Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Je, sisi asili yetu ni watu wazuri? Ukiangalia nchi yetu pmj na matatizo yoote ya Kiuchumi lkn bado ni nchi yenye Amani na Utulivu kabisa, hakuna mauwaji ya mara kwa mara ya kutisha kama nchi nyingine, binafsi naweza kwenda popote bila ya shida kuanzia Mwananyamala, Mburahati hadi Temeke hakuna no go zones kama nchi za USA, baadhi ya nchi za Ulaya kama Ubelgiji, Uingereza, Italia, au Ufaransa, Brazili na kwingineko!
Kwa mfano USA, Wamarekani waliouliwa kwa kupigwa risasi na Wamarekani wenzao ndani ya USA ni zaidi ya Wamarekani waliouliwa vitani yaani Syria, Iraki, na Afghanstani!
Hata hapa Afrika ukiangalia nchi kama Nigeria, Kenya, AK kote kuna criminals gangs kama Mungiki ambao huvamia, kupora na kuuwa watu, lkn hapa kwetu ukiondoa wavuta bangi Panya road hakuna high crime, sasa ni kwa nini?
Kwa mfano Tanga kuna sehemu nilikwenda nikakuta Ndoo ya maji nje ya Nyumba za watu pmj na glasi/kikombe cha kunywea maji, yaani wewe kama mpita njia ukisikia kiu unakunywa na kuendelea na safari yako bila ya kumsemesha mtu wala kulipia chochote kile, hii sijawahi kuona nchi nyingine!