Kwanini Tanzania Kifaransa kilipewa kipaumbele kufundishwa na siyo Kihispania?

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,444
8,291
Kitu huwa nashindwa kuelewa Kwa Nini vijana wetu tunalazimisha kujua lugha ngumu ya kifaransa.

Katika lugha rahisi kujifunza ni kihispania ndiyo ya Kwanza duniani kwa urahisi.

Lugha ya kifaransa inaeleweka mno hasa Kwa Swahili na English speakers, maana maneno Yake unatamka au kusoma kama yalivyoandikwa.

Kwa ufupi kifaransa na Kiswahili matamshi yake yako karibu mno. Bora vijana wangefundishwa español badala ya kifaransa wangeelewa haraka Zaidi.

Kwenye español herufi "J. H, Y. LL" ndiyo yanamatamshi tofauti Lakini mengine yote ni kama yalivyoaandikwa.

Naomba nikupe misamiati michache.

1. Table Kwa Kiswahili ni Meza Kwa español ni 'Mesa' inatamkwa kama ilivyo.

2. Jina Kwa español ni Nombre na inatamkwa kama ilivyo.

3. Man Kwa español ni "Hombre"na inatamkwa kama ilivyo. Hiyo ni mifano michache sana mingine tafuta mwenyewe uone ilivyo rahisi.

4. Dress Kwa español ni 'Vestido' unaisoma kama ilivyo.

Kwa kifupi español ni rahisi sana kusoma na kuandika Hata kutamka pia, Kwa Nini tuliingiza somo la kifaransa kwenye mtaala wetu na Siyo español.

Swali watangulizi wetu hawakuona ukaribu wa lugha hizi mbili?

Kingine español inawazungumzaji wengi kuliko kifaransa.

Nakutajia nchi zunazozungumza spanish.

1. Spain
2. Chile
3. Mexico
4.Argentina.

Nje ya mataifa haya wazungumzaji pia ni wengi sana Huku kifaransa kikizungumzwa haswa France na Canada tu.

Hata UN español ni lugha ya pili baaada ya English

Je, kulikuwa na sababu ipi ya msingi kufundisha kifaransa Badala ya español?
 
Pamoja na kuwa Kispanish kina wazungumzaji wengi kama lugha ya kwanza pengine zaidi ya English, lakini hatuna mahusiano ya karibu katika nyanja nyingi zitakazofanya tuhitaji Kispanish.

Tanzania hakuna nchi inayozungumza kispanish ambayo tupo nao karibu Kiuchumi, kisiasa na hata kitamaduni.

Wepesi tu wa kujua lugha haiwezi kuwa sababu ya kutaka iingizwe kwenye mitaala yetu ya elimu.
 
Back
Top Bottom