.hiyo yote inaonyesha kuwa hata ukiwa na mwanamke/mwanaume bila ndoa bado hujasitirika.

Tukija kimwili na kiafya zaidi
1. Kama miiko na mipaka ya ndoa itazingatiwa basi lengo la ndoa litatimia ambao ni kupata tulizo la nyoyo kwa wale waoanao
2. Kutokuwa na wasiwasi na ukifanyacho.mfano huhitaji kujificha katika jamii kama upo na mkeo lakini ukiwa na kimada au haupo kwenye ndoa wasisiwasi hutawala usije onekana...usije pata mimba n.k.
3. Wanaofanya tendo pa ndoa wakiwa katika ndoa wanapata faida ya hili tendo zaidi ya wale wafanyao nje ya ndoa kwani walio nje ya ndoa hulifanya huku wakiwa wametawaliwa na khofu n.k. na hivyo kufanya liwe na madhara kwa wahusika .Kama unabisha fanya utafiti juu ya hili.
4. Kuwa na kitambulisho mbadala katika jamii.Alieoa kwa kawaida hata asipokuwepo mahali akihitajika akiwakilishwa na mke/mume hakuna atakayekuwa na shaka au wasiwasi ila hali ni tofauti kama ni kimada au jamaa tu msiyeoana

NB: Faida zipo nyingi sana na hizo ni baadhi ila nisiwachoshe kwa uzi mrefu na hapa nilipo pia vidole vinauma kwani natumia simu.Kwa wanotaka faida zaidi naomba wani PM

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom