Kwa nini tarime tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tarime tu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mosachaoghoko, May 29, 2011.

 1. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu Wana jamii forums kuna haja wale ndugu zetu walioko kule Tarime kuwasaidia kujua wao ni raia wa nchi gani hapa A.Mashariki maana wananyanyaswa kama sio watanzania ,wana baguliwa ,wanaonewa ,wanapewa kila aina ya majina ya ufedhuli, mara majambazi ya kuvamia mgodi wanauawa na serikali ya Tanzania ,wanapigwa na kubambikizwa kila aina ya vyesi na kingine ambacho ni kibaya zaidi hata pale ndugu zao wanapokuwa wameuawa na polisi wa tanzania kule Nyamongo wanalazimishwa kuchukua miili ya waliouawa na kwenda kuzika na endapo watakataa kutekeleza amri ya polisi watakamatwa waombolezaji na marehemu kuchukuliwa na polisi na kutupwa barabarani ,je kwa mwendo huu hawa wakiomba wao kuhesabiwa kama sehemu ya kenya kama sio kujitenga na kuanzisha Taifa lao ili wajitawale waweze kupata serikali itakayowajali na kuwahudumia kama binadamu wengine
  Tafakari ni mipaka kiasi gani wana wekewa ndani ya nchi yao {barrier}kule kirumi chochote kinachoenda Tarime kutokea mwanza lazima kiwe na kibali kana kwamba labda wanavusha kutoka Tanzania kwenda either kenya ama nchi ambayo bado haijapata uhuru wake {Tarime}
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,814
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  kenya kuna mbuga inaitwa masai mara, haina uhusiano na huko tarime, naona jamaa hawana maadili ya kitanzania kabisa. kama nyerere asingetokea kule watu wale leo hii sijui wangekuwaje! wako ngangari ikinoma
   
 3. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #3
  May 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbukeni siku mula akisema kali hayo kitakuwa ni kilio cha ukusinsiga ne elonge
   
 4. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu NDumbayeye unamaanisha nini hasa unaposema eti watu wa Tarime hawana maadili ya ki-Tanzania?? Nadhani ungekuwa kwnye viatu vyao ungeelewa vizuri maana ya kuonewa, hebu fikiria umefiwa na kaka yako au dada yako, tena kauawa na serikali kisha serikali hiyo hiyo inabeba maiti inakuja inaitupa barabarani, how would u feel mkuu??
   
 5. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chukulia kuwa hili limekukuta wewe hili utafanya je
   
Loading...