Kwa Nini Timu za Tanzania Zinakwenda Uturuki?

KIKOSI cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kimesafiri kwa zaidi ya saa 10 hadi katika mji mdogo kabisa wa Kartepe hapa nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi.



Kambi hiyo ni kwa ajili ya kujiwinda ili kuwa fiti kabla ya mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa aAfrika dhidi ya Nigeria, mechi itakayopigwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.


Kabla haitakuwa mechi ndogo na Stars ambayo kwa mara ya kwanza, mara nyingine timu hiyo inanilewa na makocha wote wazalendo.


Safari:
Safari ya Stars kuja hapa Uturuki ilianzia Dar es Salaam na ndege iliondoka saa 9:45 usiku na kuwasili Istanbul Uturuki saa 4:45 asubuhi ikiwa ni saa saba bila ya kupumzika angani.


Safari hiyo ndeefu iliwafanya wachezaji wa Stars kuonekana wakiwa wamechoka sana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ataturk na baada ya hapo safari ya kwenda kambini iliyochukua saa tatu na shee ilianza kwa basi.


Awali ilionekana ni kama safari fupi tu, lakini haikuwa hivyo baada ya wachezaji kujikuta wakisafiri kwa saa tatu kutoka Istanbul hadi katika mji wa Izmil ambao ni wa tatu kwa ukubwa hapa Uturuki baada ya Istanbul na Ankara.
 
Kambi:


Bado Stars hawahaweka kambi mjini, badala yake wamepanda katika milima iliyo nje ya mji huo katika eneo linalojulikana kama Kartepe ambako kambi hiyo iko katika Hoteli kubwa ya The Green Park.


Kwa Dar es Salaam, The Green Park Hotel ni mfano wa Serena Hoteli, lakini hii ya hapa Uturuki ni kubwa mara tatu ya Serena.
 
Hali ya Hewa:
Hali ya hewa ya hapa ni kiboko, baridi ni kali kwa kuwa ni kuanzia nyuzi joto 12 hadi 14. Siku moja kabla ya Stars kuwasili, mvua zilinyesha mfululizo kwa saa 72.


Lakini tokea timu imewasili hali ya hewa si ya mvua tena, lakini baridi na hasa unapowadia usiku, inakuwa kali zaidi.
 
Uturuki wamejipanga kwenye suala la utalii wa michezo (Sports Tourism). Kutokana na kuwa kati ya mabara mawili, Asia na Ulaya na miundo mbinu mizuri timu nyingi huwependelea kuweka nchini Uturuki.
 
Back
Top Bottom